Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
- Thread starter
- #701
1: Nimwemmbia factors zinazosababisha changing in price ni supply na demand. Yeye akaja na jibu kwamba West walitaka kununua bei ya chini. Nikampa jibu ni efficiency. West wanatumia advanced commercial agriculture with higher technology, halafu Nyerere na Ujamaa anataka kwenda kuuza mazao ya Ujamaa kwenye World Trade? hiyo ni joke ya Nyerere kwamba alishindwa kuelewa kuna competitive around the world especially from nchi za kutoka ktk free market zenye advanced tech. Hiyo ni failure ya kiongozi.
2: Ok wakoloni walitaka kwa "makusudi" tutumie jembe!! is that your rational thought? Blame wakoloni. By the way, Nyerere alichukua uamuzi kwa makusudi kwa njia ya kujaribu idea. Alifikiri yeye ni "Genius" Huwezi kuongoza nchi kwa kujaribu. Na Nyerere alifanya hivyo ili aonekane kama anaejali ya maslahi ya WTZ, lakini alishindwa kujua madhara yake.
3: Do you know what I know? Nyerere alichukua WTZ kwa nguvu na kuwapeleka vijijini kwa makusudi lil waanze kulima. Kuna ushahidi tosha ambao unaonesha jinsi WTZ walivyofanyiwa na kuhamishwa kwa nguvu na sera hizo za Nyerere. Sasa kama Nyerere alikuwa smart, kwa nini aliwapeleka WTZ vijijini bila ya misingi imara ya Kilimo kama vile maji nk?
4: Nyerere alikuwa na choice, alichagua wrong choice-Ujamaa. Sasa kwa nini tusiangalie benefit ambazo tungezipata kama tungechagua njia nyengine.
Unaweza kusema ni Scam. Unajua viongozi wote kama kina Nyerere alikuwa wanajifanya wanapinduzi lakini tabia waliyopata baada ya kuchukua nchi ilikuwa terrible kwa wale waliowachagua. Viongozi wa Ujamaa walikuwa wanapromote haki kwa wote, maisha bora nk. Lakini walipopata hayo madaraka walibadilika na kuwa Madictator wakubwa akiwemo Nyerere. Ndiyo maana nimesema ni scam. Wanapromise halafu wanabadilika.
Kuhusu suala la vijiji vya ujamaa, naomba ukasome kidogo dhana yake nzima, ili utofautishe intention za vijiji vile, utekelezaji, na mapungufu yake, then urudi tuvijadili vyote, otherwise kwa sasa hoja yako kuhusu Ujamaa inasukumwa na kuhadithiwa zaidi;
Kuhusu Nyerere kwamba alikuwa na choice after uhuru - the only choice he had ni kuendeleza muundo ule ule wa kikoloni ambao ulihakikisha Tanzania remains a rural backyard - 95% of tanzania ilikuwa ni vijiji; naomba usome kwenye historia mkoloni alifuata vitu gani Africa...na anatumua mbinu gani kuendelea kuvipata mwaka huu 2011; Otherwise kusema nyerere alikuwa na choice, ilikuwa ni either kuendeleza sera za mkoloni, au kulipa taifa a self determination - kwa mtazamo wako, alikuwa na choice gani?
Unaposema jembe la mkono - nyerere angefanya nini in 1961 alipopokea kilimo cha jembe la mkono? Angewanunulia wakulima wote matrekta? Otherwise alifanya mechanization, irrigation systems etc kwa uwezo wa wakati ule, na data zipo, au nikupe sasahivi kuhusu jinsi gani ali improve sekta ya kilimo ambayo aliipokea ikiwa ni ya jembe la mkono? Miaka ya late 60s to 1970s sekta ya kilimo ili experience tremendous growth, na ndicho kilichojenga viwanda, toa huduma za kijamii etc; hoja yako kuhusu jembe la mkono inapwaya, ipe mashiko zaidi ili tuwe ukurasa mmoja;
This is a quote from you to Mkandara, ipo hapo juu but naomba niiweke tena kwani ina mapungufu sana:
"Nimwemmbia factors zinazosababisha changing in price ni supply na demand. Yeye akaja na jibu kwamba West walitaka kununua bei ya chini. Nikampa jibu ni efficiency. West wanatumia advanced commercial agriculture with higher technology, halafu Nyerere na Ujamaa anataka kwenda kuuza mazao ya Ujamaa kwenye World Trade? hiyo ni joke ya Nyerere kwamba alishindwa kuelewa kuna competitive around the world especially from nchi za kutoka ktk free market zenye advanced tech. Hiyo ni failure ya kiongozi".
Unachokisema hapo juu hakileti maana yoyote, jaribu kukipanga zaidi; otherwise price isn't only determined by supply and demand, that's just the beginning of it;
Mpaka leo hii west wanataka kununua mazao yetu kwa bei ya chini, sijui kwanini unakuwa mzito kumuelewa mkandara - je wajua kwamba condition ya kwanza ya IMF kwa Nyerere in 1984 ili kutoa fedha kwa tanzania was kumlazimisha Mwalimu to devalue the shilling? do u know what devaluation means? it means, make your exports cheaper. Na madhara ya hiyo measure ndio we are paying the price na hela yetu ya madafu mpala leo; Unahitaji ufafanuzi zaidi juu ya hoja ya mkandara kuhusu wakubwa wa nje kulazimisha wanunue bidhaa zetu za mazao kwa bei ya chini? soma kuhusu devaluation and mazao ya kilimo then urudi tujadili;"
Hoja ifuatayo haina mashiko kabisa, nimekuwa naipuuza lakini unairudia ruda sana:
"West wanatumia advanced commercial agriculture with higher technology, halafu Nyerere na Ujamaa anataka kwenda kuuza mazao ya Ujamaa kwenye World Trade?"
Je, hapa una maana west walikuwa wanalima kahawa, mkonge, tumbaku, chai, pareto, na kushindana na sisi under ujamaa kuuza hizi bidhaa soko la dunia?
Ni dhahiri kwamba haujui kabisa unazungumza nini ndugu yangu, yani hata sijui nijibu vipi hii hoja; nina imani wengine watanisaidia;