Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,264
Kweli inawezekana hivi vifo ni vya kawaida? Tunaopenda kutafakari kidogo tunaona kuwa si rahisi kuamini hivi hivi tu. Sijamfahamu huyo Nyiti kwa uzuri ila nadhani ni milionea fulani. Mawalla na Sambeke walikuwa mabilionea, na hawa kwa kiasi kikubwa walikuwa mstari wa mbele kuunga mkono upinzani nchini. Kuna tetesi kuwa tangu M4C ianze baadhi ya hawa wadau wamekuwa mchango mkubwa sana kwa kukua kwa vuguvugu hili. Kwa nini hizi roho zipotee bure na kwa urahisi hivi?