Hivi umeshawahi ona popote pale duniani kuliko kuwa na maendeleo bila ya political stability, bila ya kuangalia the mode of production. Kwetu Nyerere alifanya kazi kubwa sana kujenga hiki kitu, lakini lawama zinakuja thereafter hapo ndipo mnaposhindwa kuwa wakweli.
Yes he was intelligent hilo halina ubishi, but his long term visions are still open to scrutiny. Hata huyo Deng Xiaoping learned a lot from Mao Zedong, lakini halikubal ukweli wa muda wake hili taifa liendelee his masters ideology had to be scrapped completely na kupunguza hegemony media propaganda.
Kwetu bado ni tatizo kwa sababu a complete approach in socialism is bound to fail na hii ni kwenye mi-nchi ambayo inamisomi kibao, hila tu kwakuwa bado atuna tabia ya kuukubali kweli kwa kupenda kutumia biased propaganda and emotional attachments ndio bado tunabisha kitu ambacho kiko in the open (Mwalimu was a failure).
Amna raisi aliye-mfuata kuwa bora zaidi yake, lakini policies zake, mawazo yake and the style of his governance produced the rest of the failures we witness today (hawa viongozi ni by-product ya mwalimu tu, either luck of patriotism aliyowafundisha au kuja kuweka watu juu pending on loyalty or just may be he wasn't as strict as we are made to believe to everyone except to his enemies and a few examples, simple).
Juma, sijui kama umefuatilia mijadala mingi kwa undani. Kama umefuatilia mjadala wa Mohamed Said ungeelewa watu wanaongelea nini.
Nyerere kama kiongozi anaweza kujadiliwa kama kiongozi yoyote yule. Mazuri na mabaya yake yajadiliwe kwa uwazi. Mweka mada ameeleza kwanini kuna juhudi za kumchafua kama wachangiaji wengine wengi wanavyoona.
Hakuna anayemtetea Nyerere ya kuwa alikuwa malaika na alifanya mazuri. Huko Nyuma mimi binafsi nimewahi kueleza yale ambayo sikuridhishwa nayo wakati wa ezi zake.
Tofauti na wale wanaomchukia, mimi ninaweza kueleza kwanini sikukubaliana na sera zake. Sio lazima kila mtu akubaliane nami lakini basi hoja zinajieleza na mtu anaweza kupata nafasi ya kujibu kwa hoja zake, yaani wote tukalingania mada kwa uelewa.
Hawa wenye chuki ambazo zimejikita katika udini na mafunzo ya kukariri bila kutafakari ndio tunaojaribu kuwarudisha katika mstari.
Si kukubaliana na hoja zetu la hasha, ni kuwasaidia jinsi ya kujenga hoja na si kumeza hoja za Mohamed Said bila kujua anafanya biashara ya uandishi wa vitabu na ame target kundi analojua ni sehemu ya soko lake, lakini pia akiwa na frustration zake anazozijenga kama fustration ya taifa na hasa umma wa waislam.
Mfano ni Mr Right anaposema tungekuwa na free market economy tungekuwa mbali. Inaweza kuwa ana hoja na ndipo tuna muuliza Kenye, Uganda, Malawi, Zambia walikuwa hawana ujamaa. Kwa vile wao tuna mahusiano makubwa ya kijamii na kiutamaduni wamepiga hatua gani tunayoweza kusema si matokeo ya ujamaa. Pengine kwa kuona hoja hii itaua dhana ya chuki ndio maana nawe umekuja kuijibu kwa kiwango hicho ulichojaliwa.
Unaposikia mtu anasema Nyerere hakufanya lolote, wengine huwa tunahitaji kujua zaidi na ni hapo ndipo tunauliza ukilinganisha na marais 3 waliotawala miaka 25 na 24 ya Nyerere wamefanya nini kwa pamoja ambacho mwalimu hakukifanya?
Hapo ndipo tunasikia hakujenga bara bara ila Kikwete anajenga kwa kuweka lami ! jamani.
Tunauliza ni jambo gani ambalo linafanyika sasa hivi ambalo si msingi wa Nyerere, hakuna jibu! baada ya kukosa majibu wanarudi na kusema hafai, mbovu,mchawi badhirifu, mwizi n.k!
Lakini hao hao wasioweza kujibu maswali ndio mafundi wa kuhubiri Nyerere mbovu, hafai kuitwa baba wa taifa n.k.
Hivi unawezaje kusema Juma Contena ni mbovu kama huna hoja za kusaidia kauli yako. Je hapo si chuki.
Wengine tunahitaji msaada wa kujua wapi alikosea na kwanini na angefanya namna ipi mbadala. Je waliomfuata walifanya nini kukosoa makosa yake. Hakuna anayeweza kueleza. Tunarudi kule kule ni mtu mbaya sana.
Kundi hili limelishwa amini kuwa ukisema Nyerere ni mbaya basi unapata thawabu. Just say it even if you cannot back up with any evidence or any substantial and meaningful arguement!! Just open the mouth you will have lots of Thawab.
Imefika mahali watu wanadhani baba wa taifa ni biological father bila kujua ni language tu. kuna father of economy, father of genetics, father of the physics etc etc . Kama neno father halimfai Nyerere kama founder wa taifa basi hatuna sababu ya kumuitwa Mendelin father of genetic, au Newton kama father of 'physics'.
Najua wapo watakaokuja na hoja kuwa founder of the nation haina maana kwasababu nchi ilikuwepo. Sitashangaa kwasababu ni mwendelezo wa chuki dhidi ya mwalim hata kama wanakubali Mahtama Gandhi ni father of the India sub continent au founder of the Nation.
Nimalizie kwa kusema kila kinachosemwa au kuandikwa kiwe na mashiko. Kuleta hadithi za kusimuliwa gogo vivu ni kudhalilisha umma. Chuki ikitamalaki busara huhama na akili huvia. Ni ugonjwa mbaya sana.