Haya Mambo ya Viongozi wa Kisiasa Kwenda na Viti Vyao Kwenye Nyumba za Ibada Yasitishwe

Konny Joseph

Member
Aug 28, 2016
98
174
Screenshot_20240428-222139_YouTube.jpg

Screenshot_20240428-222030_YouTube.jpg

Screenshot_20240428-221812_YouTube.jpg

Screenshot_20240428-221758_YouTube.jpg

Kumekuwa na picha zinazoenea kwenye mitandao zikimuonyesha rais samia akiwa katika ibada kanisani,sina uhakika ikiwa ni ibada ya pasaka au otherwise lakini kinachoonekana ni kwamba amekwenda na kiti chake cha ikulu kwenda kukalia kanisani,sawa na alivyofanya Makamo wake wa Rais.

Hili jambo kwa ujumla linapaswa kukemewa kwa sababu liko kinyume kabisa na maadili ya kiroho.

Inapaswa ieleweke kwamba kuna maeneo huwa binadamu tunapaswa tufanane katika safu moja ili utofauti abaki nao mwenyezimungu peke yake.

Ni wazi kwamba nyumba za ibada ni nyumba za mwenyezimungu,na ni mungu pekee anaepaswa kuenziwa katika nyumba hizo.

Bila kujalisha madaraka uliyonayo,unapofika katika nyumba ya mungu ni vyema kujidunisha na kukubali kuwa sawa na viumbe wengine.

SSH ni muislam na taratibu za kiislam anazifahamu.Anataka kutwambia hata anapokwenda msikitini huenda na kiti cha ikulu kukalia??

Au anataka kusema siku akienda kuhiji Makka atakwenda na kiti cha ikulu kukalia??

Au atakataa kuvaa mavazi ya hija kwa kuwa yeye ni rais??

Nafikiri ufike wakati,binadamu tupunguze kuwakweza binadamu wenzetukwa namna ya kumkufutu mwenyezimungu.

Nafasi ya urais haipo Tanzania tu.Pichani juu ni rais wa Zambia na Rais wa Marekani wakiwa katika nyumba za ibada na wamekalia bench.Huyu wa kwetu anashindwa nini kukalia bench,kwamba utakatifu wake umezidi marais wengine ama vp??

Mungu awabariki sana!!
 
Mi Kuna kanisa jirani hapa la sabato na Kuna lingine la EAGT mbona naona waumini wanaendaga na viti vyao vya cello ....
Kwa hao kwenda kanisani na viti vyao ni sahihi kwa sababu ya uhaba wa viti katika makanisa yao.

Hata sisi waislamu huwa tunakwenda na miswala au mabusati misikitini kukiwa na uhaba wa vifaa vya kukali.

Lakini ni kwwli hapo aliposwali mama kuna uhaba wa bench mpaka kiende kiti cha ikulu??
 
Hili jambo kwa ujumla linapaswa kukemewa kwa sababu liko kinyume kabisa na maadili ya kiroho.
Kwahiyo kiroho unatakiwa kukalia benchi? Hebu acheni hekaya za kijima hizi.

Kiti cha rais au benchi la kanisani haviingiliani kwa vyovyote vile na mchakato wa maombi. Mtu anaweza hata akaja na godoro lake kanisani na wala hakuna shida. Msikariri.
 
Kwa hao kwenda kanisani na viti vyao ni sahihi kwa sababu ya uhaba wa viti katika makanisa yao.

Hata sisi waislamu huwa tunakwenda na miswala au mabusati misikitini kukiwa na uhaba wa vifaa vya kukali.

Lakini ni kwwli hapo aliposwali mama kuna uhaba wa bench mpaka kiende kiti cha ikulu??
Nimekumanya....
 
Sasa unatoa mfano wa marais wa marekani, kwanini hukutoa mfano wa marais wetu? JPM, Nyerere, Kikwete, Mkapa, Mwinyi walivyokuwa wanaenda makanisani walienda na viti vyao?
Upo sahihi,ila nimemua nitoe mfano wa marais ambaokwa sasa wapo madarakani.

Ningewatolea mfano hao,ingezuka hoja kwamba kwa kipindi chao mfumo wa ulinzi ulikuwa haujaboreshwa kwa marais!!
 
Kwahiyo kiroho unatakiwa kukalia benchi? Hebu acheni hekaya za kijima hizi.

Kiti cha rais au benchi la kanisani haviingiliani kwa vyovyote vile na mchakato wa maombi. Mtu anaweza hata akaja na godoro lake kanisani na wala hakuna shida. Msikariri.
Jifunze kuwa sawa na viumbe wenzio,ndio msingi mkuu wa kiimani,ndio maana hata ukiingia msikitini nyote mnakaa chini kwenye mkeka,hakuna cha rais wala mlala hoi!!
 
Kwani shida ipo wapi hapo?.
Tatizo wabongo tunapenda ku- judge na kuhoji vitu visivyo na msingi. Hivi kuna madhara ama tatizo gani Kiongozi akiwekewa kiti Kanisani.
Kwa hiyo USA president angekuwa kawekewa kiti ndio ungeona sahihi kwako?.
Tusiwe watumwa wa kuiga vitu vya nje.
 
Upo sahihi,ila nimemua nitoe mfano wa marais ambaokwa sasa wapo madarakani.

Ningewatolea mfano hao,ingezuka hoja kwamba kwa kipindi chao mfumo wa ulinzi ulikuwa haujaboreshwa kwa marais!!
Inaonekana yeye anavyoona SSH kimamlaka kiti cha SSH kiko juu sana kuliko kiti cha Mungu wa hilo kanisa!
 
Back
Top Bottom