Nyerere na ndoto kubwa ya Tanzania

Magufuli 05

JF-Expert Member
May 7, 2023
942
1,988
Mungu ibariki Tanzania🇹🇿

Julius Kambarage Nyerere.
1. Kiongozi aliyekuwa mzalendo wa kweli.

2. Kiongozi aliyewapenda Watanzania na kuwalilia siku zake za mwisho.

3. Kiongozi aliyekuwa na msimamo na mjamaa wa kweli.

4. Kiongozi aliyelinda raslimali za ndani kwa nguvu. Hakuwa na haraka ya kuingia mikataba ya dhuluma kwa nchi.

5. Kiongozi ambaye hakujilimbikizia mali na hakuta ufahari na mikogo.

6. Kiongozi aliyechukia ufisadi na RUSHWA na alikuwa mkali kweli.

7. Kiongozi aliyeamini katika utu,undugu na usawa.

8. Kiongozi aliyekuwa aliyeapa kulinda na kupigania mipaka ya Tanzania kwa jasho na damu.

9. Kiongozi aliyeamini katika kufanya kazi.

10. Kiongozi aliyeamini Urais kwake ni kazi ngumu, haipaswi kukimbiliwa kwani Ikulu ni mahali patakatifu na si pango la wezi.

11. Kiongozi aliye asisi VIWANDA vingi ikiwemo mwatex, mutex, sungura tex na urafiki.

12. Msomi na mwana mapinduzi wa kweli.

13. Aliyeshitakiwa na kufungwa akiipigania Tanzania.

14. Aliyekataa kuuza utu wake kwa RUSHWA,

15. Hadi anatoka ikulu hakuwa hata na majumba ya kifari nyumbani kwake, Hadi jeshi lilipoamua kumjengea kwa heshima yake.

16. Aliyekuwa na upeo mpana na akawa rafiki wa wenye upeo mpana kama akina Samora Machel, Mao TSE Tung, Kwame Nkrumah, Eduardo Mondlane, Kenneth Kaunda, Robert Mugabe, na akawa Leninist, Marxist wa kweli.

17. Kiongozi aliyeamini katika diplomasia ya win win.

Huyu ndiye Nyerere kwa ufupi Nina mengi ya kwake moyoni mwangu.

Tarehe 14.10.1999 alimaliza mwendo, lakini kazi aliifanya.

Lakini cha kushangaza alipong'atuka mwaka 1985 kama Rais wa nchi yetu, wakafuata warithi wake, Hawa wakawa wazalendo wa matumbo Yao.

Wakamkosoa sera zake, wakailangua nchi, wakajilimbikizia mali, wakaua VIWANDA, nchi ikawa lango la matapeli.

Hadi sasa nchi haina hata kiwanda cha kuyeyusha dhahabu, haina kiwanda cha kuzalisha nguo, haina hata kiwanda cha kutengeneza betri za magari wakati madini adhimu yapo.

Gesi ipo, dhahabu ipo, almasi ipo, rubi ipo, tanzanite ipo, bati ipo, nickel ipo, uranium ipo, cobalt ipo, mito, maziwa, BAHARI yapo, ulanga, chuma, helium, makaa ya mawe, Serengeti, Ngorongoro, Kilimanjaro, na vingine vingi vipo.

Nchi Bado ipo hivi kama unavyoona Mtanzania.
Nani alaumiwe?

Ni Mtanzania mwenyewe.

Kataa wahuni na matapeli,weka Tanzania mbele, hatujachelewa Sana,

Kataa viongozi wenye akili ndogo, wanao amini nchi haiwezi kwenda mbele bila kukopa Sana,

Kataa viongozi wanaodharau Watanzania wenzao.
Kataa viongozi wanaokupumbaza kwa vitu vidogo.

Jitambue sasa, 2025 angalia mtu, usiangalie chama.
Nyerere aliupiga mwingi.
Asnte baba wa taifa.🇹🇿
 
Wengine wanasema eti jiwe ndiye aliye anzisha ukabila, udini na undugu katika shughuli za serikali
 
Nyerere alikuwa ni kama mzazi ambaye yuko tayari familia ile ugali maharage lakini iwekeze kwenye mipango ya maendeleo ya muda mrefu itakayokwamua vizazi vyote kutoka katika umasikini.

Hawa wa sasa kila mtu anahofia 'legasi' yake, wako tayari kuzitoa rasilimali za nchi kwa bei ya kutupwa ili tu wapate fedha ya kutimiza matamanio yao ya muda mfupi.
 
Kuna member mmoja humu ni ama kwa kujua au uelewa mdogo wa mambo jana aliniuliza nyerere kafanya nn hapa nchini?

Huyu memba anajiita DIVISHEN FOO bilashaka ataiona hii itamsaidia sana.

Asante mkuu
 
Kosa la Mwalimu ni kuyachukia yote hata Yale mazuri ya wakoloni.

Alikua na nia nzuri akakosaa wenye mawazo sawa na yake
 
Hakuwa na ndoto kubwa
Angekuwa na ndoto angefanya yafuatayo

Angepangilia miji na majiji kwa miaka 100 ijayo.

Angekuwa na ndoto asingeweka Katiba ya Kifalme Falme

Angekuwa na Ndoto angewekeza kwenye Elimu bora

Angekuwa na ndoto angeilazimisha Zanzibar iwe Mkoa wa Tanganyika, au aiache ijitawale ka nchi, maamuzi yake yanaiumiza Tanzania

Kwa ufupi Nyerere ndo sababu ya Tanzania mbovu ya leo.

Yeye aliangalia Chama Chake badala ya Nchi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom