Nyerere! Huyu mzee kiboko!

Nchi ikiwa corrupt itaabudu wenye mali. Ndivyo RA, EL, JK, Chenge et al na genge lao la wezi wanavyoitafuna pesa ya walipa kodi.
 
Ukisikiliza hii speech utajua kwanini watu wa uganda wanataka kumfanya huyu mtu awe mtakatifu...any way hii ni imani yao.

Mie ningependekeza kabla ya vikao vya baraza la mawaziri, bunge na vyama vya siasa, wawe wanaweka speech kama hii baada ya dua, na kabla ya kuanza mijadala yao.
Hii italeta discipline,focus,transparency, hata kuwaondoa watu walioitia mfukoni serikali ya JK (RA na wenzake).
Katika CCM ya leo hakuna mtu angependa kumsikiliza Nyerere. Wangefurahi zaidi kama angesahaulika katika fikra za Watanzania kama walivyomsahau katika fikra zao.
 
Kuna ile aliyosemaga ati kiongozi bora kwa mtazamo wake ni yule ambaye ataichukua nchi na kuielekeza katika mema kwa faida ya wananchi ila cha muhimu asisahau kurithi mazuri yaliyofanwa ktk awamu zilizopita ila mabaya yawe abandoned ili kuepuka kurudi kule tupilokuwa.

Sasa nikiangalia hivi leo naona wazi kwamba tumerudi kulekule tena tukifanya masihala tutapitiliza na tutajikuta hata mabarabara yetu yote yapo owned na mafisadi ( private owned)
 
Huyu mzee angelikuwa hai 2005 piga ua Rais angekuwa ni SAS.Sijui Mkapa angejibinafsishia kiwira?
 
Nimeshindwa kujizuiz leo baada ya kuiona hii ya Hayati JK wa ukweli alipoongea 1995!, Tumekwishaaaaaaa!

Dah! Hotuba aliitoa miaka 16 iliyopita lakini utadhani kama kaitoa leo kuhusiana na uongozi mbovu sana ndani ya Serikali ya kifisadi na Chama Cha Mafisadi/Majambazi. Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi~AMEN
 
Last edited by a moderator:
Nyerere kilikuwa kifaa kingine,alikuwa akiishi keshokutwa leo.Nd'o maana alikuwa ameona pia haiwezekani kilaza kama jk apewe nchi yeye anaangalia tu,lakini pia alitokota kwa kutomuachia mrema awatie adabu hawa.Vinginevyo asilimia kubwa ya mawazo yake nayakubali.
 
Katika CCM ya leo hakuna mtu angependa kumsikiliza Nyerere. Wangefurahi zaidi kama angesahaulika katika fikra za Watanzania kama walivyomsahau katika fikra zao.
Nakubaliana na wewe jasusi,na kwa namna wanvyomchukulia,mtu yoyote atakuwa sahihi kuamini kuwa huyu nyerere aliuwawa.
 
LoyalTZ...
Uzoefu unaonyesha kuwa wengi wala rushwa ni wanaume, ndo maana mwl akapelekea kusema hiyo sentensi ya kwenda kumuonyesha mke wake.....:)

Hapo red si kweli, kwa sasa ni wazi kuwa rushwa haina jinsia, unajua zamani wanawake walikuwa sio wengi madarakani hivyo ilikuwa si rahisi kujua uovu wao, ila kwa sasa mifano ni mingi ya wanawake corrupt. Nigeria kule waliopelekea msukosuko wa mabenki ni wanawake kwani hapo kabla waliaminiwa kuwa safi. Kwa Tanzania mifano kila mtu anaijua. Hivyo ukipima kwa ratio utagundua kuwa ngoma ni droo.
 
Wacha aliyoyasema sasa yanawatokea puani.
Aliwaeleza kila kitu kinagaubaga, hakuficha chochote ,kwani alijua hayo yatatokea baaadaye
 
Hivi mnayajuwa ya Nyerere au mnasikiliza porojo zake za kwenye vibaraza vya kuchezea bao?

Hana jema aliloifanyia hii nchi. Lipi moja?

Hajaacha misingi imara ya kuendesha hii nchi kama aliacha ni ipi?

Hata katiba alizokuwa akiandika Ikulu na mawakili wake wabovu leo kila mTanzania hazitaki.

Hebu mmoja tu, anambie kitu kimoja kizuri alichofanya Nyerere zaidi ya kuongea sana na wanafiki kucheka hata pasipo chekesha.

Angekuwa na mawazo na fikra nzuri japo chembe, leo Tanzania na utajiri ilionao ingekuwa kwenye neema ya ajabu.
 
Nakubaliana na wewe jasusi,na kwa namna wanvyomchukulia,mtu yoyote atakuwa sahihi kuamini kuwa huyu nyerere aliuwawa.

