Obama hakuzaliwa marekani??????

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,108
115,837
Kila nikifuatilia hii issue ya wapi alizaliwa Obama huwa

nashangazwa mno na mambo meengi..

1.kwanza inawezekana mtu kuidanganya Marekani nzima na
mashirika yake ya upelelezi?

2.pili kama jibu ni hapana na alizaliwa Marekani kwa nini watu wenye heshima zao
kama Donald Trump hawakubali kuamini?

3.mbona hili suala haliishi?

saa juzi kuna mtu anadai cheti cha Obama ni feki....na kina social security ya mtu mwingine..

yaani hili jambo linanishangaza hadi basi

nyinyi mnaonaje??
 
sidhani kama Obama amezaliwa Kenya, na hata hivyo wamerekani wasingekubali kumpa urais kama kazaliwa nje ya nchi. Hizi ni siasa lazima wachafuane na kuuaminisha umma kuwa hakuzaliwa US.
 
sidhani kama Obama amezaliwa Kenya, na hata hivyo wamerekani wasingekubali kumpa urais kama kazaliwa nje ya nchi. Hizi ni siasa lazima wachafuane na kuuaminisha umma kuwa hakuzaliwa US.

But mbona aliwahi kutoa majibu tofauti kuhusu birth certificate
halafu alipopata shinikizo akaitoa...
huoni labda kuna kitu?
 
Obama alizaliwa Marekani period...Hizi ni propaganda zinaanza tena kupoteza mwelekeo wa Wamarekani baada ya kugundua Republicans wana chance ndogo sana ya kushinda uchaguzi baada ya kugundua waliemchagua ni bomu...Mitt Romney hawezai kushindana na Obama sasa hivi upeo wao umepishana sana. Romney anajicontradict kwa kila jambo. Donald Trump ana chuki binafsi
 
USA kama waliweza kum-tress Osama kwa kutumia programes za chanjo za WHO watashindwa kuthibitisha uraia wa rais yao? common guys hizo ni dirty politics za wabaguzi wa rangi mfano wa Donald trump.
 
Kila nikifuatilia hii issue ya wapi alizaliwa Obama huwa

nashangazwa mno na mambo meengi..

1.kwanza inawezekana mtu kuidanganya Marekani nzima na
mashirika yake ya upelelezi?

2.pili kama jibu ni hapana na alizaliwa Marekani kwa nini watu wenye heshima zao
kama Donald Trump
hawakubali kuamini?

3.mbona hili suala haliishi?

saa juzi kuna mtu anadai cheti cha Obama ni feki....na kina social security ya mtu mwingine..

yaani hili jambo linanishangaza hadi basi

nyinyi mnaonaje??

mkuu huyo jamaa anaheshima gani marekani tofauti na hela alizonazo?
 
Obama alizaliwa Marekani period...Hizi ni propaganda zinaanza tena kupoteza mwelekeo wa Wamarekani baada ya kugundua Republicans wana chance ndogo sana ya kushinda uchaguzi baada ya kugundua waliemchagua ni bomu...Mitt Romney hawezai kushindana na Obama sasa hivi upeo wao umepishana sana. Romney anajicontradict kwa kila jambo. Donald Trump ana chuki binafsi

Sasa mbona bibi yake wa Kenya alisema alikuwepo Obama alivyozaliwa? Alimaanisha nini?

Last edited by a moderator:
................. Ungetaraji kuwa uamuzi huo wa busara wa Obama ungemnyamazisha Trump. Lakini katika kile kinachotafsiriwa kama kutapatapa, licha ya kujimwagia sifa kuwa “amempelekesha” Obama hadi akaamua kuthibitisha uraia wake, tajiri huyo mwingi wa vituko ameibuka na madai mengine mapya kuhusu elimu ya Rais huyo wa Marekani.
Trump anadai kuwa ana mashaka jinsi Obama alivyomudu kujiunga (na hatimaye kuhitimu) vyuo vikuu vyenye hadhi kubwa vya Columbia na Shule ya Sheria ya Harvard (Harvard Law School). Tajiri huyo anadai kuwa “vyanzo” vyake vimemfahamisha kwamba Obama alikuwa “kilaza” (mwanafunzi asiye na uwezo kitaaluma) na haingewezekana kujiunga na vyuo hivyo vinavyofahamika kama Ivy League kutokana na ubora wake wa hali ya juu kitaaluma.
Madai haya mapya ya Trump yamepelekea baadhi ya watu kumtuhumu kuwa ni mbaguzi wa rangi.Hoja yao inaelemea kwenye tafsiri kuwa tajiri huyo anaamini kuwa Wamarekani Weusi (kama Obama) hawana uwezo wa kitaaluma kustahili kujiunga na vyuo vyenye hadhi ya juu.
 
