Serikali: Hospitali ya Muhimbili kujengwa upya, itawekewa miundombinu ya kisasa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,832
141,749
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema hospitali ya Muhimbili imejengwa miaka 60 iliyopita na miundombinu yake imeelemewa kabisa.

Hivyo serikali itajenga miundombinu mipya na ya kisasa kabisa itakayokidhi mahitaji ya miaka 50 ijayo itakayojikita kwenye Ubingwa na Ubobezi.

=====

Muhimbili kujengwa upya
January 24, 2022

Na Sophia Mtakasimba
Serikali ina mpango wa kuijenga upya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la watu wanaofika katika hospitali hiyo kupatiwa matibabu pamoja na kuendana na kasi ya utoaji wa huduma bora za kibingwa na kibobezi

Hospitali hiyo ilianza kutumika rasmi mwaka 1905 ikilaza wagonjwa 1,013 kwa mwaka ukilinganisha na hivi sasa wagonjwa 3,400 wanaonwa katika hospitali ya MNH kwa siku.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu alipofanya ziara katika hospitali hiyo kwa lengo la kupata taarifa ya utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa, taarifa ya maendeleo ya hospitali, changamoto, mapendekezo na mikakati ya maendeleo ya baadaye iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali wa MNH, Prof. Lawrence Museru.

Baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya Hospitali pamoja na taarifa nyingine, Waziri Ummy Mwalimu amesema Serikali itajenga Muhimbili mpya hasa ikizingatiwa kwamba Muhimbili ya sasa haikidhi mahitaji ya wagonjwa wala kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika utoaji wa huduma bora za matibabu.

“Ni lazima tufanye tathmini ya kina na kujiridhisha kama miundombinu ya hospitali hii ambayo ilijengwa miaka zaidi ya 100 iliyopita kama inakidhi kasi na mahitaji ya ubora wa utoaji huduma za afya za kisasa. Nimefurahi Prof. Museru katika taarifa yake amesema tayari hospitali imeandaa mpango wa matumizi ya ardhi (Master plan) na sisi kama wizara tuangalia namna bora ya kumshauri Rais Mh. Samia Suluhu Hassan na kuona namna ya kutekeleza mpango huu kwa awamu tatu,” amesema Waziri Mh. Ummy.

Awali, Prof. Museru akitoa taarifa ya maendeleo ya MNH, amemweleza Waziri Mh. Ummy kwamba hospitali imeandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi (Master plan) unaogharimu TZS 500 Bil. kwa lengo la kuboresha miundombinu ya kutoa huduma ikiwemo ujenzi wa majengo mapya ya hospitali hiyo.

Prof. Museru amesema ujenzi huo utasaidia kuboresha huduma za utoaji wa huduma za kibingwa na kibobezi kwa ufanisi kwa kuwa hivi sasa yapo majengo machache ambayo hayakidhi mahitaji ya wananchi wanaofika katika hospitali hiyo kupata huduma.

“Mpango wa ujenzi wa hospitali mpya ya Muhimbili utakuwa na faida nyingi, kwanza kutoa huduma yenye viwango na ubora wa juu, wananchi na wagonjwa kutoka nchi za jirani kutumia wodi nzuri za kulaza wagonjwa, kutua helikopta za wagonjwa na kuwezesha Muhimbili kutoa huduma bila kuwapo kwa changamoto za kimfumo,” amesema Prof. Museru.



Pia, Prof. Museru amesema Hospitali inaendelea kutekeleza azma ya Serikali ya kuazisha huduma za kibingwa ili kupunguza rufaa za nje ya nchi.

Mkurugenzi huyo amefafanua kwamba hadi sasa huduma zilizoanzishwa ni upandikizaji figo, upandikizaji vifaa vya kusaidia kusikia, upandikizaji uloto, tiba radiolojia na kwamba hospitali ipo mbioni kuanza kutoa huduma ya kupandikiza mimba.

Katika hatua nyingine, Mh. Ummy ametoa muda wa miezi mitano kwa maduka ya dawa yaliyo karibu na hospitali kuondoka ikiwa ni utekelezaji ya kanuni inayoyataka maduka hayo kuwepo umbali wa zaidi ya mita 500 kutoka sehemu zilipo hospitali zikiwemo Zahanati na vituo vya afya.

“Tulipotoa kanuni hii mwaka 2020 kuna baadhi ya watu walitoa malalamiko kwamba walipata leseni kabla ya kanuni na tulitoa kipindi cha mpito ambacho kinaisha tarehe 30 Juni, mwaka huu hivyo itakapofika tarehe 1 Julai mwaka huu hakuna cha kupeana muda tena,” amesema Mh. Ummy.