Exactly! hivi jamani huyu mzee aliugua muda gani? na haswa kilichomuua ni nini?? maana kila mtu anasema chake. Ukiangalia kwa makini ktk hizi videos anaonekana yuko fit to the extent, anasema kwa sauti, physical na wala haonekani kama anastruggle healthwise. Kwa sababu hii imenifanya ku employ doubts kuwa kuna kitu huenda kilifanyika! Mungu atusamehe.
 
Hivi mnayajuwa ya Nyerere au mnasikiliza porojo zake za kwenye vibaraza vya kuchezea bao?

Hana jema aliloifanyia hii nchi. Lipi moja?

Hajaacha misingi imara ya kuendesha hii nchi kama aliacha ni ipi?

Hata katiba alizokuwa akiandika Ikulu na mawakili wake wabovu leo kila mTanzania hazitaki.

Hebu mmoja tu, anambie kitu kimoja kizuri alichofanya Nyerere zaidi ya kuongea sana na wanafiki kucheka hata pasipo chekesha.

Angekuwa na mawazo na fikra nzuri japo chembe, leo Tanzania na utajiri ilionao ingekuwa kwenye neema ya ajabu.

kila mtu anauelewa tofauti hapa duniani. hakuna afananae na mwenzie kamwe. japo hayo mawazo tofauti hayawezi kuwa yote yako sahihi. haya ya kwako wewe ndo yale yasiyo sahihi. wakati nchi inapata uhuru babu yako wewe nikujuavyo alikuwa masikini wa kutupwa na hata babayo asingesoma hilo darasa lake la nne bure lililomfanya awe na uelewa na akupeleke shule wewe. leo hii alhamdulilah unaweza japo ku type kwa kudonoa na unaweza kuvaa tai umeshasahau. watu wengine hamna hata aibu. najua una lengo lako tofauti na unalificha. weka wazi kama wenzio wasiojificha na idea zao za kizembe. alikandamiza.... huo ni uongo na upuuzi. the problem of u guyz wants to be treated special. huo utajiri si ndio mmautafuna na ndugu zako bila uchungt sasa? duh!
 
Exactly! hivi jamani huyu mzee aliugua muda gani? na haswa kilichomuua ni nini?? maana kila mtu anasema chake. Ukiangalia kwa makini ktk hizi videos anaonekana yuko fit to the extent, anasema kwa sauti, physical na wala haonekani kama anastruggle healthwise. Kwa sababu hii imenifanya ku employ doubts kuwa kuna kitu huenda kilifanyika! Mungu atusamehe.

Mnasahau kuwa "tumetoka kwa udongo, tutarudi kwa udongo"?

Nyerere kafa kwa Ukosefu wa Kinga Mwilini kwa kuwa na kansa ya damu. Na kafia hospital Uingereza.

Na kama hilo gonjwa lilimuua lilikuwa la kuuawa na binadamu mwingine, basi huyo binadamu inafaa apongezwe sana. Kwani Nyerere alishauwa wengi tu kwa ama makusudi ama maamuzi mabovu aliyokuwa akishinikiza.

Wanojidai kumpenda Nyerere hawakuwepo wakati wake na wala hawana fikra za kufikiri kwa kujiuliza hivi, Nyerere ni kipi chema alichokifanya? Hakuna.
 
Mnasahau kuwa "tumetoka kwa udongo, tutarudi kwa udongo"?

Nyerere kafa kwa Ukosefu wa Kinga Mwilini kwa kuwa na kansa ya damu. Na kafia hospital Uingereza.

Na kama hilo gonjwa lilimuua lilikuwa la kuuawa na binadamu mwingine, basi huyo binadamu inafaa apongezwe sana. Kwani Nyerere alishauwa wengi tu kwa ama makusudi ama maamuzi mabovu aliyokuwa akishikiza.

Mkuu! sidhani kama aliua kama JK anavyoua sasa hivi kwa muda huu mfupi aliokaa madarakani ni mudamfupi sana ukilinganisha na Mwalimu na haya mabomu na ufisadi unapelekea catastrophic deaths kwa raia wasio na hatia!, nchi imekosa uadilifu kuanzia ktk afya, ustawi wa jamii mpaka usalama wa raia. Ni maisha ya mashakamashaka tu. Kuua imekuwa ni legal kwani wenye power wanaua tu! kuongozi au mkewe au mtoto wake anaweza ua raia na raisi anachekacheka tu hakuna hatua atakayoichukua! yaani nchi ipo shaghalabaghala!
 
I do not see anything in this posting! Is it my problem???

Angalia hapo juu kwenye tool bar, kuna maandishi madogo ebu ya CLICK na baada ya hapo yatakupa Options na mojawapo ni Run Add on
Click hapo na utakuwa sawa.
Ubarikiwe!
 
Hiyo thread ingekuwa inakaa mwanzo kabisa mtu akifungua jamii kila siku anakutana nayo asianze kuisaka. Naona itakuwa nzuri sana hasa kwa akina ss ambao hatuna hotuba za baba.
 
