wabunge wetu ndio wapi hao?
ujinga kipaji,hujui maslahi yako na kizazi chako ndio yanatetewa.Unaleta mipasho tu hapa,bila hao wapinzani ufisadi mwingi wa nchi hii ungefukiwa.Watafanya kazi kwa adabu kama wapo kwenye kamati.
Wabunge wa upinzani huchangia kwa kukosa adabu pale matangazo yanaporushwa papo. Wakati mwingine hutaka bunge lisitishwe kusubiri hitilafu irekebishwe ili mtu wao aongee na kutukana. Ilifanyika hivyo kwenye Bunge la katiba wakati Tundu Lisu akichangia.
Natamfaham muda wa wapinzani kuhutubia papo kwenye Tv ni kipindi cha bunge nje ya hapo ni nadra sana. Wanahaki ya kulia
Bunge kuonyeshwa au kutokuonyeshwa live, kunawapunguzia nini Wabunge jukumu lao la kuishauri na kuisimamia Serikali?
Wakae ndani humo humo waisimamie Serikali kwa hoja zenye mashiko sio fitina fitina na uchochezi tu, baadhi Wabunge wanataka kugeuza Bunge kama ukumbi wa kufanya siasa ili kujipatia umaarufu mwepesi mwepesi huku wakionekana live.
Sasa tuone kama Bunge lisiporushwa live watatueleza walikwenda Bungeni kuonekana live, au walikwenda kuwasilisha hoja za msingi juu ya matatizo ya wananchi na kuisimamia Serikali kuhakikisha inawajibika?
Mara nyingi watu ambao wao kwanza ni chama
na taifa baadae ndo huwa na matatizo ya kiufahamu. Mfano bunge lililopita baadhi ya wabunge walipaza sauti wakisema mikataba ya
gase ni mibovu hivyo isisainiwe; kwa ushabiki wa kichama watu fulani aidha kwa kujua au kufuata mkumbo wa chama, wakasema wapinzani ni waongo na wachochezi.
Haya wakaambiwa tena escrow ni hela za umma chama chetu kikasema hamna siyo za umma na watu washangilia eti wapinzani ni waongo!!
wakaambiwa tena elimu yetu imeharibiwa na big result now! tena wakasema hayo ni mambo ya upinzani tu; waakambiwa tena serikalini kunaufisadi mkubwa unafanyika; wakasema wapinzani ni wakupuuzwa!!
katika yote hayo wabunge wa chama chetu walikuwa "ndiyoooooooooooooo"
Sasa majipu yanatumbuliwa eti nao tena wamegeuka "heeee raisi anafanya kazi nzuri" wakati majipu hayo yamekuwepo mda wote wa miaka tangu uhuru hadi leo lakini mda wote chama chetu na wabunge wake "ndiyoooooooooooo"
Leo wanachama wetu nao eti wanashangilia utumbuaji majipu!! ama kweli ni wafuata upepo misili ya nyumbu,
Ikitokea raisi akasema wote waliotumbuliwa warudi kazini hawana makosa, utawasikia wanachama wetu "ndiyooooooooooooooo"
sasa hapo ndo ujue watanzania hawana ufahamu bali chama chetu kidumu hata kama kitaamua kutuuza ni sawa tu si ndiyo chama chetu jamani utaifa baadaye.
Hahahaaa mlyataka!!Mliyataka wenyewe ... Sitegemei kuona malalamiko kila siku.
Tuendelee na maisha.
Shame on me? No, shame on u brother, kwani hakuna namna nyingine ya sisi kujulishwa kilichokuwa kikiendelea Bungeni iwe na Wabunge wetu au hizo Media, badala ya watu kukaa mwanzo mwisho wanaangalia live, nyinyi hamna kazi za kufanya?
Kuonyeshwa au kutokuonyeshwa live kunawapunguzia nini Wabunge uwezo wao wa kujenga hoja na kuisimamia Serikali.Huna unaloongea zaidi ya kupiga siasa. Hivi kama hata hilo bunge wanaligomea kuonyeshwa live, ndio unategemea bunge hilo lipewe mikataba ya nchi ili waipitie? Awamu iliyopita ilikuwa dhaifu lakini hii ya viwanda haipendi kukosolewa kabisa. Halafu wewe unaonekana ni mbunge wa ccm, mmoja wa mazoba walioko huko bungeni. Niliwahi kusema huko nyuma katika taasisi zisizo na tija kwenye nchi hii basi ni bunge. Bunge lisiloweza hata kuangalia mikataba iliyoingiwa na serekali na bado linajiita ni muhimili mwingine ni kichekesho cha mchana kweupe.
Naunga Mkono Hoja Yako Mtoa Post,
Hili Halihitaji Elimu Kubwa ya kiwango cha P.h.d Kulijua,
Imetokana Na Uimara Na Hoja Nzito Za Wa Wabunge Wa Upinzani,huku wabunge wa chama cha magamba na majipu wakikoroma na kumwagika udenda, Jambo Ambalo Limezidi kukishushia Heshima chama chakavu (CCM )mbele ya wananchi. ndio maana wame amua wasionekane live ili kujaribu kujivika nguo kidogo. katika karne hii ya sayansi na teknoloji jambo hilo ni ujuha mkubwa. linapaswa kulaaniwa na kila mwenye pumzi.
CCM ni waoga sana !Waambieni wabunge wenu wasusie bunge.
mchukulie mbunge kama Lijuakali , huyu jamaa polisi mkoa mzima wa morogoro walimkamia lakini alipambana na kutwaa ubunge .Kweli mkuu,wapinzani walioko bungeni wameingia kwa uwezo wao binafsi.Wengi ni wapambanaji hodari,si kama ccm ambako kuna wabunge mpaka unashangaa kapitaje,hawezi hata kujenga hoja ikaeleweka.
Kuonyeshwa au kutokuonyeshwa live kunawapunguzia nini Wabunge uwezo wao wa kujenga hoja na kuisimamia Serikali.
ccm ni waoga sana !
bila upinzani hii nchi ingetafunwa hadi mifupa .Ile clip ya Wenje kwenye Bunge la Serikali iliyopita kuhusu Mkurugenzi Wilson kabwe nadhani utakuwa umeiona leo.Kwa hayo machache tu inatosha wewe kukubali upinzani ni very strong.
Kwa mchango huu kiukweli sijakuelewa hata kidogo.
Mimi sishabikii vurugu kabisaa bungeni,lakini kwa kitendo hiki kiukweli hakuna sababu ya uchaguzi 2020 kwani ntashindwa kujua mbunge wangu kafanya nini na kajitahidi vipi kadri ya uwezo wake?? Nikuibie tu siri kwamba
""" moshi mzito wa moto usijidanganye kuufunika kwa neti"" kiukweli tulipofika utambuzi wetu hauzuiliki tena kwa kuzima vyombo vya mawasiliano
Katika mengi ambayo serikalu imefanya kiukweli wengi tunaipongeza, lakini kwa hili la kuzima au kuzuia matangazo kwenye chombo muhimu kama hicho kiukweli mimi nalipinga kwa akili yangu ya juu na kwa hili nikipewa sababu zozote nikakubaliana nalo basi nikamwe akili.
ccm tujikubali tunaweza,,,
Lakini kwa kuzuia matangazo nanyosha mikono
Kama mipira hua inarushwa sembuse bunge????
Kama nilivosema
"" KUAMBIWA SABABU YOYOTE KUHUSU HILI NA NIKAKUBALIANA NA HILI, NAOMBENI MNIKAMATE MNIPELEKE NIKAPIMWE AKILI"""
Wahusika lioneni hili