Nyumba ya Mh. Mariam Kassembe sh. 400mil

Nyumba ya Mh. Mariam Kassembe sh. 400mil

Tuchambue mambo kwa makini. Hivi ni ajabu mbunge kumiliki nyumba ya mil400? Mshahara wake kwa miaka mitano ni mil420 na bado wanachukua mikopo. Kwa hiyo kuwa na vitu hivyo si ajabu. Bodaboda wajue adui yao ni nani, si mbunge wala nyumba wala matrekta ni mfumo. Tupigane kuondoa mfumo si kuharibu mali.

Mkuu ni ajabu sana kwa mbunge kumiliki nyumba ya milioni 400 ikizingatiwa kuwa spika wao alishasema wabunge ni watu masikini sana.

Spika alisema nusu ya wabunge wanataka kuacha ubunge kutokana na hali ngumu ya maisha. Alisema wabunge wa Tanzania ndio wanaongoza kwa kulipwa posho ndogo duniani na hata wabunge wa nchi jirani kama Kenya wanawashangaa.

Thread husika ni:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-ubunge-kutokana-na-hali-ngumu-ya-maisha.html

Sasa kama spika anadai wabunge ni masikini wa kutupwa lazima bodaboda wajiulize imekuwa mbunge wao akamiliki nyumba yenyewe dhamani ya milioni 400? Na siyo bodaboda tuu, mtu yoyote ana haki ya kuhoji uhalali wa kumiliki nyumba yenye dhamani hiyo, wakati ameshaambiwa kuwa wabunge ni maskini wa kutupwa.

For as the old adage goes, "members of parliament are men and women of high rank, [but] they have nothing in the bank!" – Pius Msekwa, Former Speaker of the National Assembly of the Tanzania Parliament.

 
Wao waliitwa kikao na wakasusia kwa kuwa wao ni SSM? Vyama vingine vyote wilihudhuria kikao kile!!! Sasa wao wakatunisha misuli!! Nakuhakikishia angeshiriki vikao vile wala hakuna angegusa mali zake!!! Sasa linapokuja suala sensitive ni lazima mpime!!! Kama mliogopa Atumas wenu atawakoroga sasa wananchi wameamua kuwakoroga!!! Habari zinazozagaa kuna mahusiano makubwa sana kati ya SSM na gas wa Mtwara na nyara za serikali!!! While heading to 2015!!! Mpo hapo!!! Kama ilivyo kwa ile senti tunaambiwa ni road toll kwenye gas stations!!! Unajua matumizi yake!!! Inaingia Green company!! Han ha ha!!
 
Thamani za nyumba zetu sinema tupu!..........milioni 400? Masasi?

VURUGU+MTWARA+NA+MASASI+%25281%2529.jpg

hii yumba mbona ya kawaida tu wanaikuza tu wala sio 400 million
 
Tunataka wabunge wazalendo kama huyu ambaye hatumii nafasi yake ya ubunge kujinufaisha, tutizame mbunge ambaye ni mtu wa watu asiye na tamaa wala uroho wa mali kupitia nafasi yake ya kisiasa:

 
Last edited by a moderator:
thamani za nyumba zetu sinema tupu!..........milioni 400? Masasi?

vurugu+mtwara+na+masasi+%25281%2529.jpg

kwa kweli hii inatia uchungu sana na hii inatokana na baadhi ya wananchi kufikiri eti serikali ni baba au mama yao na kuhisi ni lazima kwao kupata kila kitu ilihali wakisahau wajibu wao kwa serikali.

Picha inaonesha jinsi gani vijana hawa wanavyofurahia mwenzao kuwa maskini kama wao huko wakisahau nyumba na magari ni vitu vya kupita bora kuwa na amani ya roho na wepesi wa nafsi.
 
Pengo la maskini na tajiri lilipo sasa litaleta dhahama kubwa kuliko hiyo,hapa ndo Maccm walipopataka,let them feel the heat!
 
mama kasembe ana elimu ya darasa la saba alikua mwalimu wa U.E kabla ajaacha na kugombea udiwani then ubunge viti maalumu then ubunge wa jimbo

achana naye anakurupuka akijibiwa analeta beti za taarab
 
kapata pa kutokea. magorofa ya masaki milion 300-400 je hiko kinyumba chake atasemaje mil 400? hiyo nyumba haizidi milion 70. aache kudanganya
 
Ndo wachome? Sababu ya bei tu?
soma habari kwa makini. bei ya nyumba imefahamika baada ya kuchomwa....wazalendo walichoma kwa kuwa walikuwa na hasira....hata kama ingekuwa ya makuti bado wangechoma coz ni ya gamba ambalo halijawafanyia chochote zaid ya kujilimbikizia...
 
Tony Blair alishawahi sema, katikati ya maskini tajiri hawezi kuishi kwa amani.
 
Ninachokiona hapo ni chuki ya wananchi juu ya baadhi ya wana siasa. Haiwezekani upigane na polisi halafu ukachome nyumba ya mheshimiwa fulani.
Ina maana wananchi hawako pamoja na wana siasa katika mitazamo ya maisha ya kila siku.
hapana hii ni chuki ya tabaka tawaliwa dhidi ya tabaka tawala.
 
