Odinga ampiga 'tafu'Rais Museveni kusaka kura

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,173
Odinga ampiga 'tafu'Rais Museveni kusaka kura


KAMPALA,Uganda

KATIKA ishara ya kuonesha mshikamano,Waziri Mkuu wa Kenya, Bw. Raila Odinga juzi aliungana na Rais Yoweri Museveni katika mbio za kusaka kura katika Wilaya ya Iganga iliyopo Mashariki mwa nchi hiyo.Habari kutoka nchini
humo zilieleza jana kuwa,Bw. Odinga aliwasili mjini Jinja mapema juzi na kupelekwa katika hoteli ya Nile Resort kabla ya kupelekwa katika hoteli ya Jinja State Lodge ambako alikutana na Rais Museveni na kisha kuambatana naye kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Bunyiiro iliyopo katika eneo la Kigulu Kusini na baadaye viongozi hao wakaelekea katika Wilaya ya Luuka na mjini Iganga.

Alipoombwa kusalimia umati wa watu waliojazana katika mikutano, Bw. Raila alisema: “Nipo mahali hapa kwa ajili ya kumtembelea rafiki na kipinzi changu wangu wa siku nyingi.Hapa ni nyumbani kwa sababu nina mahusinao mazuri watu mahali hapa. Na pia mahali ni sehemu ambako napewa hifadhi salama endapo itahijika,”Alisema kuwa rafiki mara nyingi uwa anahitaji rafiki wa kweli na Uganda ni rafiki wa kweli wa Kenya na akasema kwamba linapotokea tatizo ndiyo mahali pa kukimbilia ili kutafuta njia ya kumaliza tatizo hilo.

Bw.Raila, ambaye ameambatana na wabunge 10 wa bunge la Kenya alisema kuwa Uganda na Kenya zinafurahia mahusiano huku akiukumbusha umati huo kuwa Uganda imepitia katika matatizo mbalimbali kikiwemo kipindi cha utawala wa Bw. Idi Amin ambapo watu walikuwa wakichinjwa kama kuku.

“Katika kipindi hicho, Kenya ilikuwa imesimama na Uganda, licha ya rafiki yangu Museveni kuwa nchini Kenya,”alisema.Alibainisha kwamba tangu uganda ilipojikwamua katika hali hiyo, uchumi wake unakua vizuri huku akisema kuwa Kenya nayo kwa sasa inataka kuf anya kila jitihada liundwe Shirikisho la kisiasa Afrika Mashariki.

“Mna uchaguzi hivi karibuni.Tunataka mchague mtu kwa ajili ya watu mnayemfahamu na tupo nyuma yenu.Tutafanya kazi pamoja,raia wa Uganda wanapaswa kuja Kenya wakiwa na biashara na vijana wa Uganda wanapaswa kuja Kenya na kupata ajira,"alisema Bw.Odinga.

Alitoa wito kwa Waganda kuhakikisha kuwa amani iliyopo inalindwa ili kuwezesha nchi hizo mbili dada kuendelea kufanya biashara kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom