Mr. Right
Naomba tujudaliane kidogo labda tutaeleweshana; nimekusoma naona kuna kijichanganya kidogo; nimeona umesema wewe ni pro free market economy; mpaka hivi sasa tunapoongea free market economy ipo kwenye vitabu tu ni theory na utekelezaji wake ni mgumu naweza kukupa mfano mwaka huu Lockheed Martins walishinda tenda ya kutengeneza ndege za kujaza mafuta kwa matumizi ya jeshi la Marekani; ilionyesha dhahiri wao tenka zao ni bora na za gharama nafuu ukilinganisha Boeing; mara baada wizara ya ulinzi kuipa Lockheed tenda hiyo Bunge lilingilia kati na kuinyanga`nya Lockheed tenda kwa sababu za kuilinda Boeing kibiashara; ipo mifano mingi serikali ya Marekani imetoa tenda kwa makampuni kadhaa bila kuwepo kwa ushindani wa kibiashara, swali la msingi inakuwaje hapo kwenye free market pia kuna kulindana? Naamini umeshawahi kusikia vitu kama tarrifs, import quarters; hakuna hata nchi moja ya magharibi ambayo haina vitu hivyo je kwa nini wasiruhusu bidhaa zisitoke nchi moja hadi nyingine bila mikingamo? Ukweli hiyo free market wanaoyoihubiri sisi tuifuate wakati wao wenyewe wanaitekeleza kinadharia ; pia hakuna hata nchi moja ya kiafrika yenye uwezo wa kushindana na nchi za magharibi kwenye bidhaa za viwandani, wao walipolenga Afrika tuwe na free market lengo hasa ni kwa makampuni yao kuuza bidhaa zao Afrika.
Kwa nini Mwalimu Nyerere alikazania kilimo? Jibu ni rahisi wakati tunapata uhuru sekta viwanda ilikuwa duni kumbuka waingereza hawakuwa watawala walikuwa ni caretaker; waliwekeza zaidi kwenye makoloni yao kenye; Uganda na kwingineko ni kama vile unapopata jukumu la kumlea mototo wa jirani; mfano Kenya baada ya uhuru ilikuwa na miundo mbinu bora kuliko Tanganyika yote hayo si kuwa Mzee Jomo Kenyatta alifanya kazi ya ziada kuliko Mwl. Nyerere bali alirithi miundo mbinu bora.Kilimo ilikuwa ndio njia pekee ambayo ingeweza kutuokoa kiuchumi; na kutufanya tusiwe na tatizo la ajira; mpaka hivi sasa kilimo kinaajiri zaidi ya 60% za wakazi wa sub sahara Afrika; suala la vijiji vya ujamaa hilo labda nikueleweshe na nina uhakika Mkandara ama Mchambuzi waliligusia wengi walilipinga vijiji vya ujamaa lakini ukweli leo Tanzania imetengamaa kwenye kilimo kwa vijiji vya ujamaa ambavyo Mwalimu Nyerere alivianzisha kama vingekuwa vibaya basi wengi wangerejea kwenye utaratibu wao maisha kabla ya vijiji vya ujamaa.
Umekuwa ukisema eti Mwalimu Nyerere alifeli huo ni mtazamo wako nikiangalia nchi za sub Sahara Afrika Tanzania ya Mwalimu Nyerere ilikuwa bora zaidi ya nchi nyingi sijui kama umewahi kutembelea nchi za kiafrika na hapo ndipo utapoona matunda ya ile sera ya Mwalimu maendeleo mikoani; alijaribu kuhakikisha kila mkoa unakuwa na sera ya maendeleo. Lengo kuu la Mwalimu ilikuwa kuhakikisha tunakuwa ya wakulima na wafanyakazi. Mwalimua alipigwa vita sana na nchi za magharibi kwani alikuwa anahatarisha maslahi yao na hiyo ndiyo iliyopelekea kuhitilifiana na vyombo kama IMF na WB.
