Nyumba ya Mh. Mariam Kassembe sh. 400mil

Nyumba ya Mh. Mariam Kassembe sh. 400mil

mama kasembe ana elimu ya darasa la saba alikua mwalimu wa U.E kabla ajaacha na kugombea udiwani then ubunge viti maalumu then ubunge wa jimbo
wakati wazazi wake wakimsisitiza elimu dunia na akhera ,hao wengine ni akhera tu sasa hivi matunda ya elimu yake yanaonekana japo ya kuunga unga wanachoma moto hahahaahah
 
kwa kipindi cha muda mfupi aliokaa bungeni anwaeza kusema mali hizo amezitoa wapi. haono kuwa tifauti ni kubwa sana wale walichoma nyumba hiyo, si ajabu walikuwa wanashangaa kuwa mali hizo amezitoa wapi.
 
" .... kama wewe (mtangazaji) ulivyo huna kitu hata mimi nimebaki sina kitu chochote sasa" aliongeza kusema Mh. Kassembe... Mwiso wa kunukuu..

Hii wakuu si ni dhereu hii? Eti kama ulivyo wewe mwandishi huna kitu....... Huyu mama ana dharau sana kumbe wangemtia kiberiti mwenyewe!
 
Tofauti ya vipato ktk jamii zetu ni bomu baya sana. Utajengaje nyumba ya thamani ya mamilioni ya shilingi kati ya watu masikini sana? Wati ambao hawajui hatma yao saa moja ijayo?!
 
Thamani za nyumba zetu sinema tupu!..........milioni 400? Masasi?

VURUGU MTWARA NA MASASI %25281%2529.jpg

kama hii ndo 400mil kweli pesa yetu imepoteza thamani.
 
Ninachokiona hapo ni chuki ya wananchi juu ya baadhi ya wana siasa. Haiwezekani upigane na polisi halafu ukachome nyumba ya mheshimiwa fulani.
Ina maana wananchi hawako pamoja na wana siasa katika mitazamo ya maisha ya kila siku.

Hawa wakina mama wabunge, Anna Abdalla na Kassembe washukuru Mungu hawa vijana hawakuwakuta kwani hasira walioionesha kwa kuangamiza nyumba zao ingeweza kuwaangukia wao!!
 
" .... kama wewe (mtangazaji) ulivyo huna kitu hata mimi nimebaki sina kitu chochote sasa" aliongeza kusema Mh. Kassembe... Mwiso wa kunukuu..

kumbe anajua mtu bila kuwa mbunge huna kitu ngoja aionje nae,kama mwandisho ambavo hana kitu boda boda na wanantwara wengi hawana kitu kabisaaa.
 
ni funzo kwa wanasiasa wote tz,is not only mh kasembe!watumikie waliokutuma bungeni na watakuheshimu.pole mama:confused2:
 
Watamconsider kwenye ile 10% ya Gas.awe na subira tu
 
Nina kajumba kamoja ka tumilioni 400 tu huko Masasi, tutrekta tuwili, ka vougue kamoja tu! Shame on you!
 
Huyu Mbunge ajiulize "ni nyumba ngapi katika jimbo lake zenye thamani kama yake"? Je hilo jumba alijenga kabla ya kupata Ubunge? Je amewasaidiaje wananchi wake kujikwamua kutoka hali ngumu za maisha?
 
Ninachokiona hapo ni chuki ya wananchi juu ya baadhi ya wana siasa. Haiwezekani upigane na polisi halafu ukachome nyumba ya mheshimiwa fulani.
Ina maana wananchi hawako pamoja na wana siasa katika mitazamo ya maisha ya kila siku.

hapo c bure kuna k2 kimejfcha,
 
Milioni mia nne unajenga mjengo wa ghorofa hata tatu,hiyo nyumba yake kama imekula m100, basi mafundi walimchakachua
 
Tuchambue mambo kwa makini. Hivi ni ajabu mbunge kumiliki nyumba ya mil400? Mshahara wake kwa miaka mitano ni mil420 na bado wanachukua mikopo. Kwa hiyo kuwa na vitu hivyo si ajabu. Bodaboda wajue adui yao ni nani, si mbunge wala nyumba wala matrekta ni mfumo. Tupigane kuondoa mfumo si kuharibu mali.

Huo mfumo unatetewa na hao wabunge wa chama tawala huko bungeni.
 
Mnakumbuka makala ya ZITTO KABWE kuhusu NCHI YA MABILIONEA 30 NA WALALAHOI 30 MILIONI?Kimantiki ni kweli kwamba kama nchi haitajishughulisha na maskini walio wengi itakuwa ni vigumu kwa Serikali kuwalinda MATAJIRI WACHACHE.Sasa kama ka nyumba kakubabaishia wapiga kura Masasi kana built value ya Millioni 400 UKIONDOA THAMANI YA ARDHI TUPU,je DAR huyu mtu ana nini?eti mwana JF mmoja kasema mkopo?wewe danganyika;WENZIO WAKISHAPATA PESA CHAFU,wanajipatia mitandao benki,Wanapata mikopo kama njia mojawapo ya MONEY LAUNDERING-Tusiwe watu wa kuamini mambo bila kutafiti vizuri jamani ,wakubwa sisi sasa- halafu kila walalahoi wakipiga kelele wanaelekezwa SACCOS,Benki na blah blah blah!Kama MHESHIMIWA MBUNGE KASEMBE kaandika maneno hii kwenye daftari la mali kule Tume ya Maadili na aweke nakala hapa JF!NYUMBA GARI NGAPI,TREKTA NGAPI ,BENKI ANA NINI NA CHANZO NI NISHAHARA NA MIKOPO YAANI MBUNGE ANAWEKEZA ASILIMIA 100 YA MSHAHARA?Hatoi hata zaka?Kweli ukiwa mwongo lazima ufe mapema-ubongo huchoka mno kudanganya kuliko kusema kweli!Haya LUDDITES wa karne ya 21 WAMEFUNJAFUNJA NA KUTEKETESA KWA MOTO STAILI YA 1200 AD
 
Thamani za nyumba zetu sinema tupu!..........milioni 400? Masasi?

VURUGU+MTWARA+NA+MASASI+%25281%2529.jpg



Huyu mama ametudanganya kwakweli!Hata kama mfuko wa simenti huko unauzwa tsh 30 elfu lakini hii nyumba haiwezi kufika mil400 labda kama ina underground apartments.
 
Jamani vijana suluhisho lenu ni 2015 hivi mnahangaika bure na kuchoma majengo si muyaache basi ili mupate cha kutaifisha baadaye au kuuza ili muongeze hazina ya umma.
 
Hilo ni Jambazi linatakiwa likamatwe na kuhojiwa fedha zote hizo alizitoa wapi wakati wananchi ni mafukara?
Katika sakata la vurugu za bodaboda dhidi ya polisi (tigo) kule Masasi watu wameshuhudia vurugu zikibadilisha mwelekeo kutoka kwa polisi hadi viongozi wa CCM na serikali yake Wilayani Masasi kulikopelekea nyumba na majengo yanayomilikiwa na baadhi ya wabunge wa CCM na ofisi za chama cha CCM chenyewe kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kutokana na sababu mbalimbali. Miongoni mwa nyumba zilizochomwa moto ni pamoja na za wah. Mariam Kassembe na Ana Abdallah.

"... ndugu mtangazaji, ukiondoa samani za ndani ambazo zote zimeungua, yumba yangu ilikuwa na thamani ya sh. 400mil"
alisikika akisema Mh. Mariam Kasembe wakati akihojiwa na mtangazaji wa kipindi cha patapata cha WAPO redio. Kassembe alivitaja vitu vingine vilivyoharibiwa ni pamoja na matrekta 2, gari na mifugo. " .... kama wewe (mtangazaji) ulivyo huna kitu hata mimi nimebaki sina kitu chochote sasa" aliongeza kusema Mh. Kassembe. Mh. Kasembe anaonekana na yeye hajui kwanini nyumba yake imelengwa pia katika vurugu hizi.

Maswali niliyokuwa najiuliza kuhusu Mh. Kasembe ni kwamba:

1.Wakati yeye akimiliki nyumba hiyo ya 400milioni, matrekta 2 na gari amewafanyia nini vijana (waliochoma nyumba yake) wa Masasi na majirani zake wanaomzunguuza katika kuwaondolea kero zao mabalimbali?

2. Wakati mikoa ya kusini ikilalamikia kutelekezwa na serikali kiuchumi viongozi wao mnamiliki mali kubwa katikati ya watu maskini, hii ni haki? mbona Nyerere hakufanya hivyo kule kwake Mara, Butiama na Msasani?

3. Ina maana kasembe hafahamu kwamba mikoa ya kusini iko nyuma kimaendeleo ikiwa chini ya Serikali inayoongozwa na chama chake tangu tupate uhuru?

4. Ina maana Kassembe hajui kama polisi ni chombo cha dola inayoongozwa na chama chake?

5. Ina maana Kassembe anashindwa kuona uhusiano uliopo kati ya waendesha bodaboda nchini, rushwa ya polisi, umaskini, serikali, wabunge wa chama tawala na chama tawala?

Nadhani tutakujashudia watumishi wetu siku zijazo wakitendewa vitendo vibaya zaidi kama kubakwa n.k na vijana wetu ambao wako irritable kwa kila jambo. Hawaoni nafuu yoyote wala hope ya maisha yao. Hata hizi bodaboda wanazoendesha huwa zinawaletea matatizo makubwa kiafya (fractures, vifua kuuma, kutekwa) huku wakikimbizana kupata kodi za matajiri wao, TRA, matumizi yao na rushwa za polisi barabarani. Iko siku waendesha bodaboda kote nchini watakuja kuungana dhidi ya jambo fulani!!!!!!
 
400m? Hata nyumba aliyojenga Nyerere Butiama haifiki hata 1 ya 10 ya hii. Ni upuuzi kuwa milionea kati ya watu wanaokufa kwa kukosa elfu 5 ya dawa ya malaria
 
Back
Top Bottom