Ocean Road kuitwa Barack Obama road

Ocean Road kuitwa Barack Obama road

Kwann apewe barabara ambayo ipo miaka mingi na imejengwa na watz?, inabidi wampeleke uswazi huko ambako barabara hazifai aboreshe moja wapo kwa kiwango cha lami, then waiite Hilo jina lake kama kumbukumbu kwa mchango wake...
 
Huo ni kukosa uzalendo na kutaka kuiua historia ya nchi. Majina ya barabara yana historia inayoungana na ile ya nchi. huu mchezo wa kugawa majina kila mara inatokana na uzoefu wa kugawa pia raslimali za nchi kiholela.

Ndivyo ilivyo. Kikwete hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi, anapenda sana kugawa, nina shaka kama first lady atasalimika katika huu ugawaji.
 
wangempa soko la kariakoo, ili akiwa pale oval office akumbuke kuulizia usafi wa soko.
 
ni uenda wazimu.kwani viongozi we2 mashujaa kwao wanawaenz? ni utahila 2 cha msingi 2tafute majina ya viongoz we2 wa africa.me ningependa waiite gadafi road.ni hayo 2.
 
huu ni utumwa wa kifikra wa miviongozi ya kiafrika iko siku hata jina la nch litabadilishwa na kuitwa OBAMALAND kisa ni kuatafuta masifa ya kijinga
NAVUMILIA KUWA MTANZANIA
 



sasa we wakuja unaifahamu historia ya dar weye! Hebu nyamaza usionekane kituko .... Acha wenye jiji lao wafanye watakavyo ... Mijitu ya bara sijui vipi...

Dr. Jk kasema itaitwa barack obama road basi ndo itakuwa hivyo... Hutaki acha rudi kwenu bara

Ndio maana anaitwa mwenda wazimu chaka la ujinga wajerumani waliojenga hopitali ya ocean road na barabara wakaipa jina na handaki la kutoka ikulu kwenda pale hospitali bado lipo leo KIkwete anaendekeza ujinga ,bado wametoa pesa nyingi wajerumani kujenga kituo cha kansa kwa nini basi hakupewa KOhler raisi wa ujerumani alipotembelea nchini m.kwere anakumbuka alivyokuwa anatembea kwa miguu toka Msata too Dar ni mshamba zaidi ya wakuja ,asingeweza hata siku moja kugawa hiyo barabara ina kumbukumbu ni barabara ambako IKULU ipo,taasis ya utafiti NIMR huyo kweli zinamtosha au bangi za utotoni ndio zinamchemka sasa , tukichukua nchi tutairudisha jina lake la mwanzo itakuwa OCEAN ROAD huyo zumbukuku muache na ushamba wake
 
Rais wa Marekan anatarajiwa kuwasili iv karibuni hapa TANZANIA. Moja ya mambo atakayoyafanya katika ziara yake hapa nchini, ni pamoja na kufungua barabara ya OCEAN ROAD. Ambapo pamoja na kuifungua itabadilishwa jina na kupewa jina lake. Ni jambo ambalo litafanyika ili kuweka kumbukumbu ya ujio wake huo mkubwa hapa nchini. chanzo: habari ya ITV.

hii serikali MaVi tuu,bado Michelle Obama Road inakuja soon! Aaaaaagh!
 
Acha propaganda za kibaguzi, wote ni watanzania

njiwa umeona watu wa Arusha tu wakuja,kwa taarifa yako ujinga wa kuibadirisha jina barabara yenye historia kubwa kama Ocean Road usingetokea kama ingekuwa iko Arusha...hebu wathubutu kuibadirisha jina 'Makongoro Road' wasikie muziki utakavyokuwa!
 
Viongoz Wetu wakienda ulaya au America wanapewa zawadi ya chai na vitafunwa .....!
 
huu upuuz wa kubadil kila jina la barabara na kuzipa majina ya watu sijui utaisha lini
 
Wengine tulishatabiri kiwango cha ushobokaji ambacho kitaonyeshwa na baadhi wa wabongo kwenye huu ujio wa Obama!

Ni aibu kupita maelezo. Kuna habari kwamba OUT wanataka kumtunuku PhD, sasa haya ya barabara kubadilishwa jina.

Kinachofuata sitaki hata kukiwaza kwa sauti ila kabisa sitashangaa kama (Obama) akiwaambia hao viongozi wavue suruali zao na wao wakavua na kusubiri kunanil@%#!
 
