Nyimbo za Maombolezo za Kumuaga Rais. John Pombe Joseph Magufuli

SEASON 5

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
481
1,000
Nyimbo nyingi zimekua zikitungwa kwa ajili yakuonyesha namna tulivyompenda Rais wetu, nadhani kila mtu ana nyimbo ambayo kwa namna moja ama nyingine akiisikiliza anajikuta anatonesha kidonda anaanza umia upya.

Kwa upande wangu nimeguswa sana na nyimbo mbili ambazo ki ukweli nimezipenda nimezi verify kweli zinagusa moyo na ni nyimbo kweli za maombolezo, ambazo zikipigwa msibani ni hakika utaumia kwanamna ya mashairi yake yalivyo pangiliwa.

No.1 nimeupa wimbo wa ASLAY - BYE, hakika aslay kaimba huu wimbo ndugu zangu, huwa napenda nyimbo mpya sipendi nyimbo zakutumia beat za nyimbo zilizopita ktk nyimbo hizi za maombolezo basi aslay kaniliza na anaendelea kuniliza.



No. 2 Naupa wimbo wa Tanzania All stars - Lala Salama huu wimbo ndugu zangu sikiliza tu audio yake utulizane, ila kama unampenda Magufuli kama ninavyompenda mimi au anavyompenda mama Janet usije logwa ukaangalia Video ya Huu wimbo. Huu wimbo utakutibua tibua na kukushusha upya machozi yaliyokauka.

Audio yake ina mashairi mazuri kila msanii kaimba anachojiskia ni huzuni na maombolezo lakini Video ya Huu wimbo inahuzunisha mara 100, hakika Rais wangu amelala, hakika ameenda kupumzika.




Naomba kila mwenye Audio video atakayoiona au ipata popote iliyomgusa asisite kuisogeza hapa, natamani pata audio na video zote za kila aliechukua muda wake kumuimba magufuli nimsikilize. Asanteni na karibuni
 
Mwenye audio ya nyimbo ya Peter msechu- Magufuli umetuacha Imara ,Tanzania salama naomba anisaidie hapa jukwaani please
 
Nenda shujaaa kijitonyama uinjilist naambatanisha audio
FB_IMG_1616407846496.jpg


Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Wekeni Wa TOT. Na mwenye wimbo Wa Komba baada ya maziko ya Mwl Nyerere wenye maneno "Ugonjwa huu sitapona..."
 
Back
Top Bottom