Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,589
- 1,679
Katika ziara yake nchini Misri, Rais Samia alipewa ofa na Wamisri waboreshe plan nzima ya mji wetu mkuu Dodoma, iwe na ubora wa plan ya mji mkuuu mpya wa Misri.
Kwa watu waliotembelea Misri hivi karibuni, kama miye, na wale waliofuatilia plan na ujenzi wa Cairo mpya, watakubaliana nami kwamba ofa hiyo ingepokelewa kwa mikono miwili.
Sidhani kama Tanzania itakuwa na uwezo wa kuiga plan nzima, kwani imewagharimu Wamisri dola $ 50,000,000,000. Ila hata asilimia 10 tu ya plan hiyo tukii adopt tutakuwa na mji wa mazingra ya karne ijayo.
Mji huo mpya wa Misri kwa kweli ni futuristic. Umekusanya na kubuni maendeleo yote yaliyofikiwa hivi karibuni na yale yatakayofikiwa miaka ijayo.
Rafiki wa mazingira, usafiri wa mustakbali na zaidi ya yote wamefikiria hata namna gani ya kutumia takataka zote kwa kuzalisha umeme, kutengeneza mbolea, kutumia upya maji yaliyotumiwa,recircling na nusu yake utaendeshwa kwa nguvu za jua!
Sidhani kama wataalamu wetu wa mipango miji, kwa jinsi ninavyoiona Dodoma inavyoendelea, walikuwa na upeo mkubwa kama huu.
Si vibaya kuiga mazuri ya wengine. Nchi zote duniani zimefanya na zinafanya hivyo. It is foolish and pointless to reinvent the wheel!
Ukitaka zaidi google: New Cairo Capital