Nyumba ya Mh. Mariam Kassembe sh. 400mil

Nyumba ya Mh. Mariam Kassembe sh. 400mil

Mh. Lowasa alishasema, tatizo la ajira kwa vijana ni ...........................Mungu saidia watanzania tupate visional leaders.
 
Thamani za nyumba zetu sinema tupu!..........milioni 400? Masasi?

VURUGU+MTWARA+NA+MASASI+%25281%2529.jpg

Million 400/ ahahahaha, hii ni Isidingo
 
Ninachokiona hapo ni chuki ya wananchi juu ya baadhi ya wana siasa. Haiwezekani upigane na polisi halafu ukachome nyumba ya mheshimiwa fulani.
Ina maana wananchi hawako pamoja na wana siasa katika mitazamo ya maisha ya kila siku.

Mkuu umesema vyema sana. Wabunge wa Mtwara hasa huyu Kasembe, Ghasia na Mkuchika ndo wameamua kuitetea CCM kwa damu zao. Na wote tunajua kuwa kuitetea CCM inabidi uwe na akili ya maiti. Sasa hii ni haki yao japo wao hawajachomwa moto. Kwanza kwenye ile nyumba vijana walikuta mafuvu ya binadamu japo vyombo vya habari havisemi.
Mi ni mkazi wa masasi na walichofanya wananchi ni kidogo sana ukilinganisha na madhila wayapatayo kutokana na utawala wa CCM.

Kama CCM ina akili basi inabidi wajifunze kitu kutokana na haya matukio ya kusini.

Japo ugomvi mkubwa ni zao la korosho kuharibiwa na CCM. Hii gesi na vurugu nyingine wametelezea tu.
 
Katika sakata la vurugu za bodaboda dhidi ya polisi (tigo) kule Masasi watu wameshuhudia vurugu zikibadilisha mwelekeo kutoka kwa polisi hadi viongozi wa CCM na serikali yake Wilayani Masasi kulikopelekea nyumba na majengo yanayomilikiwa na baadhi ya wabunge wa CCM na ofisi za chama cha CCM chenyewe kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kutokana na sababu mbalimbali. Miongoni mwa nyumba zilizochomwa moto ni pamoja na za wah. Mariam Kassembe na Ana Abdallah.

"... ndugu mtangazaji, ukiondoa samani za ndani ambazo zote zimeungua, yumba yangu ilikuwa na thamani ya sh. 400mil"
alisikika akisema Mh. Mariam Kasembe wakati akihojiwa na mtangazaji wa kipindi cha patapata cha WAPO redio. Kassembe alivitaja vitu vingine vilivyoharibiwa ni pamoja na matrekta 2, gari na mifugo. " .... kama wewe (mtangazaji) ulivyo huna kitu hata mimi nimebaki sina kitu chochote sasa" aliongeza kusema Mh. Kassembe. Mh. Kasembe anaonekana na yeye hajui kwanini nyumba yake imelengwa pia katika vurugu hizi.

Maswali niliyokuwa najiuliza kuhusu Mh. Kasembe ni kwamba:

1.Wakati yeye akimiliki nyumba hiyo ya 400milioni, matrekta 2 na gari amewafanyia nini vijana (waliochoma nyumba yake) wa Masasi na majirani zake wanaomzunguuza katika kuwaondolea kero zao mabalimbali?

2. Wakati mikoa ya kusini ikilalamikia kutelekezwa na serikali kiuchumi viongozi wao mnamiliki mali kubwa katikati ya watu maskini, hii ni haki? mbona Nyerere hakufanya hivyo kule kwake Mara, Butiama na Msasani?

3. Ina maana kasembe hafahamu kwamba mikoa ya kusini iko nyuma kimaendeleo ikiwa chini ya Serikali inayoongozwa na chama chake tangu tupate uhuru?

4. Ina maana Kassembe hajui kama polisi ni chombo cha dola inayoongozwa na chama chake?

5. Ina maana Kassembe anashindwa kuona uhusiano uliopo kati ya waendesha bodaboda nchini, rushwa ya polisi, umaskini, serikali, wabunge wa chama tawala na chama tawala?

Nadhani tutakujashudia watumishi wetu siku zijazo wakitendewa vitendo vibaya zaidi kama kubakwa n.k na vijana wetu ambao wako irritable kwa kila jambo. Hawaoni nafuu yoyote wala hope ya maisha yao. Hata hizi bodaboda wanazoendesha huwa zinawaletea matatizo makubwa kiafya (fractures, vifua kuuma, kutekwa) huku wakikimbizana kupata kodi za matajiri wao, TRA, matumizi yao na rushwa za polisi barabarani. Iko siku waendesha bodaboda kote nchini watakuja kuungana dhidi ya jambo fulani!!!!!!

viongozi wa ccm ni mfano halisi wa waziri Majivuno wa kusadikika, hii nchi ni masikini sana huku wachache wakijichukulia hata kile kidogo kinachotafutwa kwa jasho na walalahoi na wapiga kura waliowapa mamalka ili wawatumikie!
 
Sio ndugu, lakini wangeweza kumwajibisha kwa kumnyima kura na si kuchoma nyumba

Huu ni 'uharamia' kama uharamia mwingine tu

ukiona mtu anamtetea mwalifu ujue ananufaika na uhalifu unaofanyika na mhusika!!!
 
Mmh, kama unaamini hivyo, good for you
Wachomaji walikuwa na yao tu, hata walolaumiwa kwa makanisa walikuwa akina fulani, lakini ukweli ni kundi dogo tu

Siamini katika masuluhisho ya aina hii

Unadhani hawa akina mama walipolia walikuwa wanalilia nyumba zao? La hasha bima italipa......wao walikuwa wanalilia uhai wao wa kisiasa ambao umetoweka!
 
Mmh, kama unaamini hivyo, good for you
Wachomaji walikuwa na yao tu, hata walolaumiwa kwa makanisa walikuwa akina fulani, lakini ukweli ni kundi dogo tu

Siamini katika masuluhisho ya aina hii

Ni kweli si suluhisho sahihi lakini inaonyesha hasira ya wananchi kwa watawala wao. Hata vita vya dunia havikusababishwa na wanadamu wote. Ilikuwa shughuli ya watu wasiozidi hata 20 lakini watu milioni 52 na mali kadhaa vilipotea!
 
Wanajamvi naomba mnipashe yafuatayo kuhusu Mhe. Kasembe:

1. Je hizo shilingi milioni 400 amezitoa wapi?
2.Je anafanya biashara gani?
3.CV yake.
 
Back
Top Bottom