Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,627
WanaJF,
Mwaka 2009 niliomba bastola kihalali kwa ulinzi binafsi kutokana na mazingira ya shughuli zangu za kiuchumi, nilipewa bastola aina ya Beretta yenye risasi 12.
Nilipewa masharti, tahadhari na conditions za kuitunza, kutembea nayo na kuihifadhi ili isilete madhara kwangu binafsi, familia na wadau wengine.
Mimi ni mtumiaji wa beer vizuri tu, nilijikaza nikasema potelea pote.
Kuna mambo ambayo nimegundua baada ya kuimiliki kwa miaka hiyo 10:
1. Inaleta kakiburi na kujiamini kupitiliza kwa mtu yeyote, mazingira yoyote na kwa hali yoyote. Inaongeza kujiamini sana.
2. Mara nyingi nikilewa huko Baa nilikuwa nagombana na washikaji zangu lakini sikuwahi kuitoa wala kufyatua hovyo, hata mke alikuwa anaboa wakati mwingine lakini napiga moyo konde na hakuwahi kuiona na hajui kama nina chombo cha moto.
3. Utembeaji nayo ni mgumu sana maana haitakiwi mtu aione. Nilijitahidi sana sikuwahi kuhisiwa kama ninayo wala kuonesha mtu.
4. Mara kadhaa nikiwa nasafirisha mizigo yangu usiku kwa gari kubwa nimekumbana sana na vibaka wakining'inia kwenye magari, nimeshafyatua kadhaa hewani kujiweka salama.
5. Kwakweli sijawahi kukutana na majambazi nikaitumia. Sijawahi kuvamiwa kamwe
6. Ukiwa nayo mwili unakuwa sensitive sana, bora upoteze pesa kuliko hicho kifaa.
Ushauri:
Kama huna issue kubwa sana, usiombe kumiliki silaha ni mateso sana, kifo ni nje nje.
Sent using Jamii Forums mobile app