Ogopa Mgomo Baridi: Muhimbili hakufai

Ogopa Mgomo Baridi: Muhimbili hakufai

Budget ya Tanzania: 70% ya uendeshaji wa serikali, 30% ya maendeleo..! Kweli ari zaidi, nguvu zaidi, kasi zaidi. Mungu tusaidie watanzania

Kwa kweli inataka moyo!!!
Unafanya biashara halafu mtaji 70Shs kwa faida shs30. Na una wachumi first class!!!!!!
Guiness books of records hawana habari hii???
 
JUMATANO, JULAI 25, 2012 04:47 ELIZABETH MJATTA NA ASIFIWE GEORGE, DAR ES SALAAM

WAKATI serikali ikiamini adaktari wamerudi kazini, hali ya matibabu katika Hospital ya Taifa Muhimbili imezidi kudorara. Akizungumza na MTANZANIA katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mmoja wa madaktari (jina tunalo), alisema licha ya madaktari kurudi kazini hali ya matibabu imezidi kupoteza mwelekeo tofauti na hali halisi.

"Huwezi kusema madaktari wamerudi kazini wanatoa huduma…hii siyo kweli, kwa sababu madaktari bado mahitaji yao ya msingi hayajatatuliwa..huwezi kuwa na daktari mwenye manung'uniko kazini, halafu ukasema anatoa huduma bora kwa mgonjwa,

"Mimi nasema ukweli, hospitalini kuna huduma duni zisizokidhi mahitaji ya wagonjwa,nikizungumza kama mwananchi wa kawaida ni kwamba madaktari wanaingia kazini na kusaini lakini hawatoi huduma vizuri," alisema

"Nawashangaa Watanzania, sijui kwanini wanashindwa kudai haki zao..ukiingia hospitali hazina vifaa lakini utashangaa watanzania wako kimywa,sisi madaktari tukigoma tunaonekana wabaya," aliongeza daktari huyo.

Akizungumzia hali ya huduma pamoja na nia ya kufanya maandamano, Katibu Mkuu wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT),Dk. Rodrick Kabangila alisema nia ya maandamano ipo palepale.

"Niseme nia yetu ya mgomo ipo palepale, lakini sasa hivi tunashughurikia suala la ‘Intern's kwani suala hili limeingiliwa na masuala ya kisisa kidogo..kwahiyo ndiyo tunahangaia nao kwanza halafu tutatoa taarifa lini maandamano yetu yanafanyika hivi karibuni,

"Hili suala la Interns, limeingizwa siasa sana kwasababu huwezi kusema unamfutia leseni wakati yeye hana kosa…Serikali ilitaka huyu interns, afanye kazi na nani wakati madaktari ambao ndiyo wanamsimamia yeye walikuwa kwenye mgomo," alihoji Dk. Kabangila.

Alisema malalamiko yao bado yapo palepale na Baraza la Madakatri Tanganyika haliwatendei haki kwa sababu lipo chini ya Serikali.

"Lile baraza lipo chini ya Serikali, unafikiri haki itatendeka kwetu kweli..sisi tunataka baraza ambalo mwenyekiti wake asiwe mwajiriwa wa Serikali..," alisema Dk Kabangila.

Akizungumzia hali ya Dk.Stevin Ulimboka,Katibu wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Edwin Chitage alisema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.

"Dk.Ulimboka anaendelea vizuri kwa sasa na anaendelea kufanya mazoezi ila siwezi kusema atarudi leo wala kesho…hizo taarifa za kwamba atarejea hivi karibuni zitakuwa zimezushwa tu na watu," alisema Dk. Chitage.

Alitaja baadhi ya hospitali kubwa alizodai kuathiriwa na tukio hilo la kufukuzwa kazi kwa madaktari, kuwa ni Muhimbili, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Bugando (Mwanza),KCMC (Moshi) na Hospitali ya Rufaa Dodoma.


Kutoka Muhimbili Hali ni mbaya... Wagonjwa wanalala mpaka Koridoni!!!





attachment.php



attachment.php



attachment.php



attachment.php



attachment.php



Serikali, Madaktari mnaona picha hizi? anayetaka kujua ukweli atembelee Muhimbili atajua ukweli wa mambo na kupata majibu kuhusu mgomo kama umeisha au unaendea?
Chanzo: Blog ya Chinga One













 
Nape Nnauye anatuambia huduma zimerudi Muhimbili; Ukienda Muhimbili na kidonda tu Unakufa, Malaria sio kali unapoteza

Maisha; Yeye yuko kigoma anatoa Misamaa kwa Nyanya, mchicha, vitunguu, kuwa hakuna kodi ukitozwa kodi

watamuona yeye... vitu vidogo anaweka MIGUU MIWILI; Issue ya Madaktari, huyoo kwenye ndege na vizee vyenye

vitumbo vya CCM na Serikali Mmoja wao kwa kulala bungeni Mpeni A++

* UKIANGALIA HIZI PICHA UTAAMINI TUNA GAS YA $ TRILLION 60 na zaidi?; Lakini Umuhimu ni kutembelea BALOZI

kuangalia UENDESHAJI, MAJENGO na MAHESABU na KUPIKIWA vizuri kweli kulikuwa na UMUHIMU huo; kwa tuseme ni

MGOMBEA 2015
Kama ni AMERICA, HIYO TU kwenye Campaign inaamsha wananchi Macho na kumnyima Kura; sio

kuimba CCM Ukiona DIAMOND ULINGONI
 
alafu maajabu sasa pamoja na kuonewa kote huku 2015 ikifika hawa hawa madaktari wataipigia kura ccm..
 
hali ya muhimbili inatisha jamani, viongozi wetu waanze kuwa na hofu ya kifo na mungu otherswise siasa hizi zinatupeleka pabaya
 
Inasikitisha sana...lakini hichi ndicho waTanzania walichokitaka. Ni bora kuwe na total shutdown kuliko hii hali, na ubaya nikuwa hamna anayejua itakwisha lini katika mazingira gani!
 
