Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Duuh Roma hatarii sana

Najaribu kuwaza, nini lengo la yeye kutumia lugha ya picha kumuhusu Dactari anaetibu watoto jangwani?? Huyo Dr anamuwakikisha nani?

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimejiuliza sana swali hili pia. Kuna mtu amesifia wimbo Ila akaponda video mbovu. Sikutaka kukubaliana nae kwa kuwa natambua video kwa mtu mwenye akili timamu sio tu kuuweka wimbo lwenye muoekano bali kuitumia kufikisha ujumbe Fulani uliojificha

Naamini iko maana na itaeleweka ikiwa pamoja na nuio lake la kuuita wimbo Zimbabwe...naamini haaminishi Zimbabwe kama nchi bali lugha ya picha inayobeba maudhui nzima ya wimbo wake

Anyway, "Vipi report ya upelelezi ikatekwa na mtekaji??"
 
Hivi huyo Roma anajilazimisha muziki maana hata sijui anaimba nini zaidi ya kuongea ongea mistari isiyo na vina wala mpangilio alafu anaimba upuuzi tu... kuna watu hununua miziki yake au? ndio sogeza siku tu kama Soggy Doggy Hunter

Sawa Bashite
 
Hivi huyo Roma anajilazimisha muziki maana hata sijui anaimba nini zaidi ya kuongea ongea mistari isiyo na vina wala mpangilio alafu anaimba upuuzi tu... kuna watu hununua miziki yake au? ndio sogeza siku tu kama Soggy Doggy Hunter
hujui mziki wewe,siku kadhaa utaona unakua wimbo wa taifa huu
 
Huyu Roma ni GENIUS

Kwa misatari hii minne kama hujaelewa bac wewe ni kilaza, maana amejibu kila kitu.

1. Mungu wa Paulo ndio Mungu wa Daudi na ndio Mungu wa John wanayemwita Yohana wa Yahudi.

2. Na ripoti ya upelelezi
Je ni vipi akiteka mtekaji?

3. Walioniteka hawakuja na Noah
Ni uvumi na visanga
Ila kutekanatekana huu ni uhuni wa kishamba.


4.Mi sikuona nyota kwa shoulder
Ila najua wewe ni soldier
Ulikuja mwenyewe ama ulipewa order.
akiteka mtekaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakwenda Zimbabwe, kuna kila sababu yakuamini anaitabiria Tanzania inaelekea kuwa Zimbabwe, kiuchumi (inaanguka) kisiasa (udikteta) kijamii (Maisha duni).

Kuna ule mstari kuhusu ripoti ya kutekwa kuna fumbo kubwa sana pale. Yan mtekaji ndie anapewa kazi ya kuchunguza mtekaji.
Mkuu umebobea vema katika Fasihi
 
Leo nmemsikia mkewe roma alikuwa clouds radio akaulizwa roma yuko wapi akajibu kuwa roma yupo ZIMBABWE hapo mm pia baada ya kuisikia nyimbo yake nmeshindwa elewa kuwa yupo Zimbabwe kweli au yupo Zimbabwe kifasihi kama nyimbo yake ilivyo...

Samsung note7
 
1.Majibu yote roma mkatoliki amayaweka kwenye hii nyimbo na yameeleweka kabisa kuwa watesi wake ni akina nani

2.Ametoa taswira hata ya akina sa8 kilichowatokea

3.Katika mistari yake kuna neno mungu wa "paulo" mungu wa "Daudi" pia mstari uliosema kuwa yupo aliyetabiri kuwa kabla ya jumapili Roma atapatikana na kweli akapatikana hapo ametoa majibu tosha kuwa mhusika mkuu ni nani wala haihitaji kuwa na Degree kuelewa

4.mstari aliogoma kusema kuwa hawakuja na noah na pia aliposema kuwa kwa shoulder haukuwa na nyota lakini alitambua kuwa yeye ni soul...ja haihitaji kuwa na PHD kuelewa waliom...**teka walikuwa ni watu wa aina gani

5.Nilimlaumu sana huyu jamaa kuwa ni mwongo lakini hadi kufikia kutoa nyimbo yenye mafumbo yenye ujumbe mzito namna hii anaashiria alikuwa ana maumivu makali rohoni

6. Nampongeza roma kwa kutoa shukrani kwa watu hasa sisi wanamtandao kwa kupaza sauti popote alipo aachiliwe kitu ambacho kilipelekea kuachiliwa mapeema kabla ya jumapili kama Dab mwenyewe alivyoahidi baada ya kuona presha imekuwa kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora aende zimbabwe ijulikane moja kuwa anaishi na Le Dictator

Kupima mkojo na uchochezi wapi na wapi??
 
Ila huju jamaa haya...

Kupima mkojo na uchochezi wapi na wapi??
 
Back
Top Bottom