BAKWATA haipo siku hizi? Evangelical Lutheran Church of Tanzania haipo?
Zipo, lakini kwanza zenyewe haziko above suspicion. BAKWATA kila siku ina migogoro na makundi mengine ya Kiislamu, hao Walutheri kila siku wana ugomvi huko dayosisi za kaskazini, who is to say BAKWATA hawata inflate figures ili wawpiku rivals wao? Au dayosisi hazitashindana ku inflate figures? Not that serikali ikihesabu ndo utapata perfect figures, but at least ukweli kwamba serikali inahesabu utapunguza figure inflation.
Pili, kuna madhehebu ambayo hayapo katika hizo habari za BAKWATA na wa Lutheri. Kuna kina Kakobe huko, uamsho etc ambao wanaweza ku inflate figures. Au kufanya watu wafanyiwe double counting.
Serikali inategemea figures za madhehebu? Sawa, mtu anakwenda kwenye msikiti wa BAKWATA na msikiti wa uamsho, na kote anahesabiwa.
Mwingine anasali kwa Koakobe na Lutheran. Kote anahesabiwa. Mwisho wa siku sensa inaonyesha wananchi wako milioni hamsini, lakini waumini wako milioni mia.
Unaona ugumu hapo?
Kwani Waislam wote ni uamsho? Misikiti yote iliyopo Tanzania imejaa wana uamsho? Binafsi sioni kabisa umuhimu hata wa kuuliza dini kwa sababu kama sisi wote ni Watanzania nadhani demographic information zinazopatikana kutoka kwenye sensa zinatosha kabisa katika kuunda public policy inayokidhi mahitaji muhimu ya watu.
Serikali ikibali kuhesabu watu kwa dini precisely kwa sababu waislamu wote si uamsho. haina cha kuhofia. Ikianza kukataa kuhesabu watu kwa dini inaipa uamsho msemo. Hata wale waislam waliokuwa hawaamini conspiracy theory ya uamsho wanaanza kusema "mbona serikali inaogopa, au ni kweli inaficha mambo kwa sababu inaonea waislamu nini?". Serikali itapoteza support hata ya wale waislam waliokuwa hawana sympathy na uamsho.
Serikali haina cha kupoteza kwa kuweka swali la dini katika sensa.In fact habari hizi zitasaidia katika research zinazohusu mambo ya public policy.
Kwa kutokujumuisha swali la dini serikali sio tu itajinyima yenyewe data credible zinazoweza kuwa na relevance katika public policy, itawapa hawa nutcases wa uamsho msemo, watasema "si mnaona, serikali inaogopa kuweka swali la dini katika sensa kwa sababu inaogopa nguvu ya ummat, takdeeer!!!!!"
Sote ni Watanzania bila kujali dini wala rangi wala mwelekeo wa kijinsia na kadhalika. Dina za watu hazihusu wengine. Kwa hiyo tusiruhusu yeyote yule atuambie yeye ana waumini wangapi. Haituhusu sisi.
Dini zitatuhusu pale tutakapokuja kugundua kwamba wakristo na waislam wahafidhian wanakataza kuvaa condom na hili linarudisha nyuma vita dhidi ya Ukimwi nchi nzima.
Hapo utaona public policy (vita dhidi ya UKIMWI) itataka kujua wapi wamekusanyika sana wakristo na waislam na wahafidhina wao wako wapi ili kujua kuwaingilia vizuri ili kupata ushirikiano katika vita dhidi ya UKIMWI.
Hii habari ya kwamba "dini ya mtu haituhusu" ni uongo, kwa sababu no person is an island, na as long as dini ina influence maisha ya mtu mmoja, ina influence maisha yetu wote.
Unaona sasa...ndiyo maana tusihesabu dini. Kama kanisa Full Gospel Bible Fellowship lina congregation ya watu 25,000...good for them. The bottomline is they are Tanzanians too.
Swali linakuja, utajuaje kama Kakobe haja inflate figures ili kupata hela za donors tu? Angalau ukihesabu mwenyewe katika sensa utajua kwamba una minimize figure inflation na double counting.
Kwa nini tumuache Saidi adanganye ili kupika takwimu?
Saidi hadanganyi kwa sababu dini inayoulizwa hapa inaulizwa katika maudhui ya demographics, si katika maudhui ya faith.
Hiki ndicho kitu watu wengi -pamoja na Nyerere- ama wanashindwa kukielewa ama wanakitumia ku confuse watu.
Sensa ikiuliza dini haiulizi kwa minajili ya faith, kwa sababu ili kumjua mkristo kwa minajili ya imani inabidi umuulize kama anaamini "
Symbolum Apostolorum" sasa Wakristo wangapi wanajua hata kuisema yote, let alone kuitekeleza?
Hili swali ni la ki demographics zaidi.It's not actually about whether you are truly a Christian or Muslim, it is about if you get ill are you more likely to go to the missionary hospital because you know the doctors from church than the Agha Khan down the road?
Ya nini kubishania tarakimu za idadi? Ni kwamba hakuna kuhesabu dini. Wewe na dini yako kivyako na mungu wako. Kwisha habari yake.
You will be shortchanging yourself by not using this once a decade census exercise.
Ni kama una mashine ya kuvuna inayoweza kuvuna machungwa na matufaa kwa mpigo.
Wewe unavuna machungwa tu, unaacha matufaa kwa kuogopa kivuli chako mwenyewe. Matokeo yake unapohitaji idadi ya matufaa inakubidi ufanye kazi upya piecemeal.
Trust me katika public policy formulation serikali inevitably inajikuta inahitaji habari za dini, ila haiwezi kusema tu kwa sababu imezaliwa katika mizizi ya ukomunisti ambako dini pekee ni serikali.
Na hili jambo sisikii likizungumzwa kama inavyotakiwa.
Serikali licha ya kuogopa uamsho, inaogopa hata makanisa kwa sababu inajua the power of numbers na kwamba dini zikianza kujiangalia kama constituencies ku lobby - not necessarily in a negative way- for example good governance, serikali iatatafuta pa kutokea.
Serikali imesha control vyama vya siasa to an extent, trade unions etc, inaogopa dini.
Huu ndio ukweli wenyewe.