Nyerere hakuwahi kupata tunzo ya Nobel

Hakuna swala la imani hapo, kuna suala la elimu. Kuna mtu alilisemea hilo kwenye post#93 ndio akawa anajibiwa ilikoanzia "Ilm dunia". Soma vizuri posts na usiogope utajuwa kuwa suala si imani ni elimu.
basi ndugu punguza pia na mahudhurio na kubandika kule bondeni maana integrity nayo inapungua. Mwisho wa siku mada inanajisika
 
Baada ya kuwapa darsa kidoogo kuhusu hayo hapo juu, napenda kuwafahamisha kuwa nyerere si tuu hakupata tuzo ya Nobel wala Noble, bali hajawahi hata kuwa "nominated" kupata hizo tuzo. Huo ndio ukweli.

Hahahaaa umenichekesha sana kwa uelewa wako mdogo, kwa kukujuza tu kuhusu madrasa:

Islam has, from its inception, placed a high premium on education and has enjoyed a long and rich intellectual tradition. Knowledge ('ilm) occupies a significant position within Islam, as evidenced by the more than 800 references to it in Islam's most revered book, the Koran. The importance of education is repeatedly emphasized in the Koran with frequent injunctions, such as "God will exalt those of you who believe and those who have knowledge to high degrees" (58:11), "O my Lord! Increase me in knowledge" (20:114), and "As God has taught him, so let him write" (2:282). Such verses provide a forceful stimulus for the Islamic community to strive for education and learning.

"darasa" au "madrasah"? Acha kuhadaa watu bana! Wewe ndiyo mchakachuaji, tena aliyekubuhu. Hujui hata tofauti kati ya "noble", "Nobel" - with capital N please, na "nobility". Aibu!!
 
When I was younger I thought this man was useless and a real socialist. However looking back today I feel and I know that he was a very honest person. If he had the support of Western Countries, Tanzania would have been very far today. He was the only honest leader we ever had. He didn't take any nonsense from the Western Countries unlike the present leaders. He deserves a lot of merit. GREAT MAN !!!
 
current leaders have a very close connection with the west, east, north and south yet the country is a leading begger
 
You can alike it to DR SLAA, the NEC did not announce him the winner of the 2010 Presidential General election but most of the Tanzanians believe that He won it.

The majority of the people who have ever been interested with the Politics and governance in the third world countries believe that Mwalimu deserved the honor.

It is not surprising to see the world being so unjust to this hero of African and world oppressed. Nyerere opposed any type of exploitation and oppression and feared not the powerful and mighty nations. He used to say that it was better to live free in freedom than to live as a slave in riches. He proved incorruptible when he was seduced to accept offers to open secret bank accounts abroad and ashamed them by putting their deals public. Through his stance of speaking for the poor and oppressed he made enemies world wide and became subject of mudslinging western propaganda. He had guts to rebuke powerful western countries when there was need to do so. For example he dared rebuke the Queen of England when he sensed betrayal to the accord he and Dr. Kaunda brokered to end the Zimbabwe war. In that accord it was agreed the freedom fighters to return to Zimbabwe (Then Southern Rhodesia), surrender their weapons and be put to camps. Nyerere became vociferous to tell the queen to stop political prostitution when he and Kaunda realized that the Ian Smith Army was encircling the fighters for the purpose of annihilating them. The response from the British government was to stop that heinous act by the Smith army and the program went thereafter smoothly until succession of power to ZANU. In fact Nyerere achieved more than any of the Africans who received the so called Nobel Price only that he was a victim of his stubbornness of not bending to western pressures. All in all Nyerere is the exemplar par excellence and should be a model to our current African leaders. RIP our father of Nation.
 
"To be Noble" si lazima uwe na mlolongo wa mambo uliyoyafanya, moja tu linatosha kukufanya uwe "noble" na upate tuzo hiyo. Nyerere hana hata hilo moja na wala hawajakosea:

Obama: Kuukwaa uRais tu wa Merekani kumetosha kumpatia hiyo tuzo.

Mandela: Kusamehe

De Klerk: Kumwachia Mandela

Kissinger: Kusaidia kuondowa "cold war" na mihangaiko ya kuwatafutia amani wayahudi.

And so on and so forth.

Nyerere: Nil

Angojee utakatifu kwa kusaidia mfumo kiristo Tanzania, hana zaidi.

Kumbe mnamhukumu kwa jicho la udini alioupandikiza Kikwete? Kama ni hivyo hata mwelezwe vipi hamtaelewa. Faizafox unajinadi eti ulikuwepo enzi zile za Nyerere, kumbuka si wewe pekee tu hata sisi tulikuwepo na tulikuwa active hata kabla ya Tanganyika kujitawala. Inasikitisha, na ni ushetani tu kutumia nyumba za ibada kupandikiza chuki dhidi ya mtu aliyejitoa kwa hali na mali kwa ajili ya taifa lake na hususan kwa ajili ya wanyonge. Unapotosha kusema Nyerere aliwatupa watu porini wakaliwa na simba, je ilikuwa sera rasmi ya kuwatupa watu waliwe au ilitokea kwa bahati mbaya na kutokana na uzembe wa waendaji? Ni watu wangapi basi (kama ilikuwa sera) waliouwawa namna hiyo? Lengo lilikuwa nini basi? Mbona hamsemi nia njema ya kuwahamisha watu na kuwaweka pamoja ili kurahisisha upatikanaji wa hudumamuhimu na badala yake mnapandikiza chuki tu? Hayo ndiyo mafundisho ya Mungu kweli? Kwa nini msiseme basi kwamba lengo la kuwakusanya wananchi katika vijiji pamoja kama ni kurahisisha upatikanaji wa huduma kama za shule, zahanati, utaalamu wa kilimo n.k.? Kama wewe kweli uliziishi enzi kabla ya Uhuru sema ukweli; watu walikuwa wakiishi tunavyoishi sasa? Hapana. Ukweli ni kwamba watu tulisambaa na mahali pengine ungeweza safiri hadi kilometa kadhaa kabla ya kukuta familia moja au mbili, je wangepelekewaje huduma hizo watu hao? Kwani enzi hizo hawakuwepo waislamu hadi muwasemee sasa? Au nyinyi ni waislamu bora na werevu zaidi ya wale waliokuwepo nyakati zile?
Mnasambaza uongo wa kusema ati Nyerere aliugandamiza uislamu; mnasema kweli nyinyi mbele ya Mungu? Mbona hamsemi jinsi Nyerere huyohuyo alivyolisababishia dhehebu lake hasara kubwa kwa kutaifisha shule zao karibu zote bila fidia kwa lengo la kuwawezesha wananchi wote kupata fursa sawa katika upatikanaji wa elimu. Je shule alizotaifisha kama zingekuwa zetu waislamu pangetosha hapa leo? Ni lazima kumbukumbu ziwekwe sawa kwamba asilimia kubwa ya shule zilizokuwepo zilikuwa za Kikristo idadi kubwa zikiwa za Kikatoliki.
Ni ushetani, na narudia tena kwamba ni ushetani mkubwa kuhangaika na kupandikiza chuki kwa vijana wasioijua vema historia ya tulikotoka ili kuleta mitafaruku ya kiimani isiyo lazima. Uongo, fitna, uchonganishi na chuki si kazi ya Mungu, bali shetani.Je mnatumiwa na shetani nyie?
 
mkuu nashukuru kwa kusema ukweli kama angekuwa mdini asingetaifisha shule za wakristo angeziacha mikononi mwao
 
Nimesoma wasifu wa viongozi wote walopewa hiyo tuzo ya Nobel, mimi sioni kama nyerere anastahiki. Kwa sababu wote walopewa ukiona wasifu wao ni watu walotetea mazuri katika nchi zao NA SIO NJE YA NCHI ZAO!

Nyerere kipi kikubwa alikifanya hapa Tanganyika enzi hizo mpaka ikawa TAnzania apewe hiyo Tuzo! hebu naomba uniorodheshee nini alikifanya kwa nchi yake na wananchi wake wa TAnganyika na baadae TAnzania mpaka leo atunukiwe TUNU hiyo adhimu!

