reyzzap
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 6,661
- 20,997
Kwa mara ya kwanza Katika ulimwengu wa kampuni KUBWA na MAARUFU za Simu(Tuelewane hapo, usikimbilie ligi uje unitajie Doogee, Energizer au ulefone).
Hatimaye leo mchana samsung ametoa ingizo jipya katika series yake ya 'M', series inayojuulikana kwa kutoa simu zenye battery kubwa.
Hii ni Samsung M51 yenye ukubwa wa 7000mAh,
Ni mwezi haujapita ter 6 mwezi huu alitoa M31s yenye 6000mAh, na hapo nyuma alikua na M30s, M31 zote zikiwa na 6000mAh.
Ili kuokoa mda wanakupa fast charge ambayo itahitaji takribani saa moja na nusu kuijaza charge,
Ukiachana na Battery ambayo ndio inayoitambulisha hii simu zaidi, tukiangalia specs nyingine tunaona....
Camera 4 za nyuma, ikiwemo ya 64MP
Selfie ya 32MP
Processors ya pekee katika M-series maalumu kwa ajili ya gaming
High build quality wakitumia
Glastic(glass+plastic) katika rangi mbili nyeusi na nyeupe.
Display : full HD+ Super Amoled + infinity - O display.
RAM 6/8GB(market dependable)
Storage 128GB,
Kioo cha 6.67 inch
Face unlock na side fingerprint
Na specs nyingine nyingi..
Naomba ieleweke, hii ni MID range smartphone SI flagship, na kwa kujua kuna wapenda ligi humu pia ieleweke sijasifia simu, sijasema ni the best bali nimetaja specs zake, hasa hasa nikilenga battery..
Najua na Unajua kuna simu bora zaidi ya hii nyingi tuu.
Bei ni Tsh laki 9,
Ni Hayo tuu kwa wapenda simu zenye battery kubwa.