kuna vitu vinanikeraga sana, eti preserve nyumba ya sanaa for heritage, usiweke mradi wa umeme kihansi, utaua vyura, usipitishe barabara kandokando ya serengeti, utabughudhi wanyama......usipofikiria sana utagundua wazungu wanatuona sisi waafrika kama makumbusho flani hata mahitaji yetu ya kibinadamu yanapimwa katika mtazamo huo.. vunja weka vitu vya maana hao vyura wa kihansi waite wazungu wakaweke huko kwao sisi tunao wakutosha, na hiyo nyumba ya sanaa inafaida gani kwa mtanzania wa kawaida?vitu vyote vinapatikana slipway,makumbusho,bagamoyo hakuna sababu ya kuwa nazo kama uyoga kila sehemu.
Muangalieni na HUYU!!, sidhani kama ni mzima......!!!!!
Mimi nahisi tatizo kubwa tulilonalo ni watu wa kuplani MIJI.
Hiyo wizara ya maendeleo ya makazi ipo hapo kama BOSHENi, maana hakuna sababu ya wahusika kushindwa kufanya mipango ya kuweza kuhamisha mji...
Thamani ya ardi imebaki eneo moja, kwa mfumo wa planning nzuri, mimi nahisi Serikali ingetenga maeneo sehemu hapa hapa Dar es eslaam ( amini usiamini eneo kubwa la DSM bado liko wazi, ingawa ni mkoa mdogo kuliko yote Bara TZ) Kuwa ili ni la SANAA,Hili ni la nyumba za aina flani, hapa hotels, hapa godowns,apartmets za mfumo flani nk nk.
Ardhi bado tunayo kubwa sana, tatizo bado tunataka KUJENGA KILA KITU PALE POSTA.
Serikali ikipima eneo hapa mjini na kuweka criteria flani za ujenzi, basi ardi hiyo kesho yake inapanda thamani hata mara 20, hata kama ni nje ya mji.
Wizara inatakiwa kupima viwanja nje ya City centre na kutoa maelekeze kwa anayetaka kujenga " KUWA KAMA UNATAKA KUJENGA ENEO HILI, UTAJENGA GHOROFA TISA au zaidi na unatakiwa kujenga kwa muda flani, so ingeweza kuweka mfumo wa yule anaeytaka kuwa na kuwanja eneo husika kuwa tayari amejiandaa, hasa maeneo yatakayotengwa kibiashara.
Salamanda ilivunjwa, kesho tutavunja hata ikulu, kwa kuwa tu.... serikali itajenga ingine sehemu... hamna wa kufikiria kuwa keshokutwa tunatakiwa kuwaeleza wajukuu wetu kuwa hapa alikaa rais wa kwanza nk nk.
Marekani wanazo trains za miaka 1800 (late or mid) ambazo zinakarabatiwa na kuwekwa sehemu kwa ajili ya kuingizia pato taifa kwa wanaokuja kuangalia.
LINGINE:
Wachumi wetu ni Vilaza, ingawa ni wazuri sana wa kutoa TAKWIMU, (naomba kama wapo hapa wakubaliane nami) wameshindwa kabisa ku"impose" tax kwenye vyanzo vingine ikiwemo sanaa.Ndo maana leo serikali ya MKWERE, HAIWEZI KUONA UMUHIMU WA SANAA, ILA BANK.
Ukweli sanaa , kama ikiangaliwaqa vizuri, inafukuzana na UTALII katika kuiingizia taifa pato kubwa, maana ina wigo mpana SANAA.
Wao (wachumi wetu) wamekalia kuongeza ushuru ktk, sigara, pombe, magari nk.
tunatakiwa tuwe na maeneo haya kwa kumbukumbu za baadae, ila serikali INATAKIWA SASA KUPANGA JINSI YA KUAMISHA MJI kama ABUJA, Nigeria.
Wa kulaumiwa ni serikali, hasa wateuliwa walioko ardhi kwa kushindwa kuupangilia mji kwa miaka 200 ijao.
Tanzania TUMELAANIKA
Nawasilisha