Kuna huduma ambazo lazma uende Muhimbili.
Tiba ya mifupa kwa mfano, tiba ya ubongo lazma uende Muhimbili.
Na inaonekana ni makusudi wagonjwa hawatibiwi.
Hizi ni wodi za upasuaji.
Hakuna dokta wa kupasua japo wanakuja kazini,
au japo wanapasua, ni kwa kusuasua mmoja kwa siku anapasuliwa alafu wanalazwa wagonjwa kumi.
Hebu tuone hali baada ya wiki mbili

Tumesikia Lugalo imepandishwa hadhi na kuwa hospitali ya rufaa! Huko hakuna huduma zilizotajwa hapo juu? Liwalo na liwe!:israel:
 
kwa kweli mimi siipendi sana hii serikali yetu nimeichoka mno ningekuwa na uwezo hata njama za kuipindua ningeunga mkono.
 
kwa kweli mimi siipendi sana hii serikali yetu nimeichoka mno ningekuwa na uwezo hata njama za kuipindua ningeunga mkono.

nani ataongoza mapinduzi wakati wanajesi wetu wenyewe wamechakachuka! Kuna enzi jesi ilikuwa jeshi! Walale pema wale waliotaka kufanya vitu vyao enzi hizo na wengine wakapoteza maisha.
 
Inasikitisha sana...lakini hichi ndicho waTanzania walichokitaka. Ni bora kuwe na total shutdown kuliko hii hali, na ubaya nikuwa hamna anayejua itakwisha lini katika mazingira gani!

umelazwa na fracture unaondoka na kifua kikuu!!


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Have said, and I keep on saying "Doctors are in the category of rare proffession, I can say". In view of this, much respect to them!!! Nyie mnapojilipa eti posho laki 200,000 bado sijui sitting allowance, halafu fuel over a million per month, na mambo kibao halafu eti Daktari alipwe 10,000 night call/shift sijui nesi 5,000 or so. Waliomba ongezeko la harship hasa ukizingatia hardship yenyewe inatokana na ukosefu wa vifaa. It is true Muhumbili hata na Hospital nyingine kama Temeke, Amana, Mwananyamala, etc wanafanya kuzuga tu na hakuna huduma nzuri kama humfahamu Daktari. Acheni kuwadanganya wananchi, mtalaanika. Nyie homa mnaenda India, Marekani, Europe and the like, sasa hawa wanaowapigia kura wataenda wapi? Ni mpaka wasubiri 5,000 ya kuuza kitambulisho cha mpiga kura na kanga, kofia na t-shirt only every five years!!! Do justice to your voters!!!
 
nikisema dhaifu ntapgwa bann nyingine sijui hii serkali tuiteje? hii hali sasa imekuwa ngumu
 
Mie nashangaa watu kushangaa. Serikali ilishatoa tamko kuwa LIWALO NA LIWE, au mlikuwa mnataka JKilaza mwenyewe ndiye atamke? Waziri Mkuu ni serikali pia....Very sad...oohh..LIWALO NA LIWE.
 
Tatizo ni sisi watanzania kuwa hatuna vision! MaDR wameanza harakati za kukomboa hali ya utoaji wa huduma za afya nchini!ebu angalia wagonjwa wamelala chini na wengine hata vigodoro hawana! Hata mahabusu hakuko hv! Wanalipeleka wp taifa hili?

Umegusa hasa kwenye kiini cha tatizo. Viongozi ni zao la jamii wanayotokea. Wengine huwafananisha viongozi na vioo vya jamii - yaani ili ujue jamii ikoje angalia viongozi wa hiyo jamii. Kama jamii imejaa ubinafsi na haina maadili usitegemee viongozi wawe tofauti.
 
nani ataongoza mapinduzi wakati wanajesi wetu wenyewe wamechakachuka! Kuna enzi jesi ilikuwa jeshi! Walale pema wale waliotaka kufanya vitu vyao enzi hizo na wengine wakapoteza maisha.

mkuu tatizo mfumo umejaa watu waoga wenye njaa na wasio wazalendo. naamini wachache wanaweza ongoza mapinduzi ya ukweli wakitokea hao lazima mapinduzi yaratokea.

Na mfumo lazima ubadilike uwe wa kujenga kizazi cha kuhoji kutokubali mabaya na uonevu wote.ili isiweshida kushawishi watu wenge zaidi. elimu,dini familia (jamii)zinachangia sana kujenga raia waoga na wanafiki.

Umasikini na njaa vinawalazimu watu kuwa waoga wa mabadiliko pia tukiytafanyia kazi haya machache japo makubwa mapinduzi yatakuja tu.

Hata mimi na wewe ni sehemu ya namba hiyo ya hao wachache kinachohitajika ni mipango yenye akili.
 
Back
Top Bottom