Nyoka ni marafiki zetu na sio maadui, tusiwadhuru bila ya sababu bali tujenge nao urafiki

Nyoka wapo wa aina nyingi

Kuna vinyoka vya kawaida huwa wanapatikana kwenye miti majumbani hao hawana madhara ndio maana MTU anaweza kungatwa kwa bahati mbaya na kwenda hospitali hata kwa kuchelewa madhara hakuna

Kuna jamii ya nyoka hatarishi ambao huishi msituni kama koboko hawa wana sumu kali ndio maana wanaishi misituni na hata hawa usipowasumbua hawawi aggressive ila ukiwasumbua wanakuwa aggressive kama vile paka

Paka ni rafiki ila ukimsumbua na kumkanyaga mkia anakuwa aggressive
Jambo lolote pasi na elimu ni shida, jamii yetu ina elimu ya kutosha ya nyoka? Wewe wasema hayo tyr una elimu ya kutosha. Pia nyoka huishi kwa kujificha hakai wazi, usidhan watu hupenda kuwakanyaga kuwakalia au kuwabana makusudi na hapo ndio vita huanzia. So, heri kujihami nao mapema na ujue hata hospitali nyingi hazina tiba mahususi za nyoka.
 
Mtoa mada unanishawishi kwa maneno yako ila aaaaah mi siwapend kama vile nisivyopenda mjusi na jamii yake mi nikiona nafukuzia mbali
 
Nyoka hana urafiki na binadam
Ndo maana wafuga nyoka humtoa sumu na meno

Ata Biblia imeandika uadui wa nyoka na binadam
 
Nyoka ni kiumbe kilicholaaniwa, tayari alishawekewa uadui kati yake na binadamu pale alipomdanganya Hawa kula tunda, alilaaniwa na hata Mungu alimwambia ataweka uadui kati yake na (mwanamke) binadamu, na atapondwa kichwa (nyoka) na mwanamke(binadamu) atapondwa kisigino na nyoka!
Na hii ndio sababu kubwa ya madhila yanayowakumba nyoka, hizi fiction ni uongo, lkn sababu binadam hatupendi kufikiri, basi tumeamini na tumekubali kwamba nyoka popote pale anapaswa kuuliwa.
Dini zimeleta maafa mengi si kwa binadamu tu, bali kwa wanyama wengi pia.
 
Wakati watu wanayakimbia matatizo kuna watu wanayakimbilia matatizo....kuna mambo mengi ya kunukuu ambayo yanaweza kushangaza mf.kuna mtu aliwahi kusema ukikaa kuwatafiti binadamu na akili zao (wanachowaza na kuamini)utaishia kuwa chizi.Hali kadhalika imezoeleka viumbe vingi kuukimbia uchafu lakini utashangaa inzi au funza wanaupenda na kuukimbilia uchafu!!! Ila suala la kuaminisha umma kuwa nyoka ni rafiki wa watu ni jambo la kushangaza...Labda uwe tu unafanya utafiti wa nyoka au ni mwana mazingaombwe.
 
Kitendo cha mamia wa binadam kuwa hivyo ni kuwa nyoka ni wakorofi
Mbona paka wanaishi na binadam na watu huwadhuru wanawaacha2 waendelee na maisha yao
Ila nyoka ni mkorofi na anaua ndo maana mpaka sahv hunishawishi
 
Yaani muda wote umejipinda kuandika upuuzi huu, kwanini huu muda usingeutumia kumshauri Bashite azuie kuangalia ligi za ulaya ili soka letu lipande kiwango.
..Mr.Bahinda habar yako,ulivo mjibu huyo bwana khs story ya nyoka hujamtendea haki hata kidogo,always jifunze kupokea unachokipenda na kile usichokipenda kwn daima utajijengea busara na skills kila uchao.
 
Alikubali kutumika na shetani
Ata adui yako akimtumia mtu mwingine kukudhuru na wewe pia utamchukia
Wachawi wanawatumia paka

Ina maana tuwachukie paka
Ina maana paka wamelaaniwa

Shetani ,mchawi anaweza kuigeuza mithili ya chochote hata kondoo ,binaadamu nk

Mara ngapi watu husafiri na kumkuta MTU mrefu katikati ya barabara na kusababisha ajali ina maana binaadamu kalaaniwa ?

Au watu wenye mapepo mara nyingine huua hidhuru kwahiyo mwenye makosa ni binaadamu sababu kamtumikia shetani au shetani ndio mwenye makosa?
 
