Nyunga za ugali siku hizi zinatoa funza

Nyunga za ugali siku hizi zinatoa funza

Hii issue ya packaging ana utayarishaji kila mtu anafanya anavyojua yeye hakuna anayejali viwango !!
Eeh mwenyenzi Mungu tunaomba utuondolee ukungu kwenye akili zetu!!
Ili la msingi, watu wawe na elimu ya kutosha
 
Lakini uyo funza kwenye unga sio kitu kibaya sana kwa sababu akiwa amepikwa kwa pamoja ugali na ukaiva vzuri hakuna athari yyte zaidi ya ww mlaji kupata virutubisho mwilini usiwatoe hao funza kula hvyo hvyo
Eti eeeh.. Kwangu mm Funza ni indication ya ubovu, ubora hafifu au usalama uliotetereka.. Kama funza anaishi kwwnye unga kuna posibility kubwa ya vimelea vingine viletavyo ugongwa kuwemo pia.
 
Siyo utunzaji tu wengine huchukua gunia la mahindi Moja wanachanganya na gunia la pumba kwa dona iliwapate unga mwingi.

Wafanyabiashara huwa ni wanaharamu kabisa hawajali afya ya mteja.

Kibaya zaidi TFDA hawajaweka udhibiti wakutosha katika usagaji wa nafaka zinazotolewa kwenye hivi viwanda vyetu wakilifanyia kazi hili unga mwingi unaouzwa madukani haufai kuliwa na binadamu.

Nawashauri muwe mnanunua mahindi mnasaga wenyewe au mnunue unga kutoka katika brand zinazoeleweka kwa ubora siyo mradi unga tu
Pumba si ishu sana.. If hazina mabaki ya madawa.. Coz pumba zinakuwa na kiini ambacho ndicho hubeba virutubisho muhimu sana.. Bt if zinamabaki ya madawa ni hatari sna
 
Back
Top Bottom