Hiyo thread ingekuwa inakaa mwanzo kabisa mtu akifungua jamii kila siku anakutana nayo asianze kuisaka. Naona itakuwa nzuri sana hasa kwa akina ss ambao hatuna hotuba za baba.

Au ingekuwa kama inatumika ktk induction kwa kila mbunge wakati anaapishwa! ili kurefresh maadili!
 
Mnasahau kuwa "tumetoka kwa udongo, tutarudi kwa udongo"?

Nyerere kafa kwa Ukosefu wa Kinga Mwilini kwa kuwa na kansa ya damu. Na kafia hospital Uingereza.

Na kama hilo gonjwa lilimuua lilikuwa la kuuawa na binadamu mwingine, basi huyo binadamu inafaa apongezwe sana. Kwani Nyerere alishauwa wengi tu kwa ama makusudi ama maamuzi mabovu aliyokuwa akishinikiza.

Wanojidai kumpenda Nyerere hawakuwepo wakati wake na wala hawana fikra za kufikiri kwa kujiuliza hivi, Nyerere ni kipi chema alichokifanya? Hakuna.

Majimshindo uko sahihi, na mimi nakubaliana na wewe. Wewe si mnafiki kama wengine kwasababu unasema unayoyafahamu na kuyaamini. Lakini, si lazima yawe ukweli wote (absolute truth). Haiwezekani kuwafanya watu wote kumtazama Nyerere kama kiongozi mzuri sana au mbaya sana.

Hata kwenye dini ni hivyo. Kuna watu wanasema Yesu ni Mwana wa Mungu, wengine wanasema ni Nabii tu. Wengine wanasema Mtume Mohamme (s.a.w) ni Nabii wa Mwisho wa Mungu, na wengine wanasema ni Nabii wa Uongo... mlolongo ni mrefu. Je ni nani yuko sahihi zaidi?

Kuna mambo mengi magumu, yatamngoja Mwenyezi Mungu kuja kuyatolea hukumu ya haki. Hapo hakutakuwa na ubishi. Sasa hivi tutaumiza vichwa bure tu.

Mimi kama mimi, namtazama Nyerere, kama kiongozi mmoja mwenye hekima ambazo hazimithiliki, na hafanani na viongozi wengi wa duniani na hususani wa-Tz. Siwezi kumlinganisha Mzee AH Mwinyi, Mzee BW Mkapa ama Mzee JM Kikwete na Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere.

Angalia yafuatayo
  1. Aliachia madaraka ya rais wakati watu na katiba vinaruhusu kuendelea kutawala
  2. Alirudi kijijini kwao kulima kwa jembe la mkono na kukokotwa na ng'ombe. Hakuna duniani kiongozi wa namna hiyo labda Uchina ya zamani
  3. Alijitoa kuelimisha watu wake bure ili wapate kujitambua na kujilinda dhidi ya mafisadi na mabeberu kutoka ndani na nje
  4. Aliwapa watu wake huduma ya afya bure, ili waweze kuwa na afya waijenge nchi yao
  5. Aliwakusanya watu wake ktk vijiji ili apate kuwahudumia kwa urahisi zaidi
  6. Alitaifisha shule za mission ili wanchi wake wa dini zingine kama waislam (ambao si dini yake) nao wapate kusoma, kuelimika ili wapate toa mchango wa kuijenga nchi yao
  7. Alilazimisha chama chake kuanzisha vyama vingi ili kusaidia nchi iende na wakati na pia kuweka mfumo wa checks and balance (ambao sasa unafanya kazi kama alivyotegemea)
  8. Alijitolea kusaidia mataifa jirani yaliyokuwa hayapata uhuru yaweze kujikomboa.
  9. Alizuia maliasili zetu ziendelee kubaki salama hadi hapo tutakapopata utambuzi wa kutosha kuzisimamia ili ziweze kunufaisha uchumi na maisha yetu. Hapo alikataa kuwa kama Mobutu Seseko aliyejilimbikizia mali na wananchi wake wakawa masikini
  10. Alikataa kuwa na mahusiano na Israel waliokuwa wakwaonea wananchi Wapalestina
  11. Alipingana hata na Wajerumani, Waingereza waziwazi pale walipokuwa na misimamo ya ubaguzi au uonevu kwa binadamu wengine.
  12. Alikuwa hana unafiki, na alikuwa yupo tayari kukemea hata taifa kubwa la America lilipochukua msimamo wa kukandamiza mataifa madogo na masikini kwa sababu za kimabavu tu.
  13. .... orodha ni ndefu sana
Nyerere, alikuwa binadamu, anayo makosa. Lakini alikuwa akisema tujisahihishe...Alipoondoka madarakani alisema tuyaache mabaya yake lakini mazuri tusiyatupe. Hata alikubali tuache Ujamaa lakini tubaki na Kujitegemea.. Bahati mbaya viongozi wetu wameshindwa kujifunza kutoka kwake. Wanataka kuwasikiliza mafisadi zaidi ya wananchi wao masikini. Hiyo ndio shida iliyopo
 
Back
Top Bottom