Mwalimu Nyerere amka uone

Magufuli 05

JF-Expert Member
May 7, 2023
942
1,988
Mungu ibariki Tanzania🇹🇿

Julius Kambarage Nyerere.

1. Kiongozi aliyekuwa mzalendo wa kweli.

2. Kiongozi aliyewapenda Watanzania na kuwalilia siku zake za mwisho.

3. Kiongozi aliyekuwa na msimamo na mjamaa wa kweli.

4. Kiongozi aliyelinda raslimali za ndani kwa nguvu. Hakuwa na haraka ya kuingia mikataba ya dhuluma kwa nchi.

5. Kiongozi ambaye hakujilimbikizia mali na hakuta ufahari na mikogo.

6. Kiongozi aliyechukia ufisadi na RUSHWA na alikuwa mkali kweli.

7. Kiongozi aliyeamini katika utu,undugu na usawa.

8. Kiongozi aliyeapa kulinda na kupigania mipaka ya Tanzania kwa jasho na damu.

9. Kiongozi aliyeamini katika kufanya kazi.

10. Kiongozi aliyeamini Urais kwake ni kazi ngumu, haipaswi kukimbiliwa kwani Ikulu ni mahali patakatifu na si pango la wezi. Aliamini wazalendo na wenye akili kubwa ndiyo waende pale. Leo hii hata mwenye akili ndogo,fisadi anaweza akaenda pale na akapigiwa makofi.

11. Kiongozi aliye asisi VIWANDA vingi ikiwemo mwatex, mutex, sungura tex na urafiki.

12. Msomi na mwana mapinduzi wa kweli. Aliyeheshimika Duniani kote.Nenda Ethiopia,Namibia,Afrika kusini,Zimbabwe, Uganda,China,India na kwingineko utakuta majumba na Mitaa yenye jina lake.

13. Aliyeshitakiwa na kufungwa akiipigania Tanzania. Akafanya uamuzi wa Busara pale Tabora.

14. Aliyekataa kuuza utu wake kwa RUSHWA,

15. Hadi anatoka ikulu hakuwa hata na majumba ya kifari nyumbani kwake, Hadi jeshi lilipoamua kumjengea kwa heshima yake.

16. Aliyekuwa na upeo mpana na akawa rafiki wa wenye upeo mpana kama akina Samora Machel, Mao TSE Tung, Kwame Nkrumah, Eduardo Mondlane, Kenneth Kaunda, Robert Mugabe,Nelson Mandela,Fidel Castro na akawa Leninist, Marxist wa kweli.

17. Kiongozi aliyeamini katika diplomasia ya win win.

Huyu ndiye Nyerere kwa ufupi Nina mengi ya kwake moyoni mwangu.

Tarehe 14.10.1999 alimaliza mwendo, lakini kazi aliifanya.

Lakini cha kushangaza alipong'atuka mwaka 1985 kama Rais wa nchi yetu, wakafuata warithi wake, Hawa wakawa wazalendo wa matumbo Yao.

Wakamkosoa sera zake, wakailangua nchi, wakajilimbikizia mali, wakaua VIWANDA vya nyama,mkonge,mafuta,mbao n.k nchi ikawa lango la matapeli.
Na hata wakaona wao Wana akili kuliko hata aliyelala vichakani,aliyesafiri ng'ambo kufuata uhuru.

Hadi sasa nchi haina hata kiwanda cha kuyeyusha dhahabu, haina kiwanda cha kuzalisha nguo, haina hata kiwanda cha kutengeneza betri za magari wakati madini adhimu yapo tumeishia kuwapa wa Australia.

Gesi ipo, dhahabu ipo, almasi ipo, rubi ipo, tanzanite ipo, bati ipo, nickel ipo, uranium ipo, cobalt ipo, mito, maziwa, BAHARI yapo, ulanga, chuma, helium, makaa ya mawe, Serengeti, Ngorongoro, Kilimanjaro, na vingine vingi vipo.
Raslimali zinasombwa,tunaachiwa mashimo.

Nchi Bado ipo hivi kama unavyoona Mtanzania.
Nani alaumiwe?

Ni Mtanzania mwenyewe.

Kataa wahuni na matapeli,weka Tanzania mbele, hatujachelewa Sana,

Kataa viongozi wenye akili ndogo, wanao amini nchi haiwezi kwenda mbele bila kukopa Sana,

Kataa viongozi wanaodharau Watanzania wenzao.
Kataa viongozi wanaokupumbaza kwa vitu vidogo.

Jitambue sasa, 2025 angalia mtu, usiangalie chama.
Nyerere aliupiga mwingi.
Asnte baba wa taifa.🇹🇿
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom