Nyuma ya pazia Bunge live

Magu ni kitendawili.Inashangaza kwamba swala hili amelifumbia macho kabisa.Hivi niamini kwamba haelewi wananchi kujua utendaji wa Bunge na serikali ni haki yao ya msingi.Hivi haelewi kwamba muajiri wa wabunge na Rais ni wananchi?Sasa kama wasipowaona jinsi wanavyowajibika bungeni watawa-asses vipi.Inashangaza sana.
Mimi namshangaa Magu anachoogopa ni nii? Kama anasema tumuombee sisi watanzania huku anatuwekea ukungu kwenye mambo yanayotuhusu si muelewi vile!
 
Bunge LA 2010 to 2015....lilishusha heshima ya Bunge....maadili mabovu ya wabunge Wa upinzani...linatakiwa Bunge lisiwe live...litawapunguza MISIFA wabunge Wa Upinzani.......

maslahi ya wanyonge kutetewa viwavi mnaona ni MISIFA,mnafurahia uozo wa serikali kutokuwekwa wazi.Hii ni fursa kwa wapigaji,wameshangilia kweli kweli
 
yeye mwenyewe ni mpenzi wa clouds 360 kipindi ambacho kipo siku za kazi tu saa 12 mpaka saa 4 asubuhi,kuna haja ya kipindi hiki kutorushwa live ili Rais aangalie recorded usiku.
 
Kwanza nikuweke sawa kuwa kuitika ndioo ni utaratibu mujarabu katika kupitisha baadhi ya maadhimio ndani ya mabunge au vikao mbalimbali. Hivyo ni kitendo cha kujitoa akili kuchukia wakati utaratibu huu ukitumika katika bunge la Tanzania. Nimetaka niliseme hili kwa maana wanachama wa chadema wamekuwa na mzio kuhusu utaratibu huu.
Tatizo la Mzee Sita mpaka ccm hawakutaka aendelee kwa mujibu wao ni kwamba hakuwa anauacha mjadala ujiendeshe kwa wenye uzito wa hoja washinde mjadala. Badala yake alikuwa anavutwa na mjadala na kujikuta anachukuwa upande. Mengine yote alifanya mazuri
Mjadala wa Escrow ulikuzwa na wale wanaccm waliokuwa wanakiu ya kuwania uteuzi wa urais kupitia ccm. Hali hiyo iliwagawa hata kwa hoja ambazo kimsingi hazikuwa na uzito.Hivyo mgawanyo huu ndio uliofanya maazimio hayo ya funika kombe yakafanywa. Umeona baada ya mwnaharamu kupita nini kinachoendelea nafikiri hata Jaji Werema angekuwa hajastaafu angekuwa jaji wa mahakama ya Rufaa.
Hivyo kaa ukaavyo wapinzani hawawezi kuyumbisha serikali kwa hoja ambazo hazina tija kwa wanaccm. Wanatakiwa wawe wanadandia maswala wanayosikia ccm hawaridhiki nayo na kusubiri waungwe mkono. Mfano mzuri umemsikia Msigwa akilalamika kuwa wabunge wa ccm wanataka bunge lirushwe lakini wanasemea chinichini na kuahidi kuwataja kama njia ya kuwashinikiza wawaunge mkono. Mabadiliko yoyote yanayotokea kutokana na usimamizi wa bunge ni juhudi za wabunge wote kwa ujumla wao hasa wa CCM mle ndani wao ni kilakitu.
 
Ngoja apewe chama,nyie wenye akili ndogo mtakimbia chama.....ujumbe wako ni jipu.
 
Kwa sasa mnafurahi kuficha uovu wenu huko bungeni, lakini muda unakuja kila kitu kitawekwa live!!
Hata waliojenga mahekaru Msoga
na arabuni watajulikana, hamuwezi kushindana na Mungu wa Watanzania, maovu yote yatawekwa wazi kabisa kila mtu aone uozo wa viongozi wetu!!
 
