Ogopa Mgomo Baridi: Muhimbili hakufai

Sigma

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
5,006
1,254
Hii ndio hali ilivyo katika wodi za Muhimbili, pamoja na serkali kudai huduma kurejea kama kawaida.
Waandishi wa habari wanaweza kwenda kuwahoji wagonjwa wodi za SewaHaji ground floor.
attachment.php

Hapa ni mlango wa kutokea nje ya wodi
attachment.php

Juu: Hii ni korido inayounganisha wodi mbili
attachment.php

Baadhi ya wagonjwa walolala chini wakiwa hawana hata magodoro ya kulali
a.
attachment.php

Baadhi ya wauguzi wakiendelea kutoa huduma katika mazingira magumu
attachment.php

Hapo ni mwaisela
 
Hii serikali bwana
jamaa wanaomba kura kwa upole sana wakipata madaraka liwalo na liwe!
Kweli waziri mkuu unasema liwalo na liwe yaani uwezo wako wa kufikili umeishia hapo kweli!
Eeeeti mtoto wa mkulima!??
Dini gani mnasari ninyi akina pinda mbona ukristo haukubaliani na hayo mambo.
Atakuwa analaana la jina kapinda kweli!
 
Hali kama hii wodi kujaa serikali inaitafsiri kuwa huduma zimerejea.
Wao watu kummiminika kwa wingi hospitali na wodi kujaa ndo indicator ya huduma nzuri.
Serikali ya Kikwete na Pinda wanajua QUANTITY tu, QUALITY kwao msamiati.
 
Tatizo ni sisi watanzania kuwa hatuna vision! MaDR wameanza harakati za kukomboa hali ya utoaji wa huduma za afya nchini!ebu angalia wagonjwa wamelala chini na wengine hata vigodoro hawana! Hata mahabusu hakuko hv! Wanalipeleka wp taifa hili?
 
Wao wanawapeleka ndugu zao private na India,
Liwalo na Liwe na wewe Dhaifu, .
Mtendaji mkuu wa serikali, Pinda alithibitishia umma wa watanzania kuwa serikali haijali chochote kinachohusu wananchi wake, labda kwa kuwa 2015 bado mbali
 
Tatizo ni sisi watanzania kuwa hatuna vision! MaDR wameanza harakati za kukomboa hali ya utoaji wa huduma za afya nchini!ebu angalia wagonjwa wamelala chini na wengine hata vigodoro hawana! Hata mahabusu hakuko hv! Wanalipeleka wp taifa hili?
Hii yote serikali iliipindisha ikaonekana kuwa madokta wanataka mijihela tu!
 
Nimepata Taarifa kuwa hata Bugando uko wa kichinichini,ili upate huduma lazima uongee na mlinzi akutafutie Dr.te umpe kitu kidogo, vinginevyo utapoteza mgonjwa wako.
Nadhni ni nchini kote,
morali iko wapi?
Unaweza kulazimishwa kuja kazini, lakini huwezi lazimishwa kutibu mgonjwa
 
Jamani hivi neno MUHIMBILI linatokana na nini?? Kama halieleweki...tusistaajabu haya.
 
Miaka 51 ya uhuru bado Ujinga haujatutoka?
Wengi wetu tumezaliwa juzi hapa,
hata hivyo mawazo yetu yako nyuma ukaavyo mkia.

Tunawaza kuukata kwa vijirushwa mbuzi wakati wa uchaguzi,
ndoto zetu ni kuwa na fedha mifukoni,
ziwe za wizi au kukanyagwa yote sawa tu.

Vijana ndiyo chachu ya maendeleo,
lakini kwa mtaji huu tuna zidi kuchina.
 
yaani hata kununua vitanda vya wagonjwa wameshindwa?...kwanini tunawalipa posho na mishahara wabunge ambao hata bunge lenyewe huwaoni? pesa za misafara ya rais na kamati za bunge hizo zipo..pesa za kuunda tume za uchunguzi ambazo hazinaga majibu hata siku moja zipo...kuna wizara moja imetengewa zaidi ya billion 3 kwenye entertainment package, kwanini u entertain watu wakati hospital zetu wagonjwa hata magodoro hawana wanalala sakafuni....ONLY IN TANZANIA
 
Back
Top Bottom