Majimshindo uko sahihi, na mimi nakubaliana na wewe. Wewe si mnafiki kama wengine kwasababu unasema unayoyafahamu na kuyaamini. Lakini, si lazima yawe ukweli wote (absolute truth). Haiwezekani kuwafanya watu wote kumtazama Nyerere kama kiongozi mzuri sana au mbaya sana.
Hata kwenye dini ni hivyo. Kuna watu wanasema Yesu ni Mwana wa Mungu, wengine wanasema ni Nabii tu. Wengine wanasema Mtume Mohamme (s.a.w) ni Nabii wa Mwisho wa Mungu, na wengine wanasema ni Nabii wa Uongo... mlolongo ni mrefu. Je ni nani yuko sahihi zaidi?
Kuna mambo mengi magumu, yatamngoja Mwenyezi Mungu kuja kuyatolea hukumu ya haki. Hapo hakutakuwa na ubishi. Sasa hivi tutaumiza vichwa bure tu.
Mimi kama mimi, namtazama Nyerere, kama kiongozi mmoja mwenye hekima ambazo hazimithiliki, na hafanani na viongozi wengi wa duniani na hususani wa-Tz. Siwezi kumlinganisha Mzee AH Mwinyi, Mzee BW Mkapa ama Mzee JM Kikwete na Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere.
Angalia yafuatayo
- Aliachia madaraka ya rais wakati watu na katiba vinaruhusu kuendelea kutawala
- Alirudi kijijini kwao kulima kwa jembe la mkono na kukokotwa na ng'ombe. Hakuna duniani kiongozi wa namna hiyo labda Uchina ya zamani
- Alijitoa kuelimisha watu wake bure ili wapate kujitambua na kujilinda dhidi ya mafisadi na mabeberu kutoka ndani na nje
- Aliwapa watu wake huduma ya afya bure, ili waweze kuwa na afya waijenge nchi yao
- Aliwakusanya watu wake ktk vijiji ili apate kuwahudumia kwa urahisi zaidi
- Alitaifisha shule za mission ili wanchi wake wa dini zingine kama waislam (ambao si dini yake) nao wapate kusoma, kuelimika ili wapate toa mchango wa kuijenga nchi yao
- Alilazimisha chama chake kuanzisha vyama vingi ili kusaidia nchi iende na wakati na pia kuweka mfumo wa checks and balance (ambao sasa unafanya kazi kama alivyotegemea)
- Alijitolea kusaidia mataifa jirani yaliyokuwa hayapata uhuru yaweze kujikomboa.
- Alizuia maliasili zetu ziendelee kubaki salama hadi hapo tutakapopata utambuzi wa kutosha kuzisimamia ili ziweze kunufaisha uchumi na maisha yetu. Hapo alikataa kuwa kama Mobutu Seseko aliyejilimbikizia mali na wananchi wake wakawa masikini
- Alikataa kuwa na mahusiano na Israel waliokuwa wakwaonea wananchi Wapalestina
- Alipingana hata na Wajerumani, Waingereza waziwazi pale walipokuwa na misimamo ya ubaguzi au uonevu kwa binadamu wengine.
- Alikuwa hana unafiki, na alikuwa yupo tayari kukemea hata taifa kubwa la America lilipochukua msimamo wa kukandamiza mataifa madogo na masikini kwa sababu za kimabavu tu.
- .... orodha ni ndefu sana
Nyerere, alikuwa binadamu, anayo makosa. Lakini alikuwa akisema tujisahihishe...Alipoondoka madarakani alisema tuyaache mabaya yake lakini mazuri tusiyatupe. Hata alikubali tuache Ujamaa lakini tubaki na Kujitegemea.. Bahati mbaya viongozi wetu wameshindwa kujifunza kutoka kwake. Wanataka kuwasikiliza mafisadi zaidi ya wananchi wao masikini. Hiyo ndio shida iliyopo