Nyerere alianzisha azimio la arusha na kutaifisha mali za wananchi wake na kuwaacha masikini na kusababisha uchumi wa nchi KUPOROMOKA!,
Akaona hiyo haitoshi akawalazimisha watu kuanzisha vijiji vya ujamaa kwa nguvu na kuwatoa watu katika makazi yao nakuwapeleka sehemu ambazo zilikuwa mapori na kusababisha wengine kuliwa na simba na kugongwa na nyoka wenye sumu kali na kuwaacha wanawake wakiwa wajane na watoto wakiwa yatima.
Upande wa Zanzibar (Ungaja na PEmba) akawaingiza katika muungano ambao unaonekana kabisa ni hauna tija kwa wa TAnganyika na wazanzibar na kuwaacha watu wakilalama mpaka leo !
Akaona haitoshi , akaingia katika vita isiyo yake kwa sababu tu ya kumsaidia swahiba wake Obote na kusababaisha UMASIKINI WA HALI YA JUU kwa nchi na wananchi wake kwa ujumla.

Watu walikuwa wanakula NJANO unga wa kulisha farasi kule marekani ambao sasa hivi ndio angalau una heshima! jamani

Mtu kwanza unaze na nyumbani kwako halafu ndio uende nje ! sasa kipi kikubwa babu nyerere alikifanya mpaka apate hiyo Nobel award! USINCHEKESHE FaizaFoxy anasema !
 
quote_icon.png
By Kiranga Tenda wema wende zako, usingoje shukurani. Hizi tuzo zenyewe miyayusho tu.

And Nyerere is not all that, kafanya nini cha ajabu katika world stage?

Mzee hili swali lingeulizwa kwa Obama vile vile alipopata Nobel Peace Prize alikuwa amefanya nini? Kwani Wathari naye amefanya nini kwenye world stage? Mandela na De Clerk walifanya nini kwenye world stage?

Yeye anakuuliza wewe, kuwa ana kipi alichokifanya huyo nyerere mpaka apewe hiyo award! watanzania bwana , unaulizwa swali badala ya kujibu na wewe unauliza swali ... jibu "ORODHESHA" nini kakifanya nyerere mpaka astahili kupata hiyo award ?
 
