Nyie mmemuelewa mama ?

Nyie mmemuelewa mama ?

Samia kaongea kwa kuelewa kuwa Tanzania ishasaini mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu. Labda watu ambao hamjatoka Tanzania, au hamjafuatilia hili jambo kwa karibu kimataifa, mnaweza kuwa na ugumu wa kuelewa hili jambo kutokana na muktadha wa kimataifa. Kimataifa, haki za mashoga ni sehemu ya haki za binadamu. Yani ni sawa na haki za watu weusi kutotaka kubaguliwa kwa rangi ya ngozi zao.

Ndiyo maana hata kabla Samia hajawa rais,Makonda aliwaandama mashoga, halafu ikabidi Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Balozi Dr. Mahiga aje kusawazisha mambo na kusema maneno yale yalikuwa ni ya Makonda binafsi. Si ya serikali. Na jibaba mwenyewe anayependa kuwasema mabeberu (Jiwe) alikaa kimya. Kwa sababu alijua mziki ule ni wa kimataifa hatauweza.

Samia hana ubavu wa kulianzisha kwenye ushoga wakati kila siku anaongea na kina Kamala Harris wanampa somo, na yeye misaada anaitaka.

Zaidi, suala la ushoga kwa watu wazima ni jambo la kulindwa ki faragha za kikatiba , nchi za kidemokrasia hazibagui watu kwa dini, rangi, kabila, umri wala sexual orientation. Mkianza kubagua watu kwa sexual orientation kwa sababu ni minorities tu, basi hakuna sababu ya kutobagua minorities wengine wowote.

Samia kasema exactly alichotakiwa kusema katika ulimwengu huu.

Watu wazima wana haki ya kufanyana wanavyotaka, si kazi ya serikali wala kazi yako kuwaingilia.

Watoto wadogo hawatakiwi kuingiliwa kivyovyote vile, bila kujali ushoga au straight.

Ila, naelewa Watanzania wengi sana bado hawaelewi suala la autonomy.

Yani ni hivi, kama wewe usivyopenda ushoga na ukaachiwa kuwa na haki zako uwe na mtu wa different sex, kuna watu hawataki kuwa na mtu wa different sex wanataka kuwa na mtu wa same sex. Kama wewe usivyitaka kulazimishwa ufanye usichotaka, na wao pia hawataki kulazimishwa wafanye wasichotaka.

As long as ni watu wazima, hawajalazimishwa, wewe kinachokuwasha ni nini?

Serikali iache kufukuzana na wezi aliowataja CAG ije kuangalia nani anamfira nani? Kwa watu wazima wenye akili zao na walioamua wenyewe kufanyana wanachotaka?

Na nyie watu wazima mnaona sawa hilo?

Mimi si mshabiki wa Samia, lakini katika hili namuunga mkono.

Zaidi ya argument za kidini, ambazo ni mufilisi katika nchi secular, hakuna argument dhidi ya ushoga kwa watu wazima waliokubaliana katika nchi inayothamini uhuru wa watu binafsi inayoweza kusimama.

Ila, Watanzania wengi hatuelewi uhuru binafsi ni nini, ndiyo maana watu wanapinga ushoga kwa mkumbo.

Wakati matatizo yao mengi makubwa ni ya kiuchumi, na wanayakubali tu bila ya kuyapinga.

Ni kama vile dini zime short circuit akili za watu wawe wana prioritize mambo yasiyo na priority, wakati mambo ya priority yanaachwa.

Ushoga ni kosa la jinai sio haki za binadamu. Tuache kuendekeza uchafu wa wazungu.
 
Tatizo Una assumptions zako kichwani ndio maana hata ukiambiwa ukweli huwezi kuelewa

Ukweli upi? Wewe ndio umeleta tafsiri yako kichwani na kulazimisha tuikubali. Rais kasema wakubwa fanyaneni ila msiwalegeze watoto. Wewe unatuletea tafsiri yako ya chumbani. Kiufupi Rais karuhusu ushoga kwa wakubwa.
 
Na nukuu maneno haya amesema hivi “Msiwalegeze watoto wetu fanyaneni wakubwa kwa wakubwa watoto waache”

Chawa nawasubiri muandamane kuunga mkono au kumpongeza mama yenu karuhusu fanyaneni wakubwa lazima tutaelewana tu dhambi tulioifanya itaturudiaView attachment 2581271
Hii kauli ni sawa kabisa, hivi karibuni kumekuwa na jitihada za kuinculcate huu ujinga kwa watoto hasa,kwenye boarding schools,kumbi za muziki na majumbani kwa kuwa tu mtoto anakuwa bado hajawa na maamuzi wenyewe,ukiangalia hata mashoga wengi watakuambia walifundishwa wakiwa wadogo hivyo kisaikolojia hawezi tena kuacha.hivyo basi tukitaka kuondokana na hili tatizo tuwalinde watoto wetu sana,hiyo ndio maana ya Rais, haya majitu mazima yanayojitambua yenyewe yaachwe yatakutana na mkono wa sheria.maneno mengine yeye ni mzanzibari,kiswahili na utani ndio hulka yao so muwe mnachambua hotuba wazee.Kwani hata JPM alikuwa anaingiza utani sana ila nia inakuwa njema
 
Tatizo wanajitangaza wazi wazi kupitia media n.k.
 
Point kubwa sana Mkuu.
 
Something must be wrong somewhere!

Kwakuwa tumeamua kuanzisha mjadala, acha tu tuendelee...

Unapaswa kufahamu kwamba kwenye maisha kuna masuala ya kisiasa, kidini, kiuchumi, kijamii nk.

Kwenye masuala ya kisiasa kwa mfano, unadhani kwanini taifa moja linapopigana na taifa jingine; mataifa mengine huingilia kati? Kwanini wasiachwe tu wapigane kadri watakapoishia?

Vivyo hivyo kijamii, watu tunategemeana kiutamaduni, mila na desturi. Unaporuhusu mila au desturi fulani zisizofaa kuingia katika jamii, unaathiri jamii nzima.

Huwezi kukaa kimya eti kwasababu ni maamuzi yao!
Nimekuuliza,wewe binafsi unathirika vipi na kitu ambacho hakikuhusu?

Watu wameamuakufanyana wanavyotaka wenyewe, miili yao, wao watu wazima, wamekubaliana.

Nakuuliza, unaishia kunijibu something must be wrong na mifano isiyoeleweka.

Kwenyemasualaya kisiasa nakwambia tushasaini mikataba ya kimataifa ya kutetea haki a mashoga, sasa kama hatuzitaki, kwa nini tuli sign?

Mila na utamaduni ni weak argument, kwa sababu kwanza hatujakubaliana mila na utamaduni, pili mila na utamaduni zinabadilika, zamani tulitahiri wanawake, siku hizi tunaacha.

Hujtoa sababu nzuri za kukataza ushoga kwa watu wazima walioamua wao wenyewe kuwa mashoga.
 
Ushoga ni kosa la jinai sio haki za binadamu. Tuache kuendekeza uchafu wa wazungu.
Ushoga ni nini kwanza? Mana tusibishane kuhusu ushoga kumbe hujui hata ushoga ni nini.

Watanzania wengi wanahusisha ushoga na tendo la wanaume kufirana au wanawake kusagana.

Unaposema ushoga ni kosa la jinai unamaanisha nini? Sodomy?

Unaelewa sodomy mtu mume anaweza kumfanyia hata mkewe?

Ndiyo unamanisha hiyo?
 
Mama kakulia kwenye utamaduni huo huko zanzibar. Toka akiwa msichana anayasikia hayo. Mzee Juma kamkaza Abdul. Kwa hiyo si kitu kigeni.

Sie wabara haya mambo ni mageni na pengine yametokea zenji huko huko. Miaka ya zamani tuliwaogopa sana wapemba na watu kutoka Mombasa. Ilikuwa tusi kubwa kumuambia mtu nitakupeleka Mombasa au Lamu. Tuliyasikia tu kutokea kanda hizo.

Hizo ni kanda alizokulia mama. Kwa hiyo bado anaamini hayo mambo yanaweza fanywa ila wafanye wakubwa kwa wakubwa. Sio wakubwa kuwafanya watoto.

Lakini mama anashindwa kuelewa kuwa haya mambo huanzia utotoni, ukubwani ni muendelezo tu. Hakuna anayeanzia ukubwani. Labda iwe fumanizi la mke wa mtu.
 
Kwa mantiki hii basi hata wadada wanaojiuza wachwe na wasisumbuliwe kukamatwa maana ni watu wazima wana haki ya kuamua, Si ndio tumefika huko?

Watumiaji wa madawa ya kulevya ( bangi nk) waachwe maana wana haki ya kuamua! Hakuna sababu ya kuwa na sheria maana kila mtu ana haki ya kuamua!

I see! Njaa haijawahi kumuacha mtu salama!
Na watu wazima wanao amua kujiuwa nao waachwe wajiuwe, maana wameamuwa wao Kama watu wazima!!
 
Umeuliza maswali ambayo ni illogical.
Hayana mantiki kabisa. Yaani kwasababu uko tofauti ndio ushindwe kujisimamia?

Swali la msingi ni je, hao wanaofanya, wanafanya ili iweje? Nini athari za wao kutofanya?

Tujue wazi ushoga ni tendo la mwanaume kumuingizia mwanaume mwenzake uume kwenye sehemu ya haja kubwa.
Kimaumbile mifumo ya binadamu imegawanyika katika hali tofauti.