What I can say is "Nothing is the same"-Drake, and I can see ''Things are real falling apart"-Chinua Achebe
 
Wanjamvi,
Hii mada ina maana sana. Kwa bahati mbaya sana wachangiaji wameongozwa na jazba na kuigeuza kama sehemu ya kashfa, kejeli na hata matusi. Tuache hayo tuijadili yenyewe

Kwanza,majina ya vitu, mitaa n.k. ni sehemu ya historia na utambulisho (Land Mark) na hivyo yanapaswa kupewa heshima.

Mtaa wa Aggrey ukitajwa fikra za msikilizaji zinaenda Dar es salaam na kuuhusisha na siasa za nchi hii.

Ngamiani ni landlmark ya Tanga kama ilivyo Mikindani Mtwara, Mukendo Musoma au Isevya Tabora.
Kwa nchi za wenzetu ni nadra kuondoa majina au alama za utambulisho au historia.

Wana utaratibu wa kutoa majina kwa maeneo mapya unaoongozwa na bodi maalumu ya wataalam.
Kuna nchi yenye sheria kiongozi hapewi alama hadi miaka 5 ipite tangu uongozi wake kwsababu maalum

Pili,utaratibu wa nchi yetu serikali za mitaa ndizo zenye wajibu wa kupanga miji yao yakiwemo majina ya mitaa,siyo jukumu la serikali kuu unless utaratibu huo umebadilika mwaka huu.

Kwa mintaarafu hiyo siyo sahihi kumlaumu JK. Watu wa kwanza kulaumiwa ni baraza la madiwani la jiji la Dar es Salaam.Meya wa jiji la Dar es Salaam ndiye 'mtuhumiwa nambari moja''

Meya, mameya, madiwani na wabunge wanapaswa kuja hapa na kutueleza utaratibu wa kubadilisha majina umetumia vigezo gani na nafasi ya historia ya nchi hii itazibwa na kitu gani.

Barabara ya Ocean road imekuwepo enzi na Ocean road ni hospitali ya matibabu ya kansa.
Hospitali inadhaminiwa na serikali ya ujerumani.

Moja ya umuhimu wa Ocean road ni kuwa hospitali ambayo mtaalam maarufu wa tiba (Dr Robert Koch) aliwahi kufanya utafiti wa maradhi ya malaria, black water fever,na homa ya malale.

Kupitia tafiti hizo Dr Koch alitunukiwa medali ya Nobel. Hospitali ya ocean rd ina historia pia kati ya umishenari(Lutheran), ujerumani, Zanzibar na Uingereza.

Yapo mahusiano kituo cha NIMR. Ni kwa maana hiyo German cancer research ina udau mkubwa sana na Ocean road.Kubadili jina la barabara inayokwenda katika eneo hili maarufu ni kuipoteza kabisa historia.

Kama ambavyo barabara ya Bagamoyo ilivyopoteza kiunganisho chake na jiji la mzizima, tunaendelea kuona sehemu ya Ocean rd nazo zinapoteza maana ya historia, utafiti na mengineyo.

Kama walitaka kumtunuku Obama bado walikuwa na nafasi ya kujenga barabara kwasababu walijua ujio huu muda mrefu.Au basi wangeweza hata kuita uwanja mpya 'Obama stadium' n.k

Lakini pia kuna jambo zuri linalotokana na hoja hii. Kuna wanahistoria feki hapa jamvini wanaoeneza uongo kuwa majina ya wazee wao yanafuta katika mitaa kwa chuki za Nyerere dhidi ya jamii fulani.

Barabara ya Bagamoyo imebadilishwa wapo kimya, sasa ocean road wapo kimya.
Miaka miwili au mitatu ijayo watakuja na paper na vitabu kulaani Nyerere kwa kubadili Ocean rd.
kwa hili lazima nafsi zao ziwasute na ni ushahidi tusisikilize tungo zao zilizodhamiria kueneza chuki na fitna.

Naomba tujikite katika mada tuachane na hoja ya aya ya mwisho
 
Kwanini wasibadili jina la Kijiji cha Msoga kuwa Obama Village? Au kama ni sifa sana wangebadili jina la Ikulu kuwa Obama House...
 
Na ile hospitali yetu ya kansa nayo itaitwa obama hospital, ndio maana hatuendelea, yaani viongozi wetu wakikaa ofisini wanawaza mambo ya ajabu ajabu tu. Kweli tunaongozwa na watu wenye maji ya madafu kichwani na sio ubongo
 
Back
Top Bottom