Nyota ya Punda na character zake

Nyota ya Punda na character zake

Mimi nimezaliwa tarehe 08/08 herufi ya mwanzo ya jina langu ni "A"
Nyota yangu ni ipi? Maana wengine huniambia ni Aries (punda) na wengine huniambia ni Leo (simba). Ila nyota zote nimejaribu kuzisoma tabia zake naona kama zinafanana/zinaingiliana ila kwa upande wangu binafsi nimeegemea/kulingana sana na Aries (punda)..
Na kwa mujibu wa tarehe yangu inaonyesha ni nyota ya simba, ila herufi ya kwanza ya jina langu inaonyesha ni punda sasa nashindwa kuelewa nyota yangu halisi ni ipi? Naomba msaada MziziMkavu , MshanaJr na wengineo naomba msaada wenu.
Fuata Tarehe yako ya kuzaliwa ndio sahihi kulliko herufi ya jina lako sio sahihi.
 
Mimi nimezaliwa tarehe 08/08 herufi ya mwanzo ya jina langu ni "A"
Nyota yangu ni ipi? Maana wengine huniambia ni Aries (punda) na wengine huniambia ni Leo (simba). Ila nyota zote nimejaribu kuzisoma tabia zake naona kama zinafanana/zinaingiliana ila kwa upande wangu binafsi nimeegemea/kulingana sana na Aries (punda)..
Na kwa mujibu wa tarehe yangu inaonyesha ni nyota ya simba, ila herufi ya kwanza ya jina langu inaonyesha ni punda sasa nashindwa kuelewa nyota yangu halisi ni ipi? Naomba msaada MziziMkavu , MshanaJr na wengineo naomba msaada wenu.
Mkuu tumezaliwa tarehe na mwezi sawa.

Hongera sana kwa hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NYOTA ANAZOTUMIA BINADAMU ZIMEGAWANYIKA SEHEMU KUU 4 UDONGO,MAJI, UPEPO NA MOTO. INAPOZIDI MOJAWAPO KATIKA MWILI WAKO NDIO TUNAYOITA NYOTA YAKO.TABIA YAKO KATIKA MAISHA YAKO YOTE YA KILA SIKU UNAYOISHI MPAKA MWISHO WA MAISHA YAKO AKA KIFO CHAKO.

NYOTA YA UDONGO, NYOTA YA MAJI, NYOTA YA UPEPO,NA NYOTA YA MOTO
NYOTA YA Upepo inaendana Kitabia na Kimapenzi na NYOTA ya Moto NA NYOTA YA Udongo inaendana Kimapenzi na kitabia na NYOTA YA Maji,

NYOTA ZA TABIA YA Moto-Kondoo,Simba,Mshale

NYAOTA ZA TABIA YA Maji-Ng'e,Samaki,Kaa

NYOTA ZA TABIA YA Upepo-Mapacha,Mizani,Ndoo

NYOTA ZA TABIA YA Udongo-Ng'ombe,Mashuke,Mbuzi

1.Aries-March 21-April 19 (Punda/Kondoo) Siku yake ya Mafanikio ni siku ya Jumanne Asubuhi

2.Taurus-April 20-May 20 (Ng'ombe) Siku yake ya Mafanikio ni ijumaa Mchana

3.Gemin-May 21-June 20 (Mapacha) Siku yake ya Mafanikio ni Jumatano Asubuhi

4.Cancer-June 21-July 22 (Kaa) Siku yake ya Mafanikio ni jumatatu Asubuhi

5.Leo-July 23-August 22 (Simba) Siku yake ya Mafanikio ni Jumapili Asubuhi

6.Virgo-August 23-September 22 (Mashuke) Siku yake ya Mafanikio ni Jumatano mchana

7.Libra-September 23-October 22 (Mizani) Siku yake ya Mafanikio ni ijumaa Asubuhi

8. Scorpion-Oct 23-November 21 (N'ge) Siku yake ya Mafanikio ni Jumanne mchana

9.Sagittarus-November 22-December 21 (Mshale) Siku yake ya Mafanikio ni Alkhamisi asubuhi

10.Capricon-December 22-January 19 (Mbuzi) Siku yake ya Mafanikio ni Jumamosi mchana

11. Aquarius January 20-February 18 (Ndoo) Siku yake ya Mafanikio ni Jumamosi Asubuhi.

12.Pisces-February 19-March 20 (Samaki) Siku yake ya Mafanikio ni Alkhamisi mchana
 
MziziMkavu mkuu hapo kwenye cancer number 9 kama kuna kijikosa.