Mimi ni kati ya watu ambao siyo mshabiki sana wa Nyerere. Nilianza shule wakti Tanzania ndiyo mwanzo imepata uhuru. Maisha ya Tanganyika/Tanzania kwa kweli yalikuwa duni sana. Wakati Tanganyika tunapata uhuru hali yetu ya kiuchumi haikuwa tofauti sana na ile nchi za South East Asia – Malaysia, Singapaore, Thailand, etc. Leo tumeachwa mbali sana.
Nyerere alikuwa na tatizo kubwa na kudhani kuwa wengine hawajui kitu. Kila kitu anajua yeye na ukimbishia basi wewe ni adui yake wa maisha. Hawezi kukusamehe kabisa. Hakuwa mtu anayependa kuonea watu lakini alipenda sana kulipiza kisasi. Mifano ipo mingi. Akina Tuntemeke Sanga ambaye aliambiwa asitembee nje ya wilaya ya Njombe, Oscar Kambona alimpa baba yake (an Anglican Pastor) gari la Landrover. Oscar alipokimbilia UK yule mzee aliambiwa lile gari lisitembee hata nchi moja. Liliozea lilopoegeshwa.
Katika Africa yeye alijipatia sifa nyingi katika kuongoza vita za kulikomboa bara hili. Wazungu wengi hawakupenda siasa yake ya ujamaa wakidhani kuwa itaenea bara zima. Lakini katika Afrika Nyerere vilevile aliwahi kufanya vitendo ambavyo alikuja kuvijutia baadaye kama kuunga mkono kwa kujitenga jimbo la Biafra kule Nigeria. Tulipeleka pesa nyingi na inawezekana hata ushauri wa kivita.
Mafanikio ya Nyerere kwenye uchumi wa Tanzania ni sifuri, au tuseme “negative”. Watanzania tulipata shida sana asana. Kwa wale ambao hawakuwepo wakati huo wasiombee maisha kama yale yawafike. Ilifika wakati ilibidi sukari, sabuni ya mbuni, mchele, unga wa mhogo(makopa), betri, viberiti,n.k vyote vilipatikana kwa mjumbe wa nyumba kumi. Kuwa nyumba kumi wakati huo ulikuwa umeukata. Wakati Nyerere anaachia ngazi pale Benki kuu walikuwa na dola laki tano tu. Walishindwa kununua mafuta na nchi nzima magari yalisimama. Wakati huo magari hayakuwa mengi kwani watu hawakuwa wanruhusiwa kuwa na magari na wale waliokuwa nayo walikuwa hawaruhusiwi kuendesha Jumapili kuanzia saa nane mchana.
Kuhusu “villagilisation” Nyerere hawezi kukwepa lawama. Tamaa ya Nyerere ilikuwa ni kuweka watu pamoja na kudhani watabadilika kuwa wajamaa. Kwa vile alizungukwa na wapamabe tu kama akina Kawawa, Songambele, etc. basi walifanya chochote kumfurahisha. Nakumbuka kijijini kwangu kuna mzee wa zaidi wa miaka 60 alihamishiwa umbali wa chini ya kilomita moja kutoka kwenye nyumba yake wakati nyumba zake zote alikuwa ameezeka bati na ikabidi ajenge vibanda vya miti na kueezeka majani. Nyumba zake za zamani walichoma moto kwa vile alikuwa hataki kuhama. Alikufa katika hali ya umasikini sana. Kule Tabora kuna watu wanaitwa Mgaya kumkumbuka mkuu wa mkoa wa wakati huo Philemon Mgaya ambaye alikuwa kinara wa kuchoma nyumba zao moto na wengi waliliwa na samba.
Kuna mtu anazungumzia kuwa wakati wa Nyerere hakuna ” intelletuals” waliosomeshwa. Hiyo siyo kweli. Nitataja mmoja ambaye ndiye mtu mweusi wa kwanza kupendekezwa kupewa tuzo la Nobel kwenye Science, Dr. Hezekeiah Kamuzora ambaye alikuwa anafanya kazi kama Biochemist pale Muhimbili. Hata hivyo kielime Tanzania tulididimia sana wakati wenzetu walikuwa wanendelea. Mpaka miaka ya 80 Nyerere alikuwa hataki Watanzania wengi waingie kwenye elimu ya sekondari wakati majirani zetu walikuwa wanapanua elimu ya vyuo vikuu. Kwa mfano, alipinga sana mikakati ya kujenga shule za sekondari za tarafa kule wilayani Njombe ambazo zilijulikana kama NDDT akisema kuwa badala yake wajenge “vocational colleges”

Heh! kumbe hata kwa wagalatia wenzake alikuwa mwiba ?!!! kesho kutwa anataka kutangazwa MWENYE HERI ! baada ya kukosa Nobel award !
 
Kumbukumbu zangu zinanituma kuamini hivyo. Katika Afrika ni wachache wamewahi kupata tuzo hii yenye hadhi nadhani kushinda zote. Kapata Mandela, Tutu, Wathari, n.k. Nyerere hakuwa na mchango unaostahili hii tunzo? Tunahitaji kufahamu hili toka kwa wajuvi

Kiswahili safi ni 'TUZO'. Tunzo ni kitu kingine. (Huchukia watu wanaokosea Kiswahili mimi!)
 
huoni kuwa kwa maelezo yako, hapo kwenye red ndipo matatizo yalipoanzia? kwamba Nyerere hakuwa kipenzi cha wazungu bali mwiba kwao?
 
