Nyerere alitoa wapi uwezo ule?

Nyerere alitoa wapi uwezo ule?

Misingi ilishakuwa mibovu, nchi ilikuwa ni sawa na maiti, vipi alitegemea miujiza ya kufufua wafu?

Soma Hapa:
Natamani Kuifunga Jela Mifupa Yake.

Naona malalamiko ni mengi kuliko mapendekezo yeyote ya kutupatia maendeleo..Umekuwa good at criticizing, bila ku-advice mbinu mbadala... Hawa viongozi wetu waliojaribu kuja na vitu vipya, wameiacha nchi iko unstructured kiuchumi..
 
Ni kweli huyasemayo, maana hata akili imechoka kufikiri kwa madhira tulio pata.

Yaani choka mbaya.
 
Sera zake mbovu alizo siasisi ndio zimeimaliza nchi hii. Aliposhindwa baada ya kutawala zaidi ya miaka ishirini na kushuhudia kila kitu kikishindwa na maji yapo shingoni, yanakaribia kuingia mdomoni, kiujanja ujanja na kiutu uzima akaamua kutoroka uongozi, ndio akamtupia Mwinyi kwa kusingizia kuwa anan'gatuka mapema...!

Ndugu yangu X-PASTER unajua sisi ndiyo nchi pekee East Africa kujega university yetu. Hiyo university of Nairobi na Makere walijenga wazungu. Sasa uliza nani alijenga UDSM? Leo hii wewe umefaidika na matunda ya Nyerere kwa kusoma hadi chuo kikuu halafu unasema sera zake mbovu? Kweli shukurani za punda ni mateke.

Sasa ngoja turudi kwenye historia ya Tanganyika ili uelewe kwanini mwalimu alianzisha hizo sera zake. kumbuka Tanganyika ilikuwa ni koloni la wajerumani, Kama unavyojua koloni ni kama kuwa na mtoto wa kumzaa inabidi umlee. Uthibitisho huu upe hadi leo jinsi wajerumani walivyowekeza Tanganyika (hapa ieleweke sitetei unyonya wao) kama reli, Boma, shule, barabara, mashamba ya mkonge na miji mbalimbali.

Baada ya vita kuu ya kwanza Muingereza, alituchukua kama yatima, na utaona hakuwekeza zaidi ya kujenga vijumba vya uzunguni, hakufanya kitu cha maana kama ujenzi wa reli ya kati ya Mjerumani.

kwa hiyo nchi yetu haikuwa na kitu wakati Mwalimu anaichukua, ilibidi aijenge upya, ndiyo maana alianzisha sera zake za watu, siasa safi na uongozi bora. Katika watu aliwekeza kwenye elimu. Mimi sikubahatika kusoma kipindi hicho cha elimu bure kwasabau sikuwa nimezaliwa lakini wazazi wangu na ndugu zangu wengi walisoma bure.

Kwasababu ya elimu bure waliweza kusoma na hatimaye hata watoto wao (sisi) tumeweza kufika hapa tulipo kwasