Mkuu, OBAMA alizaliwa kisiwa cha AWAII Honolulu-mama yake mzungu mmerikani mweye asili ya ki-Irish na kiyaudi alikutana na baba yake Obama shuleni - yaani wote walikuwa wananafunzi Chuo Kikuu.
Hivi inaingia akilini kwamba Baba yake Obama angekuwa na pesa za kuweza kumsafirisha mama yake Obama na kumleta Kenya ili ajifungue? Jibu na hapana; sasa kwa nini anasakamwa na akina Trump na genge lake kupotosha RAIA wa Merikani na stori za kuchonga tu! Jibu lake linajikita kwenye mambo mawili, la kwanza: Ubaguzi wa rangi! yaani kuna Wazungu wengine wanajiona ni fedhea kutawaliwa na a-coloured President,hawataki kabisa kusikia hilo. La pili ni kwamba matajili wengi wa Merikani ni wanachama wa Republican hawataki kabisa siasa za chama cha Democrat cha kuwainua wanyonge na matajili kutozwa kodi kubwa ili zisaidie wanyonge.
Kwa kifupi siasa za maji taka kuhusu OBAMA zinatokana na sababu nilizo taja hapo juu. Ukweli unabaki pale pale kwamba OBAMA ni raia alisi wa Merikani.