Waziri Mh. Ummy ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kuendelea kutoa huduma za kibingwa ambazo kwa kiasi kikubwa zimeisaidia Serikali kupunguza mzigo wa gharama za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi kupatiwa matibabu.

Chanzo: Muhimbili blog
 
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema hospitali ya Muhimbili imejengwa miaka 60 iliyopita na miundombinu yake imeelemewa kabisa.

Hivyo serikali itajenga miundombinu mipya na ya kisasa kabisa itakayokidhi mahitaji ya miaka 50 ijayo itakayojikita kwenye Ubingwa na Ubobezi.

Chanzo: Muhimbili blog
Jenga mikoani nako kuwe kama Dar, ninaamini hakuna sheria inayokataza mikoa ifanane au iizidi Dar, sheria iliyopo inahusu makao makuu ya nchi ambalo ni jambo la kiutawala.
 
Yote mawili yanawezekana mama anaupiga mwingi.

Hayawezekani vinginevyo wangeshafanya hivyo, Dar haihitaji Hospitali mpya, kitiba tayari iko vizuri ikilingsnishwa na Mikoani, I mean kuna watu wanafafiri kutoka Tunduru au Hanan‘g huko mpaka Dar kufwata tu tiba ya kisukari au magonjwa mengine ambapo Hospitali za Mikoa au Wilaya zingeweza kutoa.
 
Unaita wivu? Kwa hiyo unaona ni sawa watu wa Mikoani kuja kutibiwa Muhimbili badala ya kujengewa Hospitali pia huko ?

Kweli Viongozi ni taswira ya watu wanaowaongoza!

Kwahiyo pesa itakayofanya marekebisho muhimbili itatosha kujenga mikoa yote 25 hospital kama ya muhimbili? Hao watu wako wa mikoani wenywe kwenda dar kutibiwa muhimbili wanaona fahari
 
Nooooo, kuna Mikoa zaidi ya 25, Wilaya kibao hazina Hospitali, watu wanasafiri kutoka Mikoani kuja Muhimbili, hiyo fedha igawanywe ipelekwe Mikoani.
Dar tayari kuna hata Mloganzila haiko mbali.

Kajengeni Mikoani pia!
Muhimbili ni hospitali ya rufaa
 
Kwahiyo pesa itakayofanya marekebisho muhimbili itatosha kujenga mikoa yote 25 hospital kama ya muhimbili? Hao watu wako wa mikoani wenywe kwenda dar kutibiwa muhimbili wanaona fahari
Haitatosha lkn itapunguza sana tu, na hata pia kufanya Muhimbili kuweza kuhudumia wakazi wa Dar vizuri zaidi kwa kupunguza foleni kwani sasa hivi Muhimbili inahudumia nchi nzima, kila mtu kutoka Mikoani akiumwa anakuja Muhimbili, kama kila Mkoa ungekuwa kama Muhimbili yake au hata tu kila Mikoa 2 kushare Muhimbili moja tofauti Ingekuwa kubwa sana.
 
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema hospitali ya Muhimbili imejengwa miaka 60 iliyopita na miundombinu yake imeelemewa kabisa.

Hivyo serikali itajenga miundombinu mipya na ya kisasa kabisa itakayokidhi mahitaji ya miaka 50 ijayo itakayojikita kwenye Ubingwa na Ubobezi.

Chanzo: Muhimbili blog
Hapo pesa inataka kupigwa na wanasiasa wa chama cha mafisadi
 
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema hospitali ya Muhimbili imejengwa miaka 60 iliyopita na miundombinu yake imeelemewa kabisa.

Hivyo serikali itajenga miundombinu mipya na ya kisasa kabisa itakayokidhi mahitaji ya miaka 50 ijayo itakayojikita kwenye Ubingwa na Ubobezi.

Chanzo: Muhimbili blog

Labda mimi sielewi maana ya kujenga upya ina maana yale majengo yanabomolewa pale muhimbiri? Kwa tunaokwenda muhimbili mara kwa mara tunaweza kukubaliana kuwa hichi anachisema Waziri hakina msingi kabisa maana kama ni muhimbili basi majengo baadhi yanahitaji ukarabati tuu na unadhifu tuu lakini sio kujengwa upya...huu ni uropokaji tuu wa waziri! Kuna maeneo mengi hayana hospitali zikajengwe na muhimbili iboreshewe vifaa tiba na madawa !
 
Back
Top Bottom