Faiza Fox ole wao wanaoshabikia na kucheka kwa sasa maana hao watalia na kusaga meno!!
It's a matter of time my dear sister!!
 
wewe na mboye akili zenu feki, mnakomaliaga ajenda zisizo na tija kwa mwananchi, mwananchi wa kule kiraracha kapata wapi tv, kule tandaimba hata umeme hakuna, badala mbowe alalamike kwa nini wanafunzi wanakaa chini, analalamikia bunge kurushwa live, mpimwe akili
 
Naona unajifanya huelewi sijui kwa manufaa ya nani!Akili za wabunge wa ccm ziko hivi;
''Mh spika jimboni kwangu hakuna maji kabisa,wananchi wangu wanakunywa maji machafu kwenye madimbwi ya maji.Bajeti ya maji haijagusa kabisa jimbo langu na sijui wizara ina mpango gani kwasababu wananchi wangu wanaishi kama wanyama.Mh spika pamoja na changamoto hizo serikali ni sikivu na naunga mkono bajeti kwa asilimia 100'',makofi pwaa pwaaa pwaaa pwaaaaaaaaa,yakichagizwa na vijembe kwa wapinzani.
 

Viwavi wa lumumba tatizo akili mmeshikiwa mpaka mnakuwa wasahaulifu kila mara.Hivi ni mara ngapi wapinzani wamepiga sana kelele juu ya changamoto za elimu ikiwa ni pamoja na madawati,madarasa,vyoo na nyumba mbovu za walimu?Mara ngapi wamesema juu ya wagonjwa kulala chini?Mara ngapi wamesemea matatizo ya wananchi?
Ngoja nikujibu kipuuzi kama maswali yako uliyouliza yalivyo ya kipuuzi,
Huko tandaiba kuna viwanja vya ndege?Mbona serikali inampango wa kununua ndege nne?
Kwanini serikali inagharamia uendeshaji wa TBC wakati kule kiraracha hakuna Tv kama usemavyo?Upimwe wewe akili,period
 
Mbona ndivyo wenye akili hufanya. Kwani Bajeti ni ya Tanzania nzima, zamu hii kwako hakukuguswa pengine kwa kutokuwa na taarifa au kuna nafuu kuliko kwingine. Kwasababu unajenga hoja lazima useme kwa kadiri utakavyo shawishi serikali kukupa pesa za mradi hii haimaanishi kuwa huungi mkono.
Ajabu ni kwa wale wasio na akili wananung'unika mwanzo mwisho kisha hawaungi mkono hoja kwa maana hata hizo pesa zilizotengwa kwa wengine zisiende kisa yeye hakupata alichotaka hizi ni akili au matope?
Hivyo kuunga mkono humaanisha maliza shida za wengine ili bajeti ijayo uhudumie jimbo langu na wengine tuliokosa safari hii. Lakini kauli ya siungi mkono hoja ina maana kuwa bila kuhudumia eneo langu bora tukose wote. Na huu ni mlengo wa fikra za kipumbavu na urofa usio na kifani. Hivyo ndugu yangu badirika usiwe kama hao.
 
Hujitambui wewe.. Na huelewi bunge ni nini?
 
Ngoja apewe chama,nyie wenye akili ndogo mtakimbia chama.....ujumbe wako ni jipu.
Tatizo akili yako imekaririshwa neno jipu kama kasuku. Maana hata pasipostahili hulazimishwa mpaka linakosa muwala wa habari.
Akili ndogo umezipima kwa kifaa kipi? Au ndiyo nyie mmeumbwa kwa ajiri ya kumsaidia shetani kuharibu dunia?
 
Ndio maana nasema hamjui kazi za wabunge,mnasema wasishupalie kuongea bungeni eti mnataka muone vitendo majimboni.Kazi ya mbunge ni kutunga sheria,kuisimamia na kuishauri serikali.Ndio hapo tunapodai haki ya kupata taarifa za bunge kwa uhuru ili tuone wabunge wetu wanatekelezaje wajibu wao ili basi pale shughuli za maendeleo zitakapokwama majimboni tujue tatizo ni nini.
Pili,wabunge wengi hawajui vipaumbele,sio kila bajeti ya serikali ni nzuri,kuna pesa ambazo zinapelekwa kwenye wizara au maeneo ambayo si ya lazima na haraka kwa wakati huo.Hapo ndio ninapokosoa wabunge kuunga mkono kila bajeti kisa tu imeletwa na serikali ya chama chao.
 
Tatizo akili yako imekaririshwa neno jipu kama kasuku. Maana hata pasipostahili hulazimishwa mpaka linakosa muwala wa habari.
Akili ndogo umezipima kwa kifaa kipi? Au ndiyo nyie mmeumbwa kwa ajiri ya kumsaidia shetani kuharibu dunia?
Kuwa mpole usipanic
 
Vipi Hawa Waandishi Wanaoandamana Na Wakuu Wa Wilaya, Mikoa Na Hata Mawaziri Kufanya Political Show Off Hawaongezi Gharama Kwa Serikali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…