Mimi ni kati ya watu ambao siyo mshabiki sana wa Nyerere. Nilianza shule wakti Tanzania ndiyo mwanzo imepata uhuru. Maisha ya Tanganyika/Tanzania kwa kweli yalikuwa duni sana. Wakati Tanganyika tunapata uhuru hali yetu ya kiuchumi haikuwa tofauti sana na ile nchi za South East Asia – Malaysia, Singapaore, Thailand, etc. Leo tumeachwa mbali sana.
Nyerere alikuwa na tatizo kubwa na kudhani kuwa wengine hawajui kitu. Kila kitu anajua yeye na ukimbishia basi wewe ni adui yake wa maisha. Hawezi kukusamehe kabisa. Hakuwa mtu anayependa kuonea watu lakini alipenda sana kulipiza kisasi. Mifano ipo mingi. Akina Tuntemeke Sanga ambaye aliambiwa asitembee nje ya wilaya ya Njombe, Oscar Kambona alimpa baba yake (an Anglican Pastor) gari la Landrover. Oscar alipokimbilia UK yule mzee aliambiwa lile gari lisitembee hata nchi moja. Liliozea lilopoegeshwa.
Katika Africa yeye alijipatia sifa nyingi katika kuongoza vita za kulikomboa bara hili. Wazungu wengi hawakupenda siasa yake ya ujamaa wakidhani kuwa itaenea bara zima. Lakini katika Afrika Nyerere vilevile aliwahi kufanya vitendo ambavyo alikuja kuvijutia baadaye kama kuunga mkono kwa kujitenga jimbo la Biafra kule Nigeria. Tulipeleka pesa nyingi na inawezekana hata ushauri wa kivita.
Mafanikio ya Nyerere kwenye uchumi wa Tanzania ni sifuri, au tuseme "negative". Watanzania tulipata shida sana asana. Kwa wale ambao hawakuwepo wakati huo wasiombee maisha kama yale yawafike. Ilifika wakati ilibidi sukari, sabuni ya mbuni, mchele, unga wa mhogo(makopa), betri, viberiti,n.k vyote vilipatikana kwa mjumbe wa nyumba kumi. Kuwa nyumba kumi wakati huo ulikuwa umeukata. Wakati Nyerere anaachia ngazi pale Benki kuu walikuwa na dola laki tano tu. Walishindwa kununua mafuta na nchi nzima magari yalisimama. Wakati huo magari hayakuwa mengi kwani watu hawakuwa wanruhusiwa kuwa na magari na wale waliokuwa nayo walikuwa hawaruhusiwi kuendesha Jumapili kuanzia saa nane mchana.
Kuhusu "villagilisation" Nyerere hawezi kukwepa lawama. Tamaa ya Nyerere ilikuwa ni kuweka watu pamoja na kudhani watabadilika kuwa wajamaa. Kwa vile alizungukwa na wapamabe tu kama akina Kawawa, Songambele, etc. basi walifanya chochote kumfurahisha. Nakumbuka kijijini kwangu kuna mzee wa zaidi wa miaka 60 alihamishiwa umbali wa chini ya kilomita moja kutoka kwenye nyumba yake wakati nyumba zake zote alikuwa ameezeka bati na ikabidi ajenge vibanda vya miti na kueezeka majani. Nyumba zake za zamani walichoma moto kwa vile alikuwa hataki kuhama. Alikufa katika hali ya umasikini sana. Kule Tabora kuna watu wanaitwa Mgaya kumkumbuka mkuu wa mkoa wa wakati huo Philemon Mgaya ambaye alikuwa kinara wa kuchoma nyumba zao moto na wengi waliliwa na samba.
Kuna mtu anazungumzia kuwa wakati wa Nyerere hakuna " intelletuals" waliosomeshwa. Hiyo siyo kweli. Nitataja mmoja ambaye ndiye mtu mweusi wa kwanza kupendekezwa kupewa tuzo la Nobel kwenye Science, Dr. Hezekeiah Kamuzora ambaye alikuwa anafanya kazi kama Biochemist pale Muhimbili. Hata hivyo kielime Tanzania tulididimia sana wakati wenzetu walikuwa wanendelea. Mpaka miaka ya 80 Nyerere alikuwa hataki Watanzania wengi waingie kwenye elimu ya sekondari wakati majirani zetu walikuwa wanapanua elimu ya vyuo vikuu. Kwa mfano, alipinga sana mikakati ya kujenga shule za sekondari za tarafa kule wilayani Njombe ambazo zilijulikana kama NDDT akisema kuwa badala yake wajenge "vocational colleges"
Nahisi una tatizo au la elimu au umri mdogo wakati hayo yakitokea. Mimi huchukia utiaji habari chumvi yaani exageration. Kwanza tuanze kwenye grey - Si kweli hata kidogo kwamba enzi za Nyerere maendeleo yalikuwa "Sifuri" kwani pamoja na uchumi duni aliourithi toka kwa wakoloni Nyerere alifaulu kikamilifu kutoa huduma za jamii bila malipo tena huduma za viwango. Matibabu hospitali yalikuwa bure kabisa tena bila rushwa wala mizengwe na waliolazimika kupelekwa nje walipelekwa bila kujali vyeo na nafasi zao; tofauti na siku hizi hadi uwe fulani. Elimu ilikuwa ya bure kwelikweli hadi ukomo wa uwezo wa mtu binafsi. Wengi wetu wa rika la JK na kumzidi tulinufaika na hayo na tulio wakweli mbele ya Mungu tutashuhudia haya. Izingatiwe Nyerere alimudu kufanya hayo kwa mapato ya pamba na mazaoya kilimo bila ya kuchimba migodi ya dhahabu kama ilivyo sasa! Hakuna shaka kwamba elimu iliyokuwa inatolewa ilikuwa bora kuliko sasa kwa vigezo vya uwiano wa wanafunzi na walimu tena wanafunzi walikuwa hawakai chini kwenye mavumbi na wala Nyerere hakulazimika kuwapeleka watoto wake nje ya nchi kama ilivyo kwa viongozi wa sasa wanaohangaika kuhubiri ubora wa elimu wanayotoa wakati watoto wao wanasomea nje ya nchi au katika ma Academy yaliyojengwa kwa fedha zilizokwapuliwa serikalini kifisadi. Kuhusu maisha magumu unayosema hadi watu kupata viberiti, sukari kupitia kwa wajumbe wa nyumba kumi kumi kile kilikuwa kipindi cha mpito wa hali ngumu kiuchumi yaani recession baada ya vita vya uvamizi wa nchi yetu na si ajabu hata kidogo kwa nchi kupitia hali kama ile au hata mbaya zaidi baada ya vita ambapo nchi huwa imemaliza akiba zake zote kwa ajili ya shughuli ya kujihami. Ujerumani na nchi nyingi tu zilipitia hali mbaya kuliko hiyo tuliyoipitia Tanzania. Wale wasomi wa historia ya dunia watashuhudia hili. Ikumbukwe baada ya vita nchi ilikabiliwa na ukame ambapo serikali ilibidi kutumia fedha kidogo iliyokuwa nazo kuagiza nje chakula cha kuwanusuru wananchi wake na Nyerere alikiri ahdharani kwamba kuwalisha wananchi kwa chakula cha kununua si mchezo. Hakuna nchi ya magharibi iliyokuwa tayari kutusaidia chakula wala fedha kutunusuru ili kumkomoa Nyerere waliyekuwa wakimwombea mabaya baada ya kuonekana "mkorofi" kwa vigezo vyao. Udhibiti wa wajumbe ulikuwa lazima kupambana na wachache waliotaka kuitumia hali ile kujinufaisha. Laiti hali ile ingetokea sasa ambapo udhibiti ni legelege tungeshuhudia vifo vingi tu.
Kwenye green inasikitisha mno kutaja takwimu kishabiki, hebu tueleze ulipata wapi hizo takwimu za dola laki tano tu? Nasema hivi, laiti kama kusingekuwa vita vya Nduli nchi hii ingeshuhudia hatua kubwa tu ya kimaendeleo kwani mambo yalikuwa yakienda vizuri kabisa hadi baada ya uvamizi ule. Tanzania tulikuwa na viwanda vingi tu na misingi imara ya kiuchumi ambayo ilsambaratika baada ya vita kwa ukata na hujuma za watu kama nyinyi.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
Kumbukumbu zangu zinanituma kuamini hivyo. Katika Afrika ni wachache wamewahi kupata tuzo hii yenye hadhi nadhani kushinda zote. Kapata Mandela, Tutu, Wathari, n.k. Nyerere hakuwa na mchango unaostahili hii tunzo? Tunahitaji kufahamu hili toka kwa wajuvi

...Pamoja na Nyerere kutopata tuzo ya Nobel mchango wake katika bara la Afrika ni mkubwa mno kuliko kiongozi mwingine yeyote yule wa Afrika. Na hii ndio sababu alipata umaarufu mkubwa katika nchi nyingi za Afrika kwa mazuri mengi aliyoyafanya kwa Tanzania na Afrika.
 
"Wanadamu wasipokuinua Mungu atakuinua!" Mwl Julius Nyerere,the greatest leader this continent EVER produced!! Semeni yote,hakuna cha kubadili ukweli!
 
Nahisi una tatizo au la elimu au umri mdogo wakati hayo yakitokea. Mimi huchukia utiaji habari chumvi yaani exageration. Kwanza tuanze kwenye grey - Si kweli hata kidogo kwamba enzi za Nyerere maendeleo yalikuwa "Sifuri" kwani pamoja na uchumi duni aliourithi toka kwa wakoloni Nyerere alifaulu kikamilifu kutoa huduma za jamii bila malipo tena huduma za viwango. Matibabu hospitali yalikuwa bure kabisa tena bila rushwa wala mizengwe na waliolazimika kupelekwa nje walipelekwa bila kujali vyeo na nafasi zao; tofauti na siku hizi hadi uwe fulani. Elimu ilikuwa ya bure kwelikweli hadi ukomo wa uwezo wa mtu binafsi. Wengi wetu wa rika la JK na kumzidi tulinufaika na hayo na tulio wakweli mbele ya Mungu tutashuhudia haya. Izingatiwe Nyerere alimudu kufanya hayo kwa mapato ya pamba na mazaoya kilimo bila ya kuchimba migodi ya dhahabu kama ilivyo sasa! Hakuna shaka kwamba elimu iliyokuwa inatolewa ilikuwa bora kuliko sasa kwa vigezo vya uwiano wa wanafunzi na walimu tena wanafunzi walikuwa hawakai chini kwenye mavumbi na wala Nyerere hakulazimika kuwapeleka watoto wake nje ya nchi kama ilivyo kwa viongozi wa sasa wanaohangaika kuhubiri ubora wa elimu wanayotoa wakati watoto wao wanasomea nje ya nchi au katika ma Academy yaliyojengwa kwa fedha zilizokwapuliwa serikalini kifisadi. Kuhusu maisha magumu unayosema hadi watu kupata viberiti, sukari kupitia kwa wajumbe wa nyumba kumi kumi kile kilikuwa kipindi cha mpito wa hali ngumu kiuchumi yaani recession baada ya vita vya uvamizi wa nchi yetu na si ajabu hata kidogo kwa nchi kupitia hali kama ile au hata mbaya zaidi baada ya vita ambapo nchi huwa imemaliza akiba zake zote kwa ajili ya shughuli ya kujihami. Ujerumani na nchi nyingi tu zilipitia hali mbaya kuliko hiyo tuliyoipitia Tanzania. Wale wasomi wa historia ya dunia watashuhudia hili. Ikumbukwe baada ya vita nchi ilikabiliwa na ukame ambapo serikali ilibidi kutumia fedha kidogo iliyokuwa nazo kuagiza nje chakula cha kuwanusuru wananchi wake na Nyerere alikiri ahdharani kwamba kuwalisha wananchi kwa chakula cha kununua si mchezo. Hakuna nchi ya magharibi iliyokuwa tayari kutusaidia chakula wala fedha kutunusuru ili kumkomoa Nyerere waliyekuwa wakimwombea mabaya baada ya kuonekana "mkorofi" kwa vigezo vyao. Udhibiti wa wajumbe ulikuwa lazima kupambana na wachache waliotaka kuitumia hali ile kujinufaisha. Laiti hali ile ingetokea sasa ambapo udhibiti ni legelege tungeshuhudia vifo vingi tu.
Kwenye green inasikitisha mno kutaja takwimu kishabiki, hebu tueleze ulipata wapi hizo takwimu za dola laki tano tu? Nasema hivi, laiti kama kusingekuwa vita vya Nduli nchi hii ingeshuhudia hatua kubwa tu ya kimaendeleo kwani mambo yalikuwa yakienda vizuri kabisa hadi baada ya uvamizi ule. Tanzania tulikuwa na viwanda vingi tu na misingi imara ya kiuchumi ambayo ilsambaratika baada ya vita kwa ukata na hujuma za watu kama nyinyi.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
Well said Mkuu, Asante kwa darasa la kina. Kwenye bold black sina la kuongeza kwani ni ukweli mtupu. Kelele za kubreshwa viwango vya elimu na matibabu ni usanii tu maana watoto wao hawasomi hizo shule "za kumwaga" kwenye kata na badala yake wanasomea ulaya na Afrika ya kusini. Kumbe hizi shule zinajengwa kutupiga dongo la macho sisi walala hoi wakati wao wanajiandalia tabaka la kuwarithi yaani watoto na wajukuu zao wanaopata elimu bora nje na kwenye ma - academy.
Kwenye grey pia ni darasa tosha kwangu na kwa wanaoweza kukuelewa kwani hata mtikisiko kiuchumi wa Marekani sasa una chanzo chake kwenye matumizi makubwa ya vita za Iraq na Afghanistan. Mwenye akili yeyote analifahamu hilo. Kwa mantiki hii hali ngumu kiuchumi iliyoukumba utawala wa Nyerere katika miaka yake ya kumalizia uongozi si kipimo cha kushindwa kwa sera zake. Tena nadhani hali ingekuwa mbaya zaidi kama tusingekuwa na sera za kijamaa, yaani kiutu. Nasema tena asante kwa darasa.
 
Mtu anayesaliti Uasili wake, hana maana kabisa! Mtu akisaliti uasili wake ambao ni utu wake awekwe kundi gani?
Uasili wa mnyama ni Unyama! Wanyama hawakuusaliti uasili wao kufikia Unyama ulio uasili na sifa yao!

Mwanadamu anayesaliti Uasili wake hawezi kuuitwa Mnyama kwani hilo si kosa kwa wanyama bali ni sifa ya tabaka lao! Mwanadamu aliyetesaliti tabaka lake hana sifa ila kajikosea heshima hivyo kumtunuku jina na sifa ya Unjama ni kumpa hadhi na kumkweza kusiko na maana!

Kuusaliti Utu wa Mtu hakuwezi kamwe kumpata Mnyama! Mtu anayesaliti Utu wake amejishushia heshima na hadhi na amejishusha daraja ... chini ya daraja la wanyama. Mtu au Kiongozi anayeenzi Utu na kuuheshimu ni mtu wa kuheshimiwa na kuenziwa!

Kumheshimu mtu mwenye kuheshimu Utu ... Ni Kuheshimu Utu wako na wa jamii nzima. Ni kujiondoa kwenye tabaka lililo duni lisillo hata na hadhi ya kulinganishwa na wanyama. Ni Kuwa na UTU, kuwa Mkamilifu na kuwa Mwanadamu Timamu!

Nyerere ali utambua UTU wa Mtu! Aliupigania, aliutetea na kuusimamia! Na aliufia!!!

NOTE: Utu ni nini? https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-lugha/192708-nini-hasa-maana-ya-utu.html
 
Kumbukumbu zangu zinanituma kuamini hivyo. Katika Afrika ni wachache wamewahi kupata tuzo hii yenye hadhi nadhani kushinda zote. Kapata Mandela, Tutu, Wathari, n.k. Nyerere hakuwa na mchango unaostahili hii tunzo? Tunahitaji kufahamu hili toka kwa wajuvi

Nyerere angeweza pewa tuzo hiyo pengine in the long run kama angeendelea na peace mission yake in the region, vinginevyo kwa mazingira ya wakati ule ambapo alikuwa ana advocate for ujamaa, mabepari (ambao ndio watoa tuzo hiyo), wasingeweza kufanya kitu kama hicho; infact sidhani kama kuna mtu yeyote anti - capitalist aliyewahi pewa tuzo hiyo;
 
Nakubaliana na wewe
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom