MkamaP, mkuu utakubaliana nami kuwa tuko hapa ili tujenge logic, za utendaji na hata hizi za kusifiwa. Sasa naomba ni kuulize, je wewe unafikiri ni mambo yapi hayo Mr. Obama anaasa nchi nyingine ziige mfano kutoka hapa Tanzania? Na kwa vile umeanza kwa kuitaja Kenya, itakuwa vyema kama utaendeleza kwa mfano huo huo ukipenda.
Unaona anaongelea fundamentals za kuijenga nchi endelevu ,nusu ya fundamentals tayari tunazo mkononi tofauti na nchi nyingi kabisa za kiafrika.
Nchi iliyoendelea ambayo haikujengwa ktk misingi hiyo anguko lake ni rahisi sana.
Nimekutolea mfano kenya, kenya kuna seikali mbili unayoijuwa na VIRTUAL serikali yani pale kama unamiliki tusema ardhi ama ng'ombe lazima ulipe ushuru serikali pia lazima ulipe ushuru wa Mungiki(virtual),Yani kila kitu unacholipia ushuru lazima ukilipe mara mbili.
Hatuna Tatizo la ukabila ,Kenya ilifikia nadhani bado ipo kuwa ili upate huduma lazima uongee kikuyu.
Tuna tatizo la Rushwa ndiyo na lahitaji kushughurikiwa lakini huwezi linganisha na majirani zetu mkuu.
Watanzania tunapendana kokote tukikutana ni ndugu wala huwa hatuulizani wewe watoka wapi.
Huduma za jamii mfano shule practically tunasoma bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu.Najuwa hapa utabisha nenda kwa majirani.
Afya huduma yake ni affordable sana japo ipo low quality kutokana na uwezo wetu hii inaashilia kwamba tukiwa na uwezo zaidi tutatoa huduma safi na affordable .Nenda kwa majirani ujionee