Nyoka ni kiumbe kilicholaaniwa, tayari alishawekewa uadui kati yake na binadamu pale alipomdanganya Hawa kula tunda, alilaaniwa na hata Mungu alimwambia ataweka uadui kati yake na (mwanamke) binadamu, na atapondwa kichwa (nyoka) na mwanamke(binadamu) atapondwa kisigino na nyoka!
Na maandiko yote lazma yatimie kabla ya kizazi hiki kupita..
Halitapita hata punje la andiko bila kutimia kabla ya kizazi hiki kupita
 
Nyoka ni kiumbe kilicholaaniwa, tayari alishawekewa uadui kati yake na binadamu pale alipomdanganya Hawa kula tunda, alilaaniwa na hata Mungu alimwambia ataweka uadui kati yake na (mwanamke) binadamu, na atapondwa kichwa (nyoka) na mwanamke(binadamu) atapondwa kisigino na nyoka!
Na maandiko yote lazma yatimie kabla ya kizazi hiki kupita..
Halitapita hata punje la andiko bila kutimia kabla ya kizazi hiki kupita
 
Ndugu zanguni kuna tabia ambayo imezoeleka miongoni mwa wengi kila waonapo nyoka wanawapiga na mawe,magongo na silaha aina yeyote ile mpaka wanawaua hata pale nyoka akiwa sehemu pekee yake ametulia bila bughudha yeyote ile ila utashangaa mtu anaanza kupiga yowe na kuita kadamnasi ya watu na kisha kumshambulia nyoka ambaye alikuwa amejituliza zake tu.

Kwanini tunawachukia kwa kiasi kikubwa nyoka?

Watu wanadai Nyoka ni adui ya binaadamu lakini tusisahau sisi ndio tunaojenga uadui nao sababu kila tukiwaona tunaanza kuwashambulia hata kama hawakuwa na kosa ya aina yeyote ile

Mfano hawa nyoka wa majumbani green snake au black snake ambao kipindi cha baridi hukimbilia majumbani kwa watu kutafuta joto.

Nakumbuka nilivyokuwa mdogo maeneo ya Mbeya hawa nyoka walikuwa na tabia ya kuingia ndani kutafuta joto na hawakuwa na nia yeyote ile mbaya lakini cha kushangaza huyo nyoka akionekana watu huanza kupiga yowe na kisha anauliwa kikatili badala ya kupewa msaada wa joto,anakimbia shida na anakutana na dhahma.

Ili kuthibitisha nyoka ni marafiki zetu na sio maadui wetu nadhani wengi ni mashahidi kuna wakati nyoka akikimbia baridi na kutafuta hifadhi yenye joto hukimbilia majumbani na wakati mwingine hujibanza karibu na mtu ,wangapi wanalala na nyoka bila ya kujijua?na wengine wakishafahamu wamelala na nyoka wakistuka wanaanza kupiga yowe kisha kumuua nyoka huyo.Inashangaza sana huyo nyoka angetaka kukudhuru basi angekudhuru kitambo sana kwani hajui kama amejibanza karibu na mtu?

Kwani harufu ya mtu haifahamu lakini kutokana hakubughudhiwa na yeye shida yake ni joto hivyo ameamua kujisogeza karibu na shuka apate joto akishapumzika anakwenda zake..lakini sie tunachowafanyia sio haki kabisa

Pia ni kesi ngapi tunashuhudia watoto wadogo wakicheza na nyoka tena muda mrefu bila kudhuriwa ,sababu haswa nyoka sio adui na mtoto hajui kudhuru

Kwa hizi sababu mbili tufahamu nyoka ni rafiki na sio adui lakini rafiki maisha yake yakiwa hatarini lazima ajilinde na njia sahihi ya kujilinda ni kushambulia

Nawasihi ndugu zangu sio kila tukimuona nyoka tunapiga mayowe na kuanza kutafuta mawe,fimbo na kuanza kuwashambulia ,sisi ndio tunawafanya wakasirike lakini nyoka ni marafiki haswa nyoka wa majumbani hawa na pale wakitafuta hifadhi ya joto tusiwadhuru

Mie hawa nyoka wamenisaidia sana kunisafishia shamba na nyumba ,wadudu kama mende ,panya na aina wafananao wameisha sababu ya hawa home snakes wana msaada sana.
Kwahiyo dini unayoiamini ndio imekwambia hivyo kuhusu mahusiano ya binadamu na nyoka?
 
Kwahiyo dini unayoiamini ndio imekwambia hivyo kuhusu mahusiano ya binadamu na nyoka?
Why useme dini na siyo nature au scientific au tafiti yoyote ile.

Wazungu wangekuwa na hizi mitizamo wasingekuwa wanafanya tafiti mbali mbali na maendeleo yasingepatikana
 
Back
Top Bottom