Kila mfumo una matatizo yake hata kwenye nchi zilizoendelea kuna matatizo ya mfumo wa kibepari si kila mtu anauafiki; je ni kwanini Taifa kubwa kama Marekani linapigania kuwepo kwa middle class? Kwa nini hawapiganii kila mtu awe milionea? Ama labda nikuulize nchi za kipebari kama Spain na Italy uchumi wao umeanguka kwa kiasi kikubwa ni kipengele gani kilichopo kwenye msahafu wa ubepari ambao hakikufuatwa?
Hili somo ni linahitaji fikra pevu ukirupuka Nyerere Nyerere hutatalielewa; ichukulie JF kama ni uwanja wa kuelemishana na si lazima tukubuliane katika kila jambo ila njoo na hoja.
Chama
Gongo la Mboto DSM
Chama,
Umecdhanganya mambo mengi sana. Umeanza na USA ukaenda mpaka Afrika, baadaye ukaenda mpaka Europe.
Anyway, issue ya market economy kuwa siyo perfect, hiyo kila mtu anajua. Lakini huwezi kuchukua protectionism zinazofanyika sasa hivi ktk kila nchi kublame market economy. Marekani ni nchi iliyofanikiwa sana duniani kwa muda mfupi kuliko nchi yoyote duniani. Marekani ina less than 235 years lakini maendeleo iliyopata ni makubwa sana. Na hiyo credit yote inapewa market economy.
Suala la protectionism. Sasa hivi nchi nyingi duniani zimeangia ktk mfumo huu bila ya kujua core principles za market economy na nchi nyengine zinaignore kwa makusudi, kama vile China. Ndiyo maana unakuta kuna mashindano au mabishano ktk import and export. Marekani walioengeza some tarrif ktk goods kutoka China, na China wakajibu kwa kuongeza import tarrif ktk goods zinazotoka USA. Hii issue ilitokea kwa sababu kuna some products ambazo zinapewa subsidize na government. Kwa hiyo USA waka argue kwamba hiyo ndiyo reason ya kuongeza hizo tarrif ktk Chinese goods. Kumbuka free market inataka market ndiyo idetermined who gets what.
To be honest, sasa hivi nchi nyingi ambazo zilikuwa ktk Ujamaa zimeingia ktk market economy, lakini bado serikali zao ndizo zinatumia hela nyingi ktk kampuni zao. Chukulia Emirates, serikali yao imeorder ndege Boeing nyingi sana, kupita hata mashirika makubwa ya ndege kama AA. Kwa hiyo issue hiyo, ya kuongeza tarrif or so called protectionism itaendendelea kuwepo as long serikali za nchi za former Ujamaa zitaendelea kucontrol hizo kampuni kubwa za biashara.
Unauliza kwa nini Marekani inapigania kuwa na middle class na siyo milionaire? Hiyo issue lazima iwepo ktk market economy. Lazima iwepo different class of citizen in order for market economy to survive. Ujamaa unapozungumzia fairness unamaanisha distribution of wealth. Kila raia awe ktk same level!! Hiyo ndiyo philosophy ya Ujamaa aliyokuwa anaipigania Nyerere. Anataka Ujamaa ili tule chakula kimoja, kuvaa nguo design moja, elimu moja.
Chukulia mfano, elimu iliyopo Marekani, kuna public school, state school, private school, na Ivy league school. Angalia ktk forum kama vile College Confidential demand ya watu wanaotaka kwenda ktk hizo Ivy league. Sasa kama ingekuwa same level usingeona bidiii ya wanafunzi ya kufanya ziada ktk masomo, community services, leadership skills ktk kujaribu kutaka kuingia ktk hizo shule za Ivy.
Ndiyo maana, nimesema Ujamaa umetufanya tuwe wategemezi. Kama tungekuwa na market economy tungekuwa mbali; kwa sababu kila mtu angetaka kufanya vizuri ili areach level fulani ya maisha. By the way, watu wengi wanakuwa millionaire in USA , ni bidii yako tu.