Aquarius tuko na matatizo gani? Yan najiona mie nina tatizo la kutopenda kuchanganyikana na watu, napenda kukaa mwenyewe tu na kama ni nyumbani basi nitulie na family mates sio mambo za majirani nk ( kama kuna zile shughuli za kkijamii za ulazima hapo naweza changamana nao otherwise naonaga tabu sana.
 
Aquarius nyota yake ni nyota ya Upepo siku yake ni jumamosi Asubuhi Tabia ya nyota ya upepo ni tabia ya kiume hata kama ni Mwanamke una tabia ya kiume marafiki zako ni wanaume ndio wazuri kwako kama ni wewe ni Mwanamke. Una Spirit Pepo mwilini mwako ndio anaye kufanya upende kuwa peke yako na maaduwi zako wengi ni Wanawake wenziwako. Unapenda kusafiri safiri na kukaa mbali na wenzako wa kike hata ukiwa nyumbani katika familia unapenda uwe peke yako ndio tabia yako. Tafuta mtu apate kukutibia Mume atakaye kufaa ni Mwanamume mwenye nyota ya Simba ndie atakaye kufaa na kukuelewa tabia zako.
 
Aquarius nyota yake ni nyota ya Upepo siku yake ni jumamosi Asubuhi Tabia ya nyota ya upepo ni tabia ya kiume hata kama ni mwanamke una tabia ya kiume marafiki zako ni wanaume ndio wazuri kwako kam ni wewe ni mwanamke. Una Spirit pepo mwilini mwako ndio anaye kufanya upendekuwa pek yako na maaduwi zako wengi ni wanawake wenzi wako.Unapenda kusafiri safiri na kukaa mbali na wenzako wa kike hataukiwa nyumba ni katika familia unapendauwe peke yako ndio tabia yako. Tafuta mtu apate kukutibia Mume atakaye kufaa ni Mwanamume mwenye nyota ya simba ndie atakaye kufaa na kukuelewa tabia zako.
Nitibiwe nini?
Sina marafiki wa kiume
Sina tabia za kiume ( labda kupendelea mpira) maybe
Muda mwingi niko around na KE, after interaction kidogo ndiyo napenda tu kuwa alone. Simply ni kwamba I enjoy my own company.
Sijawahi kuwa na adui, yan wale ninaojua kabisa huyu tulikwazanaga na sasa tuko na kichuki flani hivi baina yetu. Labda wale wachukiao watu for no reason lakini mie nakuwa sijui kama rohoni kwako una chuki.
 
Mtu wa kukupa company mzuri uwe na rafiki wa kiume ndio atakaye kupa company vizuri sio lazima awe mpenzi wako japo awe rafiki yako wa kawaida, ukiwa una matatizo anakupa ushauri mzuri ndio utakuwa upo vizuri zaidi .kuliko kuwa na amrafikiw akike watakuw wngi wao ni maaduwi zako hawakutakii mema jihadhari nao. Na kuhusu kushughulikiwa dawa au maombi una pepo katika nyota yako ndio anaye kufanya wakati mwengine marafiki zake wakuchukie na kukuonea wivu au hata kukupiga vita .Kama hivi sasa hayaja kutokea baadae ninayo kwamabia utakuja kuyaona mbele ya maisha yako. Tafuta Sheikh au Mchungaji mzuri akufanyie maombi makubwa na umpe sadaka ya pesa ndio mambo yako yatakuwa mazuri.
 
Mtu wa kukupa company mzuri uwe na rafiki wakiume ndio atakaye kupa company vizuri sio lazima awe mpenzi wako japo awe rafiki yako ukiwa una amtatizo anakupa ushauri mzuri ndio utakuwa upo vizuri zaidi .kuliko kuwa na amrafikiw akike watakuw wngi wao ni maaduwi zako hawakutakii mema jihadhari nao. Na kuhsu kushughulikiwa dawa au maombi una pepo katika nyota yako ndio anaye kufanya wakati mwengine marafiki zake wakuchukie na kukuonea wivu au hata kukupiga vita .Kama hivi sasa baadae ninayo kwmabia utakuja kuyaona mbele ya maisha yako. Tafuta sheikh au mchungaji mzuri akufanyie maombi makubwa na umpe sadaka ya pesa ndio mambo yako yatakuwa mazuri.
Mkuu utagunduaje km nyota imeibiwa
 
Aquarius nyota yake ni nyota ya Upepo siku yake ni jumamosi Asubuhi Tabia ya nyota ya upepo ni tabia ya kiume hata kama ni Mwanamke una tabia ya kiume marafiki zako ni wanaume ndio wazuri kwako kama ni wewe ni Mwanamke. Una Spirit Pepo mwilini mwako ndio anaye kufanya upende kuwa peke yako na maaduwi zako wengi ni Wanawake wenziwako. Unapenda kusafiri safiri na kukaa mbali na wenzako wa kike hata ukiwa nyumbani katika familia unapenda uwe peke yako ndio tabia yako. Tafuta mtu apate kukutibia Mume atakaye kufaa ni Mwanamume mwenye nyota ya Simba ndie atakaye kufaa na kukuelewa tabia zako.
Hii nyota ya simba mimi ninayo hii huyu atakua wangu tuuuu
 
Mkuu utagunduaje km nyota imeibiwa

DALILI ZA MTU ALICHEZEWA AU KUCHUKULIWA NYOTA

Mara nyingi kinachomuendesha mtu kwenye maisha yake ni nyota. Nyota inapokuwa sawa ndio inayokupa ujira ulio mzuri kulingana na shughuli unayoifanya.

Kuna watu hufanya kazi ambazo ni tofauti na Nyota zao. Hapa utaona mambo hayaend sawa Kwan Nyota yako haing'ri kulingana na muwako wa Nyota yako.

Kila Nyota ina tabia yake na tabia ya Nyota ndio inayotafsiri aina ya kazi unayotakiwa kuifanya. Na ukifuatisha nyota yako inavyo kueleza ni kazi gani utakayo weza kuifanya unapata mafanikio makubwa. Haimaanishi kuwa lazima ufanye kazi inayiendana na Nyota yako ila ukifanya unapata mafanikio haraka.

Kuna matatizo ya nuksi yanayosababisha na kufungwa kwenye Nyota yako hapa wanaweza wakakufunga kupitia kivuli chako au athari zako ( vitu vinavyokuhusu wewe nguo, nywele zako, nyayo zako kinyesi na kadhalika)
Na wengine huweza kuiiba Nyota na kuzifanyia shughuli zao. Mfano mnaweza mkawa mnaishi pamoja na mwenzio akatumia Nyota yako kwenye shughuli zake. Pia hata baadh ya dawa za mapenzi zinaweza kuleta nuksi kwa mfanyiwa.
Mfano zile dawa zenyewe mfano anatakiwa mfanyaji atamke kwamba fulani awe chini yangu mimi niwe juu yake Automatic kama dawa zikifanya kazi huweza kushushwa kinyota.

Dalili za mtu mwenye matatizo kinyota
Mambo yake kutokwenda sawa
Kuchukiwa na kudharauriwa na watu hata wadogo
Kuhisi mnyonge usie na faida yoyote
Mateso kwenye mahusiano
Kuvunjika ndoa au mahusiano bila sababu za msingi
Watu kukusema vibaya
Hupati pesa na ukipata haikai
Shida haziishi na misukosuko kukuandama
Hizo ni baadhi tu ya dalili za mtu aliyechukuliwa Nyota, wakati mwingine huwa ni watu wa karibu mke bosi ndugu huweza kutumia Nyota yako kwenye mambo Yao ya vipato.
Unapofikia dalili hzo tafuta tiba haraka ili ujinasue na mateso pamoja na kudhalilika. Unawwza ukafanyiwa visomo vya ufungusi na dawa na mambo yako yakaenda sawa
 
Mtu wa kukupa company mzuri uwe na rafiki wa kiume ndio atakaye kupa company vizuri sio lazima awe mpenzi wako japo awe rafiki yako wa kawaida, ukiwa una matatizo anakupa ushauri mzuri ndio utakuwa upo vizuri zaidi .kuliko kuwa na amrafikiw akike watakuw wngi wao ni maaduwi zako hawakutakii mema jihadhari nao. Na kuhusu kushughulikiwa dawa au maombi una pepo katika nyota yako ndio anaye kufanya wakati mwengine marafiki zake wakuchukie na kukuonea wivu au hata kukupiga vita .Kama hivi sasa hayaja kutokea baadae ninayo kwamabia utakuja kuyaona mbele ya maisha yako. Tafuta Sheikh au Mchungaji mzuri akufanyie maombi makubwa na umpe sadaka ya pesa ndio mambo yako yatakuwa mazuri.
Unayoyasemea me hayajikuta bado kiukweli. Maybe in the future huko uzeeni...

In short marafiki wa kike wananipenda, nilikopita shuleni, majirani nk ninawaona na baadhi wananiambia ila mimi tu ndiyo nina lifestyle ya kutopenda kujichanganya sana. Sometimes nikiamua I make friends easily afu ukishaanza kuniganda me naona usumbufu naanza kukukwepa. Tatizo langu ni ilo
 
Kazi kwako Bibie sikulazimishi ukubali kila ninacho kwambia. Lakini kama ni bado mdogo utakuja kuyaona mbeleni. Watu wenye nyota kama yako ni watu waTabia ya Negative huwa hawapendi kuambiwa kitu moja kwa moja aka (Positive) hata kama una muambia kitu cha ukweli kubisha kwake ni lazima mpaka yamkute ndio ana amini ni watu wenye nyota kama yako ni watu wenye Tabia ya NEGATIVE SIO POSITIVE.
 
Yan hapo ni umeenda OP kabisa, ukubali ukatae.

I'm in my middle 30's nishaona vingi chini ya jua...
 
Mkuu unaweza nifafanulia nyota ya mizanu

LIBRA HOROSCOPE 2020.jpg

NYOTA YA MIZANI (LIBRA)
  • Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 September na 22 Oktoba ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni VENUS (ZUHURA).
  • Siku yao ya Bahati ni Ijumaa.
  • Namba ya Bahati ni 6.
  • Rangi ya Bahati ni Kijani isiyoiva.
  • Asili ya nyota hii ni Hewa.
KIPAJI CHA MIZANI
(Extra Sensory Perception)
Wenye nyota hii wana kipaji cha kufumbua mafumbo na kujua siri za watu bila kuambiwa.

TABIA ZA MIZANI:
Wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kupenda usuluhishi, amani na upatanishi. Ni watu wasikivu, watiifu, na wepesi kuongozwa. Ni wenye maumbo ya kupendeza hasa wanawake. Kwa ujumla ni watu wenye roho nzuri na wanajua kupenda na wenye mahaba mengi.
Ni watu wastraabu, wenye adabu heshima na ni wakarimu kwa mtu yeyote na wanajipenda sana. Katika maisha yao wajipenda sana.

TABIA YA MIZANI KATIKA MAPENZI
Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye nyota hii ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye nyota hii wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.
Watu wa mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.
Kwa sababu hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina matatizo na zisizo na raha kwa sababu ya kuoa mapema bila kuangalia. Wenye nyota hii wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.
Katika suala la mahaba (Romance) na ngono (Sex) wao ni mabingwa. Wanajua sana kumpendeza mwanamke kwa maneno matamu yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.
Kwa ujumla wenye nyota ya Mizani wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao waishi katika hali nzuri.

TABIA YA MIZANI KATIKA FEDHA
Watu wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kutokuwa na maamuzi katika masuala ya fedha. Lakini hiyo siyo sababu ya wewe kufikiri kwamba wao ni wajinga.
Wanapofanya hivyo huwa wanapima au kufikiria kuona uwezekano wa fedha kutumika vizuri.
Ni watu wenye mipango mizuri na mara nyingi kwa kutumia uzoefu na kipaji chao kidiplomasia na upole, huwa wanapata mafanikio katika biashara zao.
Wana kipaji cha kuelewa watu wengine wanahitaji nini na wanatumia maneno matamu kuwashawishi wawape wanachokitaka na wanafanikiwa.
Wanapenda sana vitu vizuri na vyenye thamani na wako tayari kutumia fedha yeyote kutekeleza malengo yao.
Kwa ujumla ni watumiaji wazuri na wenye ubinafsi mkubwa.
{mospagebreak}

