Jimena
JF-Expert Member
- Jun 10, 2015
- 25,935
- 96,117
[emoji2]sista hujanitembelea kitambo kweli?
Upo?
[emoji2]sista hujanitembelea kitambo kweli?
furaha yangu umerudiPilika zilikuwa nyingi Ila nipo
Nimerudi aiseefuraha yangu umerudi
kuna mengi ila uniambie kwanza ulikuwa wapi haiweekani unitoroke kimya kimya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! nani kamficha ndege wanguNimerudi aisee
Nipe mpya zilizojiri wakati sipo ...
Hahahahaha nilikuwa masomonikuna mengi ila uniambie kwanza ulikuwa wapi haiweekani unitoroke kimya kimya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! nani kamficha ndege wangu
Mkuu MziziMkavu naomba pia utuchambulie kuhusu nyota ya Mapacha (Gemini)
Tabia zao, rangi zao, kazi, safari na kila kitu
Japo huu Uzi niwamuda kidogo mzizi mkavu unaweza kunisaidia nyota yamshale??
Vipi na wenye nyota ya simba?
Aise simba kumbe tuna viburi eeh. Ila mi sikuhizi sina kiburi mbona[emoji87]View attachment 511497
NYOTA YA SIMBA (LEO)
Hii ni nyota ya tano katika mlolongo wa nyota kumi na mbili.
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21Julai na 21 Agosti.
Sayari yao ni Jua (Sun).
Siku yao ya bahati ni Jumapili.
Namba yao ya bahati ni 1 na 4.
Rangi yao ya bahati ni Njano au rangi ya Dhahabu.
Asili ya nyota yao ni moto.
KIPAJI CHA SIMBA (INSPIRED):
Wenye nyota hii wana kipaji cha ufunuo wa kiungu , wana uwezo wa kuvumbua mambo ambayo yanaweza kuwaletea fedha pamoja na kwamba hazikai.
Wanauwezo vilevile wa kuponya kwa kutumia mikono yao kuponya watu na wanakipaji cha asili cha uongozi.
TABIA ZA SIMBA:
Watu wenye nyota hii ya Simba ni watu wanaopenda ufahari mkubwa na kutukuzwa. Ni watu wanaopenda kutumia na wanataka waonekane na wanuwezo wa kuvumbua mambo amabyo watu wengine hawajui na wanapenda sana heshima.
ni wakarimu lakini ni wajeuri na wanapenda kuonea watu. Wana hisia kali, ni wakali na wanakiburi.
TABIA YA SIMBA KATIKA MAPENZI:
Tabia ya Simba ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, huwaharibu wale wanao wapenda.
Furaha haina mpaka katika mapenzi ya simba, mioyo yao mikubwa na hisia zao nzito hutokeza dhahiri wanapompenda mtu.
Baada ya hapo ndipo sura kamili ya Simba hujitokeza. Wao wanathamini sana mapenzi na juu ya jambo lolote, na wanaweza kuwa waaminifu sana na wakati mwingine huwaabudu wapenzi wao.
Wanapenda kujishughulisha sana na mambao ya mapenzi lakini mambo yakiharibika basi inakua vigumu sana kuyatengeneza.
Tatizo lao kubwa ni wao kujisahau kwamba ni upande mmoja wa penzi na wanajifanya wao ndio viongozi.
Kwa nje wanaonekana ni wenye kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani wanaweza kuwa wanaumia lakini hawawezi kukubali. Hata hivyo mara nyingi hutegemea kupata hisia kama walizonazo wao kutoka kwa wapenzi wao.
MATATIZO YA KIAFYA:
Nyota hii inatawala moyo, sehemu ya juu ya mgongo na bandama.
Vilevile inatawala uti wa mgongo na mshipa mkubwa wa damu.
Matatizo yao makubwa kiafya yanahusiana na maradhi ya kuumwa sehemu ya juu ya mgongo.
Maradhi yanayotokana na damu kama shinikizo la damu la juu na chini na maradhi ya moyo.
Vilevile wanaugua maradhi ya homa ya uti wa mgongo.
KAZI ZA WENYE NYOTA YA SIMBA:
Wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi zifuatazo; kazi za usimamizi, kama katika kampuni yake binafsi au katika mashirika au biashara, kazi za michezo au uongozi wa michezo.
Wanatakiwa wafanye kazi za usonara au kazi za kuuza au kutengeneza mavazi ya mitindo.
Vilevile wanatakiwa wafanye kazi za uigizaji au uendeshaji sinema au kazi zozote zinazohusika na masuala ya vijana.
Kazi yao nyingine ni ya ualimu katika taasisi, shule au vyuo vya ualimu.
FAMILIA ZA SIMBA:
Kwa asili Simba ni Mfalme na mamlaka yake yamezungukwa na hisia za kifalme. Wazazi wa simba huwa wana mila ya kuwapangia watoto wao namna watakavyoishi kwa sababu wanajivunia sana familia zao.
Wazazi wa Simba wanajiona kwamba wana nafasi kubwa katika dunia ambayo inawataka wajionyeshe kwa watu ubora. Pamoja na kwamba wenye nyota hii hupenda kuzunguka na watoto wao (na wao wenyewe wakati mwingine wana tabia ya utoto) hawakubali kupoteza heshima zao wakati wanafanya hivyo.
Wenye nyota hii ni wachangamfu, wenye moyo wa kupenda na wanapenda raha, pamoja na ukali wao wanaweza kuwa wepesi kwa watoto wao.
Watu wa simba kwa uhakika wanaona raha kuwa wazazi lakini wanatakiwa wawe makini kutowaharibu watoto wao kwa zawadi nyingi na maisha ya raha.
Simba wana uhakika na nafasi yao katika jamii kwamba wao ni viongozi hivyo watoto wao huwa wanapenda kujionyesha na wanategemea wawe wanaonekana kwa watu muda wote.
MADINI YA SIMBA:
(AMBER); Jiwe hili lenye rangi ya njano iliyochanganyika na kahawia linasemekana lina uwezo wa kumpa ukakamavu na ari ya uongozi kwa anayelivaa, vilevile linamwepusha mvaaji na maradhi ya kichwa.
UHUSIANO WA KIMAPENZI
(SIMBA NA NDOO):
Tabia ya Simba ya kutopenda kudhibitiwa au kudhibiti watu inakuwa ni faraja kubwa kwa wenye nyota ya ndoo ambao wanapenda uhuru na kufanya mambo yao bila kuingiliwa.
VYAKULA VYA SIMBA:
Wenye nyota ya simba wanatakiwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao.
Vyakula hivyo ni machungwa, maboga, vitu vichachu kama ndimu au malimao na wapende sana kula nyama za ng'ombe, mbuzi na kondoo.
NCHI ZA SIMBA:
Watu wa nyota ya simba wanatakiwa wakaishi au watembelee nchi zifuatazo ambazo zinatawaliwa na nyota yao.
Nchi hizo ni Italia na Morocco na miji ni Bombay (India) na Roma (Italia)
RANGI ZA SIMBA:
Watu wote wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi zilizochangamka na zenye kuonyesha utajiri
Ukitaka Usafishwe Nyota yako ili ipate kung'ara na kuwa na bahati na ukitaka Pete yako ya Bahati na kinga Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu.
Aries are so mean.
Hello mikia mwenzangu !hata mimi sikujua kama zile pyshing zangu na kutoogopa watu ni kiburi!Aise simba kumbe tuna viburi eeh. Ila mi sikuhizi sina kiburi mbona[emoji87]
Utakosaje kuwa na kiburi? wakati ndio tabia yako ya kila siku hiyo.Kitendo cha kunikatalia kuwa siku hizi huna kiburi peke yake hicho ni kiburi bora ungelinyamaza kimya. Kiburi chako umekionyesha hapa hata kunipa neno (Like) umeshindwa? hiyo pia ni dalili ya wewe kuwa na kiburi tosha. Huna Shukran nimekutajia nyota yako hata kunipongeza umeshindwa?Aise simba kumbe tuna viburi eeh. Ila mi sikuhizi sina kiburi mbona[emoji87]
Vipi na hapo kwenye kutumia na kujitanua na kupenda ufahari?Hello mikia mwenzangu !hata mimi sikujua kama zile pyshing zangu na kutoogopa watu ni kiburi!
Ha ha haa basi sawa umeshinda lolUtakosaje kuwa na kiburi? wakati ndio tabia yako ya kila siku hiyo.Kitendo cha kunikatalia kuwa siku hizi huna kiburi peke yake hicho ni kiburi bora ungelinyamaza kimya.
Mimi ndio usiseme niko vyema kwa bata hivi ninavyo chat niko kwenye boat kutoka znz naelekea Dar kwa wikiend kurudi jpili jioni.Vipi na hapo kwenye kutumia na kujitanua na kupenda ufahari?
Naeza sema upande wangu hapo ni kweli[emoji85]
Acha kunifanya nicheke bana[emoji3]Utakosaje kuwa na kiburi? wakati ndio tabia yako ya kila siku hiyo.Kitendo cha kunikatalia kuwa siku hizi huna kiburi peke yake hicho ni kiburi bora ungelinyamaza kimya. Kiburi chako umekionyesha hapa hata kunipa neno (Like) umeshindwa? hiyo pia ni dalili ya wewe kuwa na kiburi tosha. Huna Shukran nimekutajia nyota yako hata kunipongeza umeshindwa?