Tukizungumzia mfumo wa uzazi, ndio maana mwanamke ana uke unaouruhusu mbegu za mwanaume kwenda kurutubisha mayai.

Sasa huko kwenye sehemu ya haja kubwa unabadili matumizi na ndio maana athari ni kubwa. Watu wanaoza. Wanatokwa na kinyesi muda wote na inabidi kuvaa diapers kama watoto.. Ifike mahali tuache kutetea huu upuuzi. Hata hao wanaofanyiwa hujuta sana baadae!
Mkuu huyu usimjibu tena tumeshajua yeye ni nan hasa.
Anatoa hoja za ovyo mno afu anataka wenye akili tumuelewe kirahisi.
Yeye anaamini kila jambo linaloanzishwa na mataifa ya magharibi kwa kisingizio cha Haki za binadamu ni jambo jema ovyo kabisa hili dubwana.
 
Ashki zinaanza katika umri ambao bado wanatambulika kama watoto lazima wapewe muongozo, kwahiyo hatuwezi kusema hili jambo halihusu watoto. Hapa ni mwanzo tu bado wanataka waingize hayo mambo kwenye mitaala yetu, watoto wako targeted, wanakataa hamna agenda lakini ni wazi agenda ipo. Viongozi wetu wamefeli.
Mama kakulia kwenye utamaduni huo huko zanzibar. Toka akiwa msichana anayasikia hayo. Mzee Juma kamkaza Abdul. Kwa hiyo si kitu kigeni.

Sie wabara haya mambo ni mageni na pengine yametokea zenji huko huko. Miaka ya zamani tuliwaogopa sana wapemba na watu kutoka Mombasa. Ilikuwa tusi kubwa kumuambia mtu nitakupeleka Mombasa au Lamu. Tuliyasikia tu kutokea kanda hizo.

Hizo ni kanda alizokulia mama. Kwa hiyo bado anaamini hayo mambo yanaweza fanywa ila wafanye wakubwa kwa wakubwa. Sio wakubwa kuwafanya watoto.

Lakini mama anashindwa kuelewa kuwa haya mambo huanzia utotoni, ukubwani ni muendelezo tu. Hakuna anayeanzia ukubwani. Labda iwe fumanizi la mke wa mtu.
 
Mkuu huyu usimjibu tena tumeshajua yeye ni nan hasa.
Anatoa hoja za ovyo mno afu anataka wenye akili tumuelewe kirahisi.
Yeye anaamini kila jambo linaloanzishwa na mataifa ya magharibi kwa kisingizio cha Haki za binadamu ni jambo jema ovyo kabisa hili dubwana.
Nashangaa eti mambo ya faragha, sasa huku nje yamefikaje?
 
Wanaojiuza na wanaotumia madawa ya kulevya hawana mikataba ya kimataifa inayotetea haki zao.

Unalinganisha mambo tofauti.

Kitu cha kulinganisha hapa ni hivi.

Je, wewe ambaye si shoga, ungelazimishwa kuwa shoga ungejisikiaje?

Au, leo ungekuwa katika dunia ambayo wengi ni mashoga, halafu wewe si shoga unabaguliwa, kwa sababu si shoga, watu wanakulazimisha uwe shoga, ungejisikiaje?
Kwa hiyo unawashauri wanaojiuuza na wanaotumia madawa ya kulevya nao wa apply Mikataba ya kimataifa ili kutetea haki zao! pia!?
 
Kwa hiyo unawashauri wanaojiuuza na wanaotumia madawa ya kulevya nao wa apply Mikataba ya kimataifa ili kutetea haki zao! pia!?
Sina tabia ya kutoa ushauri ambao sijaombwa, kwa watu nisiowajua, kwenye mambo nisiyoyafahamu.

Hizi ni tabia ambayo nimeona Watanzania wengi wanayo, lakini mimi naikwepa.
 
Samia kaongea kwa kuelewa kuwa Tanzania ishasaini mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu. Labda watu ambao hamjatoka Tanzania, au hamjafuatilia hili jambo kwa karibu kimataifa, mnaweza kuwa na ugumu wa kuelewa hili jambo kutokana na muktadha wa kimataifa. Kimataifa, haki za mashoga ni sehemu ya haki za binadamu. Yani ni sawa na haki za watu weusi kutotaka kubaguliwa kwa rangi ya ngozi zao.
Mbona M7 na Ruto wana uthubutu wa kusema wazi kuwa hawataki ushoga kwenye nchi zao?
Sisi kama nchi tunaweza kusema tu kuwa haki za binadamu tunakubali, lakini kipengele cha ushoga ni HAPANA!
 
Back
Top Bottom