Nyerere give us a break...Tshs 4 Millions cannot build 2 classrooms..........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Nyerere asimamisha ujenzi wa shule


na Mwandishi wetu, Musoma


amka2.gif
MBUNGE wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere, amesimamisha ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyasho baada ya ujenzi huo kuendeshwa bila mtaalamu anayetambulika kisheria.
Akiwa katika shule hiyo, Nyerere alisema kuendelea kuruhusu kujengwa kwa darasa hilo ni kukaribisha maafa ambayo yanaweza kutokea kwa wanafunzi watakaolitumia jengo hilo huku watu wachache wakiendelea kunufaika kwa udanganyifu wanaoufanya katika ujenzi, ili kutumia fedha za umma vibaya.
Nyerere ambaye alikuwa amefuatana na kamati yake ya kutembelea shule mbalimbali za jimbo hilo, alisema ana taarifa kuwa shule hiyo imepewa sh milioni nne kwa majengo mawili, lakini katika shule hiyo ni jengo moja linaloonekana.
“Ninachokielewa katika ujenzi wa majengo ya shule hii yanatakiwa kuwa mawili sasa jengo lingine liko wapi mbona linaonekana moja? Je fedha za jengo lingine zipo?” aliuliza mbunge huyo.
Kutokana na hali hiyo, Nyerere alimwagiza Mtendaji wa Kata ya Nyasho, Everist Tiginga, kuhakikisha sh milioni mbili zilizosalia zinapatikana, ili zitumike katika kutengeneza madawati ambayo yatasaidia wanafunzi watakaojiunga katika shule hiyo.
 
hiyo ni shule ya makuti na nyasi au ni aje/ yani mil 4 kwa madarasa 2 hapa kazi bado ipo
 
Sasa nyinyi mnabisha kuwa Sh 4 mil zinaweza kujenga darasa jamani?Wenzenu huko wamefanya upembuzi yakinifu na hizo ndo hesabu walizokuja nazo na pesa wamekabidhiwa kuanza ujenzi...au mnafikiri hesabu zimetoka hewani?So ndo maana hata mbunge wao hajasema
pesa kidogo anajua kuwa inawezekana tu kukamilisha ujenzi kwa mil 4.Mimi na wewe tusubiri tuone ni majengo ya namna gani hayo ya milioni 4.
 
Back
Top Bottom