Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,898
- 828,504
Maji ni kitu chenye nguvu sana!
Kamwe usijaribu kuyazuia yanapochagua njia yake, maana hutayaweza. Ukijaribu, yatakusababishia madhara makubwa!
Ni wakati wa mabadiliko… Hayazuiliki! Na kujaribu kufanya hivyo ni kujitafutia shida za kujitakia.
Nyota waliohamasisha na kufanikisha maandamano ya kudai haki ya October 29, kwa sehemu kubwa, walikuwa ni watu wa jinsia pinzani ya kiume.
Ninaposema nyota, namaanisha kwamba wapo wengi waliohusika, lakini ninaowataja hapa ni wale waliotamba zaidi.
Kutoka upande wa wanawake:
Kabla ya MO29, Pole Pole alijizolea umaarufu kutokana na kutoa data ambazo chanzo chake kilikuwa yeye mwenyewe. Watanganyika wengi waliona anawachana kisawasawa.
Mange naye akawa anapewa taarifa za ndani, na akawa anazipenyeza bila woga.
Lakini pamoja na nguvu yote hiyo, maandamano yale yakatawaliwa na kiwango kikubwa cha ukatili ulioteketeza maelfu ya roho zisizo na hatia — pamoja na majeruhi, makovu na ulemavu wa kila aina.
Hata hivyo, matakwa ya MO29 hayakutekelezwa.
Hii ikapelekea maandalizi ya maandamano ya D9, siku ya Uhuru wa Tanganyika.
Maandalizi ya D9, pamoja na wale nyota wa MO29, yamemuibua mtu mpya kabisa mahiri, mwenye nguvu, na hatari zaidi.
Huyu mtu ni kama jeshi la mtu mmoja, aliye full loaded kwa kila aina ya silaha kubwa na ndogo, za masafa marefu na mafupi.
Na huyu si mwingine bali ni:
Habil Kabil
Ana mbinu za kipekee za kuwasiliana na wale wanaowekwa kwenye rada yake:
Na mara zote anakupa chaguzi mbili tu: A au B.
Kila analoibuka nalo linatisha kuliko lililotangulia. Kwa sasa, watu hawalali hawajui nani ndiye anayefuata na atawekewa ultimatum gani.
Wengi wangetamani wasahauliwe mpaka D9 ifike… lakini kwa hali ilivyo sasa, inaonekana hakuna atakayebaki. Kila mmoja ataandikiwa wakati wake.
Jana, mbali na taasisi iliyoguswa kwa sehemu, ni Bwana Subwoofer aliyeibuliwa na kashfa ya kughushi na amepewa ultimatum ya siku 7 ajitafakari na kujibu.

- Mange Kimambi
- Maria Sarungi
- Rachel Danga
- Sativa
- Pastor Dickson
- Nuru Vazi
- Pole Pole
- Gwajima, n.k.
Kabla ya MO29, Pole Pole alijizolea umaarufu kutokana na kutoa data ambazo chanzo chake kilikuwa yeye mwenyewe. Watanganyika wengi waliona anawachana kisawasawa.
Mange naye akawa anapewa taarifa za ndani, na akawa anazipenyeza bila woga.
Lakini pamoja na nguvu yote hiyo, maandamano yale yakatawaliwa na kiwango kikubwa cha ukatili ulioteketeza maelfu ya roho zisizo na hatia — pamoja na majeruhi, makovu na ulemavu wa kila aina.
Hata hivyo, matakwa ya MO29 hayakutekelezwa.
Hii ikapelekea maandalizi ya maandamano ya D9, siku ya Uhuru wa Tanganyika.
Maandalizi ya D9, pamoja na wale nyota wa MO29, yamemuibua mtu mpya kabisa mahiri, mwenye nguvu, na hatari zaidi.
Huyu mtu ni kama jeshi la mtu mmoja, aliye full loaded kwa kila aina ya silaha kubwa na ndogo, za masafa marefu na mafupi.
Na huyu si mwingine bali ni:
Habil Kabil
- Bingwa wa mipango na mifumo
- Mtu mwenye ushawishi wa ajabu
- Mdukuzi hatari
- Anayedukua kila kitu, kidogo au kikubwa — na kila alichonacho ni silaha kuelekea D9
- Kwa sasa, ndiye mtu anayesikilizwa zaidi Tanganyika kwenye live talks mitandaoni
Ana mbinu za kipekee za kuwasiliana na wale wanaowekwa kwenye rada yake:
- Barua/Fax
- Simu
- Live talks mitandaoni