Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Mzee Kikumbi Mwanza Mpango, maarufu kama King Kiki, ana wimbo wake mmoja maarufu ambao anaimba "fungua njia, kitoto chaanza Tambaa"!
Mchungaji anakuomba Mtanzania fungua moyo na njia, Kitoto kimeanza tambaa!
Kama kuna jambo lililotoa msisimko mkubwa na kujenga hisia mpya za kimapinduzi ndani mwangu kutoka kwa Wanasiasa wa Tanzania katika miaka ya karibuni, ni hotuba ya Ndugu yangu Zitto Kabwe aliyoitoa Busanda, wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo kutafuta mbunge.
Hotuba ya Zitto imebeba kilio cha kila Mtanzania anayelilia haki, anayelilia maslahi, anayelilia tumaini, anayelilia ahueni aachane na Umasikini, Ujinga na Maradhi ili Mtanzania huyu aweze kuwa mshiriki kamilifu katika ujenzi wa nchi yake na afaidi matunda ya nchi yake.
Tofauti na hotuba za Wanasiasa wawe wa CCM au Upinzani, Zitto kanivutia kwa kitu kimoja, hakutoa ahadi hewa, bali katoa wito wa kuwaomba Watanzania kama wanajali nchi yao na hawaridhiki na hali halisi iliyoko nchini, basi jimbo la Busanda lisiangukie tena kwa CCM kama mazoea.
Hotuba yake imenikumbusha hotuba zile za Wanamapinduzi wa Afrika waliopigania Uhuru wa Afrika. Nyerere, Kenyatta, Kaunda, Cabral, Balewa, Azikiwe, Ben Bela, Lumumba, Nkrumah, Toure na wengine wengi ambao ndio walikuwa mstari wa mbele katika kuleta ukombozi kwa Afrika kutoka kwa makucha ya Wakoloni.
Hali yetu Tanzania sasa hivi chini ya CCM haina tofauti na msukumo wetu tuliouanza tangu vita vya kina Mtemi Mkwawa, Isike, Mangi Meli, Mirambo, Abushiri, Kinjekitile, mpaka walioanzisha TAA, TANU na hata UMMA, ZNP na hata ASP. Walichokifanya wahenga wetu ni kupigana vita vya nguvu, hoja na itikadi mpaka tukaushinda ukoloni na Mkoloni akakubali kushindwa na kuridhia kutuachia nchi yetu tujiongoze.
Zitto ametusaidia sisi wote Wanaharakati tunaotaka kuleta Mapinduzi mapya Tanzania, iwe tukiwa ni wafuasi wa CCM au vyama vya Upinzani, kwa kutoa hotuba moja iliyoshiba na nono kumuamsha Mtanzania atambue kuwa mazoea ya kuchagua CCM bila kudai uwajibikaji hayafai.
Nasema kuwa Nyota ya Magharibi imeng'aa, mbegu imechipua na kitoto kimeanza kutambaa ni kutokana na furaha niliyonayo kuona kuwa tulichokuwa tukimfunda Zitto kwenye kumbi zetu na kumdai azinduke, kumeleta matunda kwa yeye kuamka wakati muafaka na kutoa hotuba yenye ujumbe mkubwa kama huo.
Sidhani kama wengi wetu, tulikuwa tayari wala kutumaini kuwa kuna siku kilio chetu kitapewa matangazo ya bure na yenye nguvu kama hotuba hii.
CCM kwa muda mrefu wamekuwa wakitufanya sisi Watanzania kuwa ni wajinga, wametunyanyasa na kutunyonya na kutuacha tuwe wanyonge. Sina maana kusema Zitto ni shujaa basi nasi tupumbae kuimba nyimbo kumtukuza kuwa ni shujaa, bali ni kumshukuru Zitto kwa kuwa jasiri na kutoa msimamo uliojaa upendo, umakini na wala si vitisho au ahadi.
Zitto katoa wito kwa Watanzania kuanza kuiambia CCM, hatufurahii inachokifanya.
CCM ni kichwa ngumu, nami pamoja na mapenzi yangu kwa CCM, nimekuwa nikikiri kwa muda mrefu sana kuwa kuna haja ya kufanyika mapinduzi ya kuifanya CCM izaliwe upya.
Mwalimu Nyerere alisema Upinzani makini utatokea CCM. Je hotuba hii ya Zitto itazaa matunda ya kutimilika maneno ya Mwalimu Nyerere? Je wale Wabunge Magwiji wa CCM wanaodai kuwa wao ni Wapiganaji wenzetu, watakuwa tayari kusimama mguu sawa na kwa mwendo mkakamavu kukibadilisha Chama chao kianze kulitumikia Taifa?
Najua wengi wetu tutasema laiti kama Zitto angekuwa na umri sawia ili agombee Urais mwakani wakati wa uchaguzi mkuu, mimi nitasema, Zitto wala hana haja ya kufanya pupa.
Amepanda mbegu bora, kazi inayofuatilia ni kupalilia, kunyeshea, kuwekea mbolea, kuondoa magugu na kuendelea kuulea mmea ili utoe mazao bora.
Safari ya kuiamsha CCM imepata nishati na nguvu mpya, nasi tujiunge pamoja na kumpasha na kumhoji kila Mtanzania awe mkweli kwa nafsi yake kama anaridhika na hali ya Maisha yake na Uongozi wa CCM ambao umekomaa kwa miaka 48 na haujaleta matunda yaliyo bora ya muda mrefu kutuletea neema ambayo itatuondoa kwenye utegemezi na unyonge.