MAVAZI YA MIZANI
Wenye nyota ya Mizani wanatakiwa wavae nguo yenye kupendeza zenye mapambo na zenye kuashira mahaba.
Nguo ziwe za rangi ya Pinki au rangi ya udongo.
Kitambaa kiwe cha kotoni chepesi na chenye picha picha, kisiwe kile ambacho hakikuchorwa kitu.
Wavae sana mikanda na wapende kuvaa nakshi za maua pamoja na skafu au mitandio iliyoingia. Wanapendelea mavazi ya ushanga na mikufu.

MATATIZO YA KIAFYA
Nyota hii inatawala figo, sehemu ya utumbo mkubwa, kiuno, mpaka sehemu ya juu ya matako.
Sababu kubwa ya maradhi yao ni kwamba wanapenda sana kutafuta amani na suluhu hata wakiudhiwa au kukasirishwa. Matokeo yake wanavunjika moyo na kujinyima yale wanayoyapenda. Sana na hiyo inawafanya waudhike na wajisikie vibaya na inawasababishia maradhi.
Magonjwa yao makubwa ni figo, kibofu cha mkojo, ugonjwa usioambukiza wa ngozi unaowasha na unapojikuna huvimba (Eczema),maradhi ya misuli ya kiuno na matoki.
Tatizo lingine kubwa ni unene.Watu wa mizani wanapenda sana kula na hiyo inatokea sana wanapokuwa wameudhiwa. Wao wanaona ni bora zaidi kuondoa hasira zao kwa kula chakula.

KAZI ZA WENYE NYOTA YA MIZANI
Wenye nyota hii wanapenda sana kutumia uwezo wao wa kuzaliwa na inawawia vigumu wakati mwingine kutafuta kazi wanazozipenda.
Wanapenda kufanya kazi katika mazingira ya amani na yasiyo na usumbufu.
Kazi zao hasa zinakuwa za uhusiano wa jamii ushauri wa ndoa, biashara ya sanaa, ushauri wa mambo ya urembo au mwanasheria.

FAMILIA ZA MIZANI
Wazazi wenye nyota ya mizani wanapenda sana unadhifu na wanapenda watoto wao wawe nadhifu na wenye mavazi mazuri.
Wanapenda kutumia muda mwingi na fedha nyingi kuwafunza watoto wao tabia nzuri. Kwao ni muhimu sana mtoto akikubalika na kila mtu.
Wanapenda amani katika nyumba zao na wana tabia ya kuwapangia watoto wao namna ya kuishi na kufanya vitu ambavyo wao wnyewe wameshindwa kuvifanya.

MADINI YA MIZANI
Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa LAPIS LAZULI. Mawe kama nye rangi ya Bluu iliyokoza, wamisri wanayaita mawe ya peponi. Yakiwekwa kama kito kwenye pete ya dhahabu yanaleta mizani kwa wenye nyota hii.

UHUSIANO WA KIMAPENZI
(Punda na Mizani)
Tabia ya Punda ya haraka haraka. Vishindo na kutumia nguvu bila kufikiria, hulainishwa au kuzimwa na diplomasia, uerevu na ujanja wa mizani. Punda vile vile hupendezwa na uwezo au kipaji cha mahaba walichonacho wenye nyota ya mizani.

VYAKULA VYA MIZANI:
Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula au Matunda yafuatayo ambayo ndio yanayotawaliwa na nyota yao,Tufaha (Apple), viazi Mviringo (Potatoes), Chaza (Oyster) na Nyama ya Njiwa.

NCHI ZA KUISHI ZA MIZANI:
Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii ya Mizani.
Miji hiyo ni Copenhagen (Denmark) na Vienna (Austria) na nchi ni Canada na Japan.

RANGI ZA MIZANI
Wenye nyota hii wanapenda rangi zilizopakwa juu juu na laini hivyo wanashauriwa watumie rangi ya aina yeyote lakini iwe hafifu katika nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara.
 
Back
Top Bottom