Sasa wananchi wanaonekana dhahiri wmekosa imani na viongozi wao,naishauri serikali sasa kabla ya kufanya jambo lolote wahakikishe wanawashirikisha wananchi na wawaelimishe faida ya rasilimali za nchi kwa faida ya Taifa zima ,haya yanayotokea sasa ni udhaifu wa serikali katika kusimamia rasilimali za Taifa matokeo yake kila wananchi wa eneo fulani sasa wanataka kinachopatikana kwao kiwe chao peke yao ,haya yanayotokea sasa yasiposhughulikiwa mapema siyo muda mrefu yataleta machafuko makubwa zaidi,hizi cheche zilianzia migodini Mara na Tabora sasa zimefika kusini kwenye gesi ,baada ya muda si mrefu moto utalipuka na itakuwa siyo rahisi kuuzima.Hivi viongozi wetu hawaoni wenzetu wa Nigeria na nchi nyingine wanavyoteseka sasa ?chanzo cha yote ni misingi mibovu ya utaifa waliyojiwekea na hili ndiyo linaelekea kutokea Tanzania.
 
alijuaje huyo mwandish nae hana ki2, dharau mbaiya... Ila ni makosa kufikiri kwamba utakuwa salama wakat jamii inayokuzunguka haiko salama.. we watu wako kwenye nyumba za tembe unazungumzia nyumba ya ml 400.. na bado unatetea ges iende dar(hata kama c yeye, walau ndo msimamo wa chama)au awaunge wananch mkono bx? huo ni ubinafsi uliopindukia...hata Mungu hapendi.
 
Sasa wananchi wanaonekana dhahiri wmekosa imani na viongozi wao,naishauri serikali sasa kabla ya kufanya jambo lolote wahakikishe wanawashirikisha wananchi na wawaelimishe faida ya rasilimali za nchi kwa faida ya Taifa zima ,haya yanayotokea sasa ni udhaifu wa serikali katika kusimamia rasilimali za Taifa matokeo yake kila wananchi wa eneo fulani sasa wanataka kinachopatikana kwao kiwe chao peke yao ,haya yanayotokea sasa yasiposhughulikiwa mapema siyo muda mrefu yataleta machafuko makubwa zaidi,hizi cheche zilianzia migodini Mara na Tabora sasa zimefika kusini kwenye gesi ,baada ya muda si mrefu moto utalipuka na itakuwa siyo rahisi kuuzima.Hivi viongozi wetu hawaoni wenzetu wa Nigeria na nchi nyingine wanavyoteseka sasa ?chanzo cha yote ni misingi mibovu ya utaifa waliyojiwekea na hili ndiyo linaelekea kutokea Tanzania.
 
Sio sahihi kupora, kuharibu mali au kuchoma nyumba ya mtu mwingine yeyote bila kujali sababu zinazokusukuma kufanya hivyo. Huu ni utamaduni mpya unaojenga mwelekeo mbaya sana kwa taifa kwani leo limetokea kwa wabunge kesho linaweza kutokea kwa mtu mwingine yeyote kati yetu. Pole sana kwa wabunge na viongozi wengine waliochomewa nyumba na kuharibiwa mali zao nyingine.

Nenda masasi na uitishe mkutano wa hadhara na uzungumze haya
 
Umaskini uliokithiri miongoni mwa wananchi ndio sababu kubwa iliyosababisha chuki kwa wasionacho na kwakuwa siku zote walikuwa wakiwaamini wanasiasa na kuwasikiliza kwa kuamini kuwa watawasadia ktk kuweka mazingira ya kuwapunguzia makali ya maisha hatimaye wamegundua kuwa wanafaidi keki ya taifa wenyewe!ndio maana hasira zimewalenga wanasiasa na hii inaweza kuwa ni mwanzo tu,maana malalamiko yameenea nchi nzima!
 
Serikali inabidi iwe macho kwani tatizo la ajira linasababisha mambo tusiyoyategemea, hao waliochoma nyumba ni wahalifu, wanaanzisha vurugu ili kuhalalisha maovu yao. Naomba serikali ijipange kuwaelimisha watu wa Mtwara lsivyo hata ajira zitakazozaliwa tutazipata watu wa mikoa mingine kama walivyohamishwa WAZARAMU maeneo muhimu Dar
 
Ninachokiona hapo ni chuki ya wananchi juu ya baadhi ya wana siasa. Haiwezekani upigane na polisi halafu ukachome nyumba ya mheshimiwa fulani.
Ina maana wananchi hawako pamoja na wana siasa katika mitazamo ya maisha ya kila siku.

Na haiwezekani uwe pamoja na mtu aliyekua hafikirii mlo wake wa hata mwaka mzima wakati maskini anafikiria cha asubuhi tuu akiamka. Huu utofauti baina wenye nacho na waliokua hawana ndio madhara yake hayo
 
Back
Top Bottom