mmmh! dunia ina mambo, hii imekaa kama ile ya Jenerali Ulimwengu alivotishiwa kuhusu uraia wake, walikuwa wanamfumba mdomo asiingilie ishu za watu, binadamu ss kwa ss hatuwezani anayetuweza ni yule aliyetuumba.
 
Kila nikifuatilia hii issue ya wapi alizaliwa Obama huwa

nashangazwa mno na mambo meengi..

1.kwanza inawezekana mtu kuidanganya Marekani nzima na
mashirika yake ya upelelezi?

2.pili kama jibu ni hapana na alizaliwa Marekani kwa nini watu wenye heshima zao
kama Donald Trump hawakubali kuamini?

3.mbona hili suala haliishi?

saa juzi kuna mtu anadai cheti cha Obama ni feki....na kina social security ya mtu mwingine..

yaani hili jambo linanishangaza hadi basi

nyinyi mnaonaje??

Hii kweli ina tija kwetu sisi Wamatumbi na Wakwere?

Maana mimi ninachojua ni kwamba Jamaa keshakuwa Rais wa kwanza mwenye asili ya Mwamerika mweusi. Period!!!!!!!!

"LIWALO NA LIWE"
 
Obama alizaliwa Marekani period...Hizi ni propaganda zinaanza tena kupoteza mwelekeo wa Wamarekani baada ya kugundua Republicans wana chance ndogo sana ya kushinda uchaguzi baada ya kugundua waliemchagua ni bomu...Mitt Romney hawezai kushindana na Obama sasa hivi upeo wao umepishana sana. Romney anajicontradict kwa kila jambo. Donald Trump ana chuki binafsi

Exactly..Obama kazaliwa Marekani na kama ingekuwa amezaliwa Kenya nina hakika wakati ule akiwa Senator tungejua (nafahamu alikozaliwa baba yake) na kwa hulka ya Waluo hilo lingejulikana mapema na hata hiyo hospital ingeitwa Senator Obama kama ambavyo shule iliyoko jirani na Bibi yake Inavyoitwa (Senetor Obama secondary school)
 
Kumbe siasa za maji taka ni dunia nzima. Hapa ni swala la kumtoa kitumbua chake mdomoni na si vinginevyo. Komaa mzee waweza kuibuka tena kidedea.
 
Republicans mwaka huu wamekuwa wachovu mno matokeo yake wanaishia kutapatapa na siasa za kitoto kiasi hiki...

Kwa mtaji huu Obama anashinda kiulaini sana come November 2012.
 
................. Ungetaraji kuwa uamuzi huo wa busara wa Obama ungemnyamazisha Trump. Lakini katika kile kinachotafsiriwa kama kutapatapa, licha ya kujimwagia sifa kuwa "amempelekesha" Obama hadi akaamua kuthibitisha uraia wake, tajiri huyo mwingi wa vituko ameibuka na madai mengine mapya kuhusu elimu ya Rais huyo wa Marekani.
Trump anadai kuwa ana mashaka jinsi Obama alivyomudu kujiunga (na hatimaye kuhitimu) vyuo vikuu vyenye hadhi kubwa vya Columbia na Shule ya Sheria ya Harvard (Harvard Law School). Tajiri huyo anadai kuwa "vyanzo" vyake vimemfahamisha kwamba Obama alikuwa "kilaza" (mwanafunzi asiye na uwezo kitaaluma) na haingewezekana kujiunga na vyuo hivyo vinavyofahamika kama Ivy League kutokana na ubora wake wa hali ya juu kitaaluma.
Madai haya mapya ya Trump yamepelekea baadhi ya watu kumtuhumu kuwa ni mbaguzi wa rangi.Hoja yao inaelemea kwenye tafsiri kuwa tajiri huyo anaamini kuwa Wamarekani Weusi (kama Obama) hawana uwezo wa kitaaluma kustahili kujiunga na vyuo vyenye hadhi ya juu.

umeitoa wapi hii mamii?
 
Back
Top Bottom