Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Mistari bora katika wimbo wa Roma, Zimbabwe.

Mungu wa Paulo, ndiye Mungu wa Daudi.
Na ndiye Mungu wa John mnayemuita Yohana wa Wayahudi


Kipi bora?, nife mseme nilikufa kiharakati?.
Siogopi kufa ila nawaachaje wanaobaki?.

Je kaburi langu mtalipalilia majani?.
Nimeumwa hamjakuja kuniona mnangoja mje msibani?.

Ahsante mliopaza sauti, Nimeiona nguvu ya umma.

Nanasi linaoza msoga tikiti lanaoza shamba.

Kutekana tekana na uhuni wa kishamba.

Aminini siku hazigandi, we ni Yanga mimi ni Simba kuwa mpinzani siyo dhambi.
Ipo siku mtawala atakuwa mpinzani simba akichukua kombe sijui atapona nani?.

Mungu wa Paulo-Paul Mako.

Mungu wa daudi-Daudi Bashite.

Mungu wa John/yohana- John P. Mang'ura.

Walaah! Mwaka huu Zimbabwe patachimbika bila ya kuchimbwa.
 
Video ni nzuri lkn nimeshangaa kuona pkpk ikitengenezwa kwa wheel spanner ya gari.

Sent using Jamii Forums mobile app
0c251691b81114748ed2819c49dd5c66.jpg


Inatumika angalia alikuwa anafungua nini...
 
bonge la ngoma

majibu kwa wale wanaotaka kujua kuhus tukio lake,ila kacheza na fasihi sana hahaha
 
Kwa mara nyingine Roma ameeleweka.

Sijamuelewa anamanisha nani anaposema "hakuona nyota kwenye bega ila anafahamu huyo jamaa ni soja" ni nani HUYO soja jamani. Tuanzie hapa,

Mungu wa Daud, Mungu wa Paulo ndo Mungu wa John wanaemuita Yohana, hapa kaeleweka fika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu anayefanya ukatili nchini humjui? Yuko wapi Ben Saanane!? Mwezi wa 10 huu! Kumbuka juhudi za Mwakyembe kumzuia Roma asiseme lolote kwenye ule mkutano na waandishi wa habari.

Kachapwa mijeledi,kapigwa bila huruma na kafumbwa macho siku3.... ni kina nani hao walio mfanya hivyo? Kwann asiwataje sasa.....na mbona yupo nao.
 
Mungu wa PAUL ndo Mungu wa DAUD,
na ndo Mungu wa JOHN mnaemwita YOHANA wa wayahudi

dongo hili[emoji3][emoji3][HASHTAG]#roma[/HASHTAG]
 
ila kwa hiyo ngoma soon tutasikia Roma katekwa tena....Labda aishie Zimbabwe hukohuko.

ukiusikiliza wimbo izuri hamaanishi zimbabwe nchi ila katumia neno zimbabwe kama tafsida, chekecha kichwa utamwelewa
 
Duuh Roma hatarii sana

Najaribu kuwaza, nini lengo la yeye kutumia lugha ya picha kumuhusu Dactari anaetibu watoto jangwani?? Huyo Dr anamuwakikisha nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi huyo Roma anajilazimisha muziki maana hata sijui anaimba nini zaidi ya kuongea ongea mistari isiyo na vina wala mpangilio alafu anaimba upuuzi tu... kuna watu hununua miziki yake au? ndio sogeza siku tu kama Soggy Doggy Hunter
 
Hakuna ngoma kali ya Roma kama MECHI ZA UGENINI

......" Mimi nakomba hela zote, nasepa kama Lawassa" ni bonge moja la LYRICS, jamaa alitisha sana hapa
Mkuu Roma alitulia zaidi kwenye mathematics zaidi ya hapo bado sijaona kwa kweli
 
Harakati haziwezi isha, binadamu ni kiumbe conscious, sio kama box au sufuria umpeleke kama remote,

Mapambano yanaendelea binadamu huwez shindana nae kwa mabavu. Mifano ipo mingi kwenye historia ukitumia nguvu nin kinatokea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom