TANZIA O.J.Simpson afariki dunia. Alichomoka kesi ya mauaji ya mkewe na rafiki yake wa kiume pamoja na ushahidi kumnyooshea kidole

Sio kweli, OJ hajafa maskini. Hakuwa tajiri lakini pia hakuwa fukara. He was living comfortably.
Kwa mtoto wake. Wakati anaachiwa mwaka 2017 sharti mojawapo si ilikuwa ajulikane atakwenda kuishi wapi na nani ataendesha maisha yake??

Unajua ni kwa nini sharti Hilo liliwekwa!!??
 
Tatizo Kuna kizazi cha kutojisomea kimeibukia hapa kati...

OJ alikuwa kama nembo ya ushindi Wa wamarekani weusi dhidi ya mfumo Wa Sheria Marekani.
Wewe umedanganya kule kwingine kwamba OJ kafa kimaskini.

Muongo wewe.

OJ alikuwa anapata pension nzuri kabisa ambayo ilikuwa iko exempt na debt collection.

 

$25,000.00 kwa mwezi kwa mtu aliyestaafu, siyo kuishi kimaskini.

Jamaa hajui anachokiongelea.
Inawezekana sijaiweka vizuri. Nje ya pensheni yake ambayo alikuwa anapokea, OJ aliweza kupata Hela nje ya hiyo.

Nakumbuka kesi ya yeye na wakwe zake ilifikia mahakama ilisema OJ alipe fidia hiyo kwenye Kila Hela anayoipata nje ya Pensheni yake kwani kisheria huwezi kulipwa Kwa kutumia pensheni ya mtu.
 
Watazamaji milioni 95 tulishuhudia OJ akiwa anakimbizwa na police wakati ule
Atakumbukwa kuwa mchezaji mahiri na pia hiyo Chase ambapo alimuua mke wake na rafiki wa mke wake
Dunia hii ni mapito ila hiyo kesi angefungwa hasara ingekuwa kubwa sana maana Blacks walidhamiria kuchoma kila mahali
Wakaweka gloves ambayo ilikuwa sio yake ili kesi ifutwe tu lakini aliuwa kwa kukusudia
Au sio wakongwe
 
Inawezekana sijaiweka vizuri. Nje ya pensheni yake ambayo alikuwa anapokea, OJ aliweza kupata Hela nje ya hiyo.

Nakumbuka kesi ya yeye na wakwe zake ilifikia mahakama ilisema OJ alipe fidia hiyo kwenye Kila Hela anayoipata nje ya Pensheni yake kwani kisheria huwezi kulipwa Kwa kutumia pensheni ya mtu.
Sasa pensheni ya dola 25,000 kwa mwezi ni maskini huyo? Kwa mwaka ni doła 300,000.

Mtu mwenye kipato cha doła 300,000 kwa mwaka ni maskini?

Au labda we mwenzetu ni tajiri kiasi gani hadi utuambie kuwa kipato cha dola 25,000 kwa mwezi ni kipato cha kimaskini uliotopea?

Doła 25,000 kwa mwezi ni hela nyingi popote pale duniani.

Hicho siyo kipato cha umaskini uliotopea.

Kujifanya ujuaji tu….
 
Kwa wale ambao hamjui, umaarufu wa akina Kim Kardashian ulianzia na timbwili la O.J. Simpson.

Robert Kardashian, baba yake na Kim Kardashian, alikuwa rafiki wa OJ.

Pia, alikuwa ni wakili wa OJ.

Kwa vile kesi ya OJ ilibamba sana, wahusika wakuu wa kesi hiyo wakaishia kuwa ni watu maarufu.

Johnnie Cochran, Marcia Clark, Chris Darden, Robert Kardashian, Alan Dershowitz, F. Lee Bailey, Mark Furhman, Judge Lance Ito, n.k.

Baadaye watoto wa Robert Kardashian ndo wakautumia umaarufu alioupata baba yao kwa kuwa wakili na rafiki wa OJ, na wao kujipatia umaarufu.

Pichani hapo ni Robert Kardashian na OJ Simpson.

IMG_6272.jpeg
 
kifo kinauma, hakifurahiwi na yeyote kiwe cha mtu mzuri au mbaya. hata Yesu alipoletewa taarifa ya kifo cha rafiki yake Lazaro, alilia machozi. Mungu awape faraja wafiwa wote na yeyote aliyeguswa na msiba huo.

Bisides that, kufa ni kitu kizuri kama utakufa mikononi mwa Mungu, ila ukifa nje ya mikono ya Mungu hakika ni hasara kubwa, kwasababu maisha yote umeishi duniani utakuwa umeyapoteza, hayakuwa na faida yeyote, kwasababu mwisho wako utakuwa moto wa jehanum milele na milele.

UFUNUO 14:13 INASEMA: Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

ukifa leo hii, matendo yako ambayo haujayatubia yatakufuata, utaenda nayo, wala usidanganywe na wanaohubiri kwamba watakuombea ukiwa maiti na Mungu atakusamehe, hao waongo. baada ya kifo ni hukumu, tengeneza mambo yako na Mungu kabla haujafa.

KWA JINA LA YESU KRISTO, ninawaasa wote mnaosoma hapa, andaeni maisha yenu ya baadaye, baada ya kifo chenu, kifo kinachokuja ghafla au hat akama sio ghafla, no one knows the exactly date that you would die. WHERE WILL YOU SPEND YOUR ETERNITY? kuna maisha ya baadaye ambayo ni maisha ya milele, eidha milele motoni au milele uzimani, uamuzi ni wako sasa kumpa Yesu Kristo maisha yako sasa ukiwa hai, Mungu ameweka mbele yako uzima na mauti, uchaguzi ni wako. nakushauri chagua uzima kwa kuokoka leo, ama la, utadondokea kwenye mauti ya mielele.

hizi ni siku za mwisho. Biblia ilitabiri kwamba INJILI lazima ihubiriwe ulimwenguni kote hapo ndipo ule mwisho utakuja, wengi huwa wanasema mbona tangu enzi wanasema mwisho na hauji, ndugu, kama mwenye nyumba angeliijua saa mwizi angekuja, angelikesha. kwa sasa, hata wewe msomaji ni shahidi, mtu akitaja neno KUOKOKA hakuna asiyelijua hapa Tanzania, unaelewa kabisa nini maana ya kuokoka, ila unashupaza tu shingo yako. pia, dunia imekuwa kijiji, youtube, facebook, whatsapp, tittwer x etc vinafika kila mahali na humo injili imepenetrate, hivyo kwa kutumia internet injili imefika kila mahala, khata north korea wanakosema wamefungiwa ndani ya nchi, injili ipo, manake wanawaona watu wanaofungwa kwa kushika tu Biblia, na wanajua kushika Biblia ni kosa kwa sheria zao, kumbe wanajua Neno la Mungu lipo, hukumu ya Mungu itakapokuja hapatakuwa na mtu wa kujitetea kwamba hakusikia injili hizi hizi mnazozisikia na kuzidharau na kuzitukana na kutuita tumechanganyikiwa. Mungu akusaidie, amua leo, jiunge na wokovu na watu waliookoka, nawe utapata uzima wa milele. Mungu akusaidieni.
 
Back
Top Bottom