Nyerere hakuwahi kupata tunzo ya Nobel

Kumbuka, kuhamisha makundi kwa makundi ya watu kuwasomba na kuwatupa porini, ukiwaamrisha "anzisheni kijiji cha ujamaa", simba, chui, nyoka, ndio wanawangoja, hakuna matibabu wala usafiri, hakuna nyumba wala tembe. "Imagine scenario" kama hiyo, ni wangapi waliopoteza maisha yao! Halafu apewe Noble prize. Is that "scenario" noble to you? If not, huyo ndio nyerere na hayo yametokea na si ya kuhadithiwa. Nilikuwepo.

Mahatma Ghandhi hakuwahi kupata Nobel, naye alifanya nini kinachofanana na Nyerere!
 
Kumbuka, kuhamisha makundi kwa makundi ya watu kuwasomba na kuwatupa porini, ukiwaamrisha "anzisheni kijiji cha ujamaa", simba, chui, nyoka, ndio wanawangoja, hakuna matibabu wala usafiri, hakuna nyumba wala tembe. "Imagine scenario" kama hiyo, ni wangapi waliopoteza maisha yao! Halafu apewe Noble prize. Is that "scenario" noble to you? If not, huyo ndio nyerere na hayo yametokea na si ya kuhadithiwa. Nilikuwepo.

Bwana majimshindo!
Ni vizuri hata kama humpendi mtu, basi toa maelezo ya ukweli (yawe mabaya au mazuri). Na hata kama unapenda kutoa mabaya tu, basi toa hayo mabaya kwa ufasaha, ukiweka ukweli tu badala ya kuweka tungo tata ambazo zinaweza zikatoa maana nyingine.

Jinsi ulivyoandika hapo, ungekuwa mwandishi wa historia kama yule jamaa yetu, kitabu chako kingekuja kuonesha kama vile Nyerere alikuwa anawakamata watu na kuwatupia sehemu zenye wanyama akiwa na makusudi kabisa kuwa watu hao waliwe.

Nakuomba ufanye utafiti, nenda mikoani, katembelee sehemu mbalimbali ambazo vijiji vya ujamaa viliulindwa, na maeneo yaliyofanyiwa "operesheni sogea". Kafanye bila bias.

Utagundua kuwa nia ya Nyerere ilikuwa ni kuongeza productivity, na kusogeza huduma za jamii kama shule na hospitali kwa kaya ambazo kabla ya hapo zilikuwa zinakaa mbali mbali sana. Kuna baadhi ya miji midogo hadi sasa inandelea kukua vizuri, lakini ilianzishwa kwa operesheni sogea. Na kuna sehemu ambazo wananchi walikuwa wabishi, waligoma kusogea au kwenda kwenye vijiji vya ujamaa, sehemu hizo mpaka sasa bado ziko duni, na vijiji vyao vimekaa kienyeji zaidi.

Pia utakubali rohoni kwako kuwa Nyerere hakuwa kutoa amri kwa watendaji wake kwamba wawa "mistreat" raia hasa hilo suala la kuwatupa kwenye simba. Kama ambavyo humlaumu Kikwete kwa bomoa bomoa inayosimamiwa na waziri wake, basi hata nyerere huwezi kumlaumu kama ulivyofanya.

Lazima ufahamu pia zoezi lile la ujamaa villagisation lilikuwa sponsored na WB huku wakiwa wameagizwa na Western countries kuwa "lisifanikiwe" kwa sababu hawakutaka kuwepo na "socialist island" eneo hili. Kufanikiwa kwa lile zoezi kungeleta matatizo ya kuenea zaidi kwa ujamaa, kitu ambacho Western capitalists hawakutaka. Kulikuwa na "sabotage" kubwa ya lile zoezi ili nchi za magharibi zichukulie Tanzania kama mfano wa kushindwa ujamaa (Kama una marafiki Uingereza, wanaweza kukusaidia zaidi, kwasababu mwaka 2001 MI6 wali-declassify this information na kuwa accessible to the public. Walieleza jinsi nchi za magharibi zilivyo-conspire against Nyerere and his Ujamaa).

Nataka ufahamu pia kuwa yale unayofikiri umejielimisha mwenyewe kuhusu lile zoezi (labda kwa kujisomea au kusikiliza stories), sio yote ya kweli. Hata baadhi ya waandishi wazalendo walilishwa sumu hiyo hiyo na vitengo vya "disinformation and misinformation" vya CIA na MI6. Utakumbuka kuwa vyombo vya habari vya magharibi vili-document makusudi kuhusisha njaa ya 1974 na zoezi la ujamaa vijijini ilhali tatizo kubwa ilikuwa ukame na kupanda kwa mafuta duniani.

Sina uhakika na umri wako, lakini nina-assume utakumbuka ukame uliokumba nchi za kusini kuanzia malawi, Zimbabwe, Botswana, Zambia na Namibia miaka ya majuzi. Kama ulifuatilia kipindi kile, ndio Mugabe alikuwa anaanza ku-implement mambo yake ya land re-distribution. Kwa vile watu wa magharibi hawakupenda mambo ya Mugabe, muda wote walikuwa wanakazania (kwa makusudi) ku-report kuwa njaa ya zimbabwe ilitokana na siasa mbaya za Mugabe na walikuwa hawataki kugusia mambo ya ukame. Ukame ulikuwa unahusishwa na njaa ya nchi nyingine tu.

Kwa hiyo ndugu yangu, unaposoma na kusikiliza na kuandika, jitahidi kuwa makini. Kuna vingine unaweza ukaviamini kwa vile aliyeandika au kukusimulia anataka kweli wewe uamini hivyo.

I hope umenipata.

Kila la kheri!
 
Naomba kutofautiana na wewe. Ukisoma wasifu wake, yeye anatuhumiwa pia kwa kusababisha hali kuwa tete katika baadhi ya nchi. Yeye ndiye alikuwa anakaa na wafuasi na anawasaidia kuangusha baadhi ya serikali. Hivyo alikuwa ni kama ndumi la kuwili.

unamzungumzia Nyerere? Alikaa na wafuasi wapi ili kupindua serikali zipi? Na pia alionekana mzuri na mbaya kwa nani?
 
Unaongelea wasifu upi? na ulioandikwa na nani na umechapwa wapi?
Hapa hatuongei kwa hisia tu au hadithi za kwenye vijiwe. Tafadhali tuwekee maandiko yenye uthibitisho wa yeye kushirikiana na waasi kuangausha serikali. Kama huna takwimu au uthibitisho wa unayosema tuombe radhi kwa uzushi na umbea, lau kama unao mimi nitakuomba radhi.
 
unamzungumzia Nyerere? Alikaa na wafuasi wapi ili kupindua serikali zipi? Na pia alionekana mzuri na mbaya kwa nani?
Kama katika kufanikiwa, Nyerere alifanikiwa kutufanya tumuamini na tuamini kila linalohusu Taifa letu. Tuliimbishwa nyimbo nyingi saana za kumsifu yeye na chama chake tunachokilalamikia leo hii. Wengi wa viongozi wa leo ni zao lake na hali ya umasikini wetu pia kwa kiasi kikubwa ni zao. Nchi yetu imepata uhuru takribani miaka 50 iliyopita. Katika hiyo Nyerere ameongeza takribani miaka 25 na wengine watatu ni hiyo 25 iliyobakia. Ingawa wengi tunawadai hawa waliongoza miaka 25 kwa pamoja zaidi ya yule aliyeongoza miaka 25 peke yake. Tukiachana na haya tukarudi kwenye quote; Nyerere ndiye aliyewasaidia kina Museveni katika harakati zao kule Uganda na wengine kule Zaire. Ni Nyerere huyu ambapo watu hawakuwa na uhuru wa kupingana naye. Wengi tu walipotea au waliishia kuitwa wahaini kwa kuipinga serikali yake. Leo hii tunataka tumpe tuzo ya amani.
 
mkuu, ukimsoma Nanren hapo juu kachambua kwa ufasaha sana. Ujamaa/Socialism ni itikadi kama ilivyokuwa kwa ubepari. Nyerere aliamini katika ujamaa ambao mabepari walihakikisha haufanikiwi. Kama ujamaa haukuwa tishio kwa nini wazungu waliupinga? Leo hii tuna ubepari. Unajua ni watanzania wangapi wamekufa kutokana nao? Migodini, serikalini (kombe, malima, kolimba, et al), barabarani, huduma za kijamii, etc. Mabepari wanaua kiasi gani huko mashariki ya kati na Afrika? Kama ujamaa ulikuwa ni tatizo, ubepari umeondoa tatizo?
 
Kama katika kufanikiwa, Nyerere alifanikiwa kutufanya tumuamini na tuamini kila linalohusu Taifa letu. Tuliimbishwa nyimbo nyingi saana za kumsifu yeye na chama chake tunachokilalamikia leo hii. Wengi wa viongozi wa leo ni zao lake na hali ya umasikini wetu pia kwa kiasi kikubwa ni zao. Nchi yetu imepata uhuru takribani miaka 50 iliyopita. Katika hiyo Nyerere ameongeza takribani miaka 25 na wengine watatu ni hiyo 25 iliyobakia. Ingawa wengi tunawadai hawa waliongoza miaka 25 kwa pamoja zaidi ya yule aliyeongoza miaka 25 peke yake. Tukiachana na haya tukarudi kwenye quote; Nyerere ndiye aliyewasaidia kina Museveni katika harakati zao kule Uganda na wengine kule Zaire. Ni Nyerere huyu ambapo watu hawakuwa na uhuru wa kupingana naye. Wengi tu walipotea au waliishia kuitwa wahaini kwa kuipinga serikali yake. Leo hii tunataka tumpe tuzo ya amani.
Nadhani mkuu hata ukielimishwa kwa tani na tani za ufahamu kuhusu Nyerere hutaelimika. Hutamfahamu Nyerere na wala huna nia ya kumfahamu Nyerere. Kwa taarifa Nyerere ni mmoja wa watu aliyejipambanua kutaka kuijenga nchi yake isimame imara bila kutegemea wakoloni. Kujipambanua huko kulimjengea uadui mkubwa kutoka kwa hao Wakoloni. Mara baada ya Uhuru wa Tanganyika 1961 Nyerere aliwaambia wakoloni kuwa baada ya Miaka kumi ya uhuru wa Bendera waje Tanganyika wajionee wenyewe mabadiliko ambayo Tanganyika Huru itakuwa imeyafanya. Katika sherehe za miaka kumi ya Uhuru Nyerere alihorodhesha mafanikio na kweli yalikuwa mengi. Hatua iliyokuwa inafuata ni ku consolidate gains zilizokuwa zimepatikana ndani ya Miaka kumi. Utakumbuka hapo ndipo series of sabotage events zilipoanza. Uganda ikawa Chini ya Kibaraka Idd Amin, Mpango wa kuhamia Vijiji vya ujamaa 1974 ukahujumiwa; East Afican Community ikavunjika chini ya vinara akina Njonjo 1978. Vita ya Kagera 1978 na Uhodhi wa bidhaa muhimu na kundi la wafanyi biashara ambao walikuwa makuadi wa mapebari na mabeberu 1980 - 1984. Na ndio ukawa mwisho wa utawala wa Nyerere na Sera za Ujamaa. Nionavyo mimi wewe ni mmoja wa waumini wa sera za ubeberu na ukandamizaji wa Magharibi. Kwa hiyo sishangai mawazo yako hasi kuhusu kazi za kutukuka za Mwalimu Nyerere na wala sintoshangaa kamwe.
 
kuna watu humu wanadhani nyerere alikuwa mungu. economic policies ovyo, political system yake ilikuwa ovyo! ivi kweli nyerere amefanya nini cha kusema apewe tuzo? Zaidi ya kuunganisha Tz na kiswahili. Kuna wengine wamedai bila nyerere mandela asingetoka. embu fafanueni hiyo contribution yake kwenye hilo swala! Nyerere was no global icon, didnt make any global impact.
 
Mzee hili swali lingeulizwa kwa Obama vile vile alipopata Nobel Peace Prize alikuwa amefanya nini? Kwani Wathari naye amefanya nini kwenye world stage? Mandela na De Clerk walifanya nini kwenye world stage?

Just goes to show you how worthless these awards are. Yule nut Waathari ilikuwa wakati wa mambo ya gender balance pamoja na environmentalism, wakatafuta Mwanamke muafrika (disgraceful conspiracy theorist), we unaenda kumpa zawadi De Klerk? baada ya ubaguzi wote? Na Mandela kuikubali zawadi kawa sellout. Mwenzake Le Duc Tho wa Vietnam ya Kaskazini enzi hizo alipewa tuzo ya amani ya Nobel pamoja na Dr. Henry Kissinger, mchizi akaikataa kwa kuona ni uzushi tu.

Obama kapewa tuzo kabla hata ya kufanya chochote substantial.

Tuzo yenyewe politics tupu, bora hata alivyokosa kaenda kujiunga na kina Gandhi huko.
 
kuna watu humu wanadhani nyerere alikuwa mungu. economic policies ovyo, political system yake ilikuwa ovyo! ivi kweli nyerere amefanya nini cha kusema apewe tuzo? Zaidi ya kuunganisha Tz na kiswahili. Kuna wengine wamedai bila nyerere mandela asingetoka. embu fafanueni hiyo contribution yake kwenye hilo swala! Nyerere was no global icon, didnt make any global impact.

Sidhani kama kuna mtu anamfananisha Nyerere na Mungu. Mungu ni Mungu hawezi fananishwa na chochote. Nyerere alikuwa mtu, kiongozi mwenye msimamo, mzalendo. Lakini bado alikuwa ni binadamu.

Lakini ukiwa na sababu zako za kumchukia si lazima watu wote wakubaliane na sababu zako na wote wamchukie.

Wakati unaendelea kumchukia kwa kuwa na economic and political policies mbaya, kwa faida yako, jaribu kuangalia nchi nyingine kama Malawi na Kenya, somali, Zimbabwe, Madagascar, Zambia na nyingine nyingi za Africa. Pia angalia nchi nyingine za dunia ya tatu ambazo hazikuwa na Nyerere wala hazikufuata siasa ya ujamaa kama tulivyofanya chini ya nyerere. Angalia maendeleo yao. Wamekuzidi nini?

Kuna kipindi kirefu sana ambapo nchi za magharibi kwa kutofurahishwa na msimamo wa Nyerere wa kuunga mkono juhudi za ukombozi, walihakikisha kuwa hafanikiwi, na wakaeneza propaganda kuwa ni kutokana na sera mbovu za uchumi. Nafikiri wewe unameza tu habari kama hizo. Sasa jiulize nchi zote hizo zingine ambazo hazikufuata sera kama za Nyerere kwanini mpaka leo ni maskini?
Unawaamini watu wa magharibi wakimkandia Nyerere, ila hao hao wakikwambia wanapeleka demokrasia Iraq huwaamini!! Ajabu!!

Kwa taarifa yako, tuzo ya nobeli hasa ya amani na literature, huwa kuna "politics". Marehemu Yitzhak Rabin na Yasser Arafat walipewa tuzo ili kuwa-encourage wafanikishe amani kati ya waisraeli na Wayahudi. Mandela alipewa tuzo pamoja na Deklerk hasa ikiwa ni kuendelea kumpooza kwa kuwasamehe wazungu. Angekuwa amesamehe rangi nyingine wala asingepewa. Juzi juzi hapa kuna tuzo imetolewa kwa mchina mmoja ili tu kufahamisha ulimwengu kuwa kuna mwanaharakati yupo kizuizini nchini China. Hata Obama alipewa wakati tu kaingia madarakani.

Jaribu kusoma jinsi Nyerere alivyokuwa mwiba kwa siasa za kibeberu za nchi za magharibi, halafu ndio utajua kuwa hata kama angekuwa mzuri vipi, wasingempa. It's all politics.
 
haijalishi kama nampenda au simpendi Nyerere. I am actually neutral kwenye ishu ya Nyerere. Hizo contribution za Nyerere unazosema katika bara la Africa si uziandike hapa tusome. Mbona unazitaja juu juu tu? weka data kama unazo. Au utadai pia na hizo 'west' walichakachua?
Aliyekuwa mwiba wa siasi za kibepari ni nani zaidi kati ya hawa wawili Che Guevera au Nyerere? Now how would you compare the two katika u-mwiba wao?
Ivi siasi ya kupora wananchi mali zao ni haki? Nyerere alizuia maendeleo sana katika hii nchi. Ivi kweli tunasahau watu kupanga foleni kwa ajili ya sabuni? Sabuni yenyewe ni ile ya mche!! Ukitoka Kenya mpakani unapekuliwa kama nini, na usikutwe na sabuni au toilet paper. Ivi kweli mtu mwenye sera za kijinga ivyo utaweza kumwelewa? He simply had pathetic economical policies.
Further, wewe hata siku moja usijaribu kujifananisha na Kenya. Kenya wametuacha mbali mno kiuchumi na kielimu. Na walitupiga gap kubwa kutokana na hizo sera za Nyerere. Ivi unaweza kunitajia wasomi wakubwa watano Tanzania ambao ni product ya system ya Nyerere.People who have actually done something in Tanzania? Actually nipe mmoja tu...Born and Bread in Tanzania. Kikwete is a classical example of Nyerere's products katika sera yake ya elimu. Ona jinsi alivyo hovyo. Na kutokana na ujinga mwingi uliokithiri Tanzania, ambao umejengwa na sera za Nyerere hakuna mtu anayeweza kuona haja ya mabadiliko. Akili zimepumbazwa na proganda kibao kama 'zidumu sera za mwenyekiti', nk.
Sijasema kuwa tuzo haina upendeleo. Lakini nasema Nyerere did not deserve it!!
 
Tatizo ni kukumbatia umbumbu wa historia ya nchi na kuona fahari ya yasiyokuwepo. Nyerere alikuwa kiongozi ambaye alithubutu kutaka kuona nchi yake inakuwa huru kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Aliweka sera bayana na alionesha dira ni wapi tulitakiwa kwenda kama nchi. Watu wa aina yako ambao wanaota kuishi kwenye raha za kimagharibi ( ndoto za alinacha) na mabwana zao waliihujumu nchi na hivyo tukakwama. Historia ipo wazi katika hili. Soma maandiko yapo mengi si lazima ujuzwe hapa jamnvini. Lakini kwa vile huoni, husikii wa uambiliki ni kupoteza nguvu bure kukujuza. Maana hata huyo Nyerere unayemshambulia humjui hata chembe.
 
hahaha...nimegusa mshipa ehhe? kwa hiyo ninayosema hayakuwepo aka umbumbu wangu? hahaha! huna jipya mazee! anyway...naona wewe ndio unamjua Nyerere kweli humu jamvin. Kwa hiyo huyu bwana alileta maendeleo na sera zake ehhe? Tanzania ilitoa wasomi wangapi wakati wake?
1. whether u like it or not hakuna nchi inayoweza kuwa kisiwa hapa duniani. kwa yeye kufikiria kuwa Tanzania ingeweza kupiga hatua na sera mbovu za kujaribu kujikomboa kutoka 'the west' inaonyesha naivity yake katika kuelewa ishu za uchumi. Tafadhali usionyeshe ufinyu wa fikra zako pia.
2. Hakuna mtu anayependa kuishi kwa taabu hapa duniani. loliondo is a current live example. Sasa tuone nani ata-enjoy maisha kati yangu mimi 'ninayeota' kuishi ki-magharibi (kwa rahaaaa) na wewe usiyejua uendako na kupigwa bao na mafisadi kila siku. wewe baki na hiyo 'great knowledge' yako ya Nyerere na miujiza yake aliyotenda Tanzania, lakini ukweli unabaki pale pale...the man failed miserably.
 
Bwana majimshindo!
Ni vizuri hata kama humpendi mtu, basi toa maelezo ya ukweli (yawe mabaya au mazuri). Na hata kama unapenda kutoa mabaya tu, basi toa hayo mabaya kwa ufasaha, ukiweka ukweli tu badala ya kuweka tungo tata ambazo zinaweza zikatoa maana nyingine.

Jinsi ulivyoandika hapo, ungekuwa mwandishi wa historia kama yule jamaa yetu, kitabu chako kingekuja kuonesha kama vile Nyerere alikuwa anawakamata watu na kuwatupia sehemu zenye wanyama akiwa na makusudi kabisa kuwa watu hao waliwe.

Nakuomba ufanye utafiti, nenda mikoani, katembelee sehemu mbalimbali ambazo vijiji vya ujamaa viliulindwa, na maeneo yaliyofanyiwa "operesheni sogea". Kafanye bila bias.

Utagundua kuwa nia ya Nyerere ilikuwa ni kuongeza productivity, na kusogeza huduma za jamii kama shule na hospitali kwa kaya ambazo kabla ya hapo zilikuwa zinakaa mbali mbali sana. Kuna baadhi ya miji midogo hadi sasa inandelea kukua vizuri, lakini ilianzishwa kwa operesheni sogea. Na kuna sehemu ambazo wananchi walikuwa wabishi, waligoma kusogea au kwenda kwenye vijiji vya ujamaa, sehemu hizo mpaka sasa bado ziko duni, na vijiji vyao vimekaa kienyeji zaidi.

Pia utakubali rohoni kwako kuwa Nyerere hakuwa kutoa amri kwa watendaji wake kwamba wawa "mistreat" raia hasa hilo suala la kuwatupa kwenye simba. Kama ambavyo humlaumu Kikwete kwa bomoa bomoa inayosimamiwa na waziri wake, basi hata nyerere huwezi kumlaumu kama ulivyofanya.

Lazima ufahamu pia zoezi lile la ujamaa villagisation lilikuwa sponsored na WB huku wakiwa wameagizwa na Western countries kuwa "lisifanikiwe" kwa sababu hawakutaka kuwepo na "socialist island" eneo hili. Kufanikiwa kwa lile zoezi kungeleta matatizo ya kuenea zaidi kwa ujamaa, kitu ambacho Western capitalists hawakutaka. Kulikuwa na "sabotage" kubwa ya lile zoezi ili nchi za magharibi zichukulie Tanzania kama mfano wa kushindwa ujamaa (Kama una marafiki Uingereza, wanaweza kukusaidia zaidi, kwasababu mwaka 2001 MI6 wali-declassify this information na kuwa accessible to the public. Walieleza jinsi nchi za magharibi zilivyo-conspire against Nyerere and his Ujamaa).

Nataka ufahamu pia kuwa yale unayofikiri umejielimisha mwenyewe kuhusu lile zoezi (labda kwa kujisomea au kusikiliza stories), sio yote ya kweli. Hata baadhi ya waandishi wazalendo walilishwa sumu hiyo hiyo na vitengo vya "disinformation and misinformation" vya CIA na MI6. Utakumbuka kuwa vyombo vya habari vya magharibi vili-document makusudi kuhusisha njaa ya 1974 na zoezi la ujamaa vijijini ilhali tatizo kubwa ilikuwa ukame na kupanda kwa mafuta duniani.

Sina uhakika na umri wako, lakini nina-assume utakumbuka ukame uliokumba nchi za kusini kuanzia malawi, Zimbabwe, Botswana, Zambia na Namibia miaka ya majuzi. Kama ulifuatilia kipindi kile, ndio Mugabe alikuwa anaanza ku-implement mambo yake ya land re-distribution. Kwa vile watu wa magharibi hawakupenda mambo ya Mugabe, muda wote walikuwa wanakazania (kwa makusudi) ku-report kuwa njaa ya zimbabwe ilitokana na siasa mbaya za Mugabe na walikuwa hawataki kugusia mambo ya ukame. Ukame ulikuwa unahusishwa na njaa ya nchi nyingine tu.

Kwa hiyo ndugu yangu, unaposoma na kusikiliza na kuandika, jitahidi kuwa makini. Kuna vingine unaweza ukaviamini kwa vile aliyeandika au kukusimulia anataka kweli wewe uamini hivyo.

I hope umenipata.

Kila la kheri!

Naongea nilichokishuhudia na sio kukisikia au kukisoma. Nilikuwepo, jee wewe ulikuwepo?
 
Kwanini tumfananishe nyerere na Mahatma Ghandhi? Mahatma Ghandhi hajawahi kuwa waziri mkuu wala Rais wa India.

Kwa hiyo wewe unaona achievement ya mtu ni cheo anachopata? Ndiyo type hizi hizi zinagombea uongozi Tanzania halafu watu wanakuuliza "umeshawahi kufanya kitu gani?" Unajibu "Mi nishakuwa Waziri, nishakuwa balozi, nishakuwa mkuu wa mkoa" hujajibu swali, ulifanya nini?

Ungeijua vizuri heshima ya Gandhi katika movement ya kugombea uhuru wala usingeweza kusema hayo.

Gandhi hakupata Nobel kwa sababu ya fitna za kisiasa tu, na waliokuja kupata Nobel ni wafuasi wake kina Dr. Martin Luther King Jr.
 
Mwalimu hakutunukiwa hiyo nishani ya Nobel kwasababu ya msimamo wake thabiti juu ya ukombozi wa bara la Africa; wazungu hawakupenda sana misimamo yake hasa aliposimama kidete dhidi ya Ian Smith alipojitangazia Uhuru kule Zimbabwe, kwa kumsaidia sana kwa hali na mali Mugabe na ZANU yake; pia msimamo wake dhidi ya makaburu wa Afrika Kusini na sera zao za ubaguzi zilimfanya MWALIMU atumie muda wake mwingi kuwasaidia wakina Oliver Tambo wakati huo na chama chao cha ANC. Harakati zote hizi za kumkomboa mwafrika hazikuwapendeza wazungu{ waswede wanaotoa Nobel] kwani nyuma ya pazia walikuwa ni supporters wakubwa wa APARTHEID!!
 
Back
Top Bottom