Nyumba ya Mh. Mariam Kassembe sh. 400mil

Nyumba ya Mh. Mariam Kassembe sh. 400mil

Nyumba ya milioni 400 shilingi za kitanzania,bodaboda kapanga chumba cha 10,000 kwa mwezi halafu hiyo nayo wanapigana chenga na land lord wake kuilipa wakti huo huo ameahidiwa maisha bora kwa kila mtanzania,na Mariam ndie alikuwa akiwaahidi,unategemea wasipoyaona hayo maisha bora ingali wanamuona yeye ananeemeka tutegemee nini hapo?wakifikiria hela za kuwaletea maisha bora waliokuwawakiambiwa huenda kazichukua yeye tutawalaumu?hilo gap hilo la walio nacho na wasio nacho,ni hatari kuliko watu wanavyodhani.
 
Huwa wana inflate bei halisi baada ya majanga kutokea,wakidhani wataweza lipwa sijui nani atawalipa...watulie hiyo ndio nguvu ya umma kazini!
 
Milioni 400 mtwara Masasi! !!???? Labda kama kuna riba za mkopo pamoja na matrekta na magari na nyumba ziwe nyingi sio hio moja. Huku ni kujikweza. Na ninavyojua magamba huwa hawana utamaduni wa BIMA ZA MALI KAMA NYUMBA. Imekula kwake.
 
Tuchambue mambo kwa makini. Hivi ni ajabu mbunge kumiliki nyumba ya mil400? Mshahara wake kwa miaka mitano ni mil420 na bado wanachukua mikopo. Kwa hiyo kuwa na vitu hivyo si ajabu. Bodaboda wajue adui yao ni nani, si mbunge wala nyumba wala matrekta ni mfumo. Tupigane kuondoa mfumo si kuharibu mali.


Tatizo watanzania wamelala sana(katika) mpaka wanashangaa mbunge kumiliki vitu kama hivyo wakati ni vitu vya kawaida sana. Tunao wabunge wengi wenye pesa nyingi kuliko huyo mama na hatujaona nyumba zao zikichomwa moto. Ile kauli ya kwamba kuna eneo ukijenga nyumba nzuri unaonewa wivu inaweza kupata nguvu katika mazingira kama haya.
 
.
Kumbe anajua kabisa watu walio nje ya system hawana kitu eeh? Sasa umefika wakati wale wenye nacho hawana amani ya kukila.
Kuna wakati kwa kila jambo, wakati wa kucheka na wakati wa kulia....
.
Sasa watawala wetu wataanza kuyakumbuka maneno ya hekima ya mwalimu Nyerere alipokuwa anawatahadharisha watawala kuwa linapokuwepo pengo kubwa sana kati ya walionacho n'a wasikuwa nacho, mwisho wake lazima amani itatoweka kwa kuwa hao masikini wanapoishi n'a matajiri wanaofanya kufuru ni lazima mwisho wake watajitwalia mali za hao walio nazo kwa nguvu!!!
 
Wengi wanafurahia ila ingekuwa no wao.....
 
mimi sioni kama haya mambo ya kuchoma moto mali za watu ndio njia ya kutatua matizo yao,watu wanatumia nguvu nyingi sana kutafuta pesa,kwa mfano tractor moja New Holland 75HP;4wd ni milioni 38 tena ni punguzo toka SUMA yakiwa mawili ni zaidi ya milioni 76,mtu kajibana,kajenga nyumba yake kwa mkopo na kanunua vitu kwa pesa ya mawazo,leo anakuja mtu anachoma moto kiurahisi na tunataka kumsifu kwa ujasiri wa kufanya jambo hilo.
hatuwezi kukubaliana nalo hili.watanzania yanayomtokea mwenzako leo,yatakutokea wewe kesho,hili si jambo la kulichekea hata kidogo.
 
Ha ha ha hii ni zaidi ya over price,,, hata kama ni inflation hii ni kali..


Hivi anaijua million 400 ilivyo? Pesa lazima tuipe heshima yake.. Hiyo nyumba hata million 100 tu kufika kwa mbinde..

Nyumba za million 400 ni viota kweli kweli vimejaa mikocheni na mbezi beach sio hiyo nyumba ya vifaa vya kichina kutoka Good one, sunda etc kama inavoonekana hapo juu

Labda kaunganisha na matrekta yake mawili + Furnitures. Hapo itakuwa imefika, japo yeye mwenyewe amevi exclude.
 
Ikiwezekana wachomewe nyumba wote waliotuibia na wanaoendelea kutuibia ili waonje ugumu wa maisha
 
ya slaa bei gan.kuna uhusiano gani kati ya nyumba ya mbunge na bodaboda na rushwa za polisi
 
Pole mama, Machizi hao bhangi zilizidi uwezo wa kichwa kuhimili mikiki mikiki yake!
 
kwa taarifa yako karibu asilimia 80 ya wakazi wa masasi ni hao unaowaita wanasisitiza elimu zote,mdini mkubwa wewe na kwa hili la gesi hio kete yenu ya udini haitofanikiwa
mfa maji haachi kutapatapa na lakuvunda halikosi ubani khabari ndio hiyo meza -bado inautamu -tema bado ina utamu alamsiki
 
sidhani kuchoma mali za watu ndo suluhisho, tunakotaka kuipeleka Tanzania kweli ni kubaya.
 
Naungana na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe na mchungaji Christopher Mtikila kusema kwamba Wananchi wa kusini wana maswali mengi na hakuna hata aliyejaribu kujibu maswali yao.
 
Thamani za nyumba zetu sinema tupu!..........milioni 400? Masasi?

Mh! hata mimi najiuliza...haya! mliochoma nyumba ya watu jiandaeni kulipa fidia, bei ndio hiyo mshapewa!

Ha ha ha hii ni zaidi ya over price,,, hata kama ni inflation hii ni kali..


Hivi anaijua million 400 ilivyo? Pesa lazima tuipe heshima yake.. Hiyo nyumba hata million 100 tu kufika kwa mbinde..

Nyumba za million 400 ni viota kweli kweli vimejaa mikocheni na mbezi beach sio hiyo nyumba ya vifaa vya kichina kutoka Good one, sunda etc kama inavoonekana hapo juu

Nimepapenda sana hapa.....sijui katumia criteria gani kutambua kwamba mtangazaji hanakitu, bilashaka yawezekana wanauhusiano wa karibu sana au katumia kigezo cha kwamba watangazaji wengi hawana kitu! Nchi inavihoja hii!

Thamani ya nyumba ni Milioni 100 ... ndani zimefichwa na kuungua milioni 300 ... ndo maana kasema thamani ya nyumba ni milioni 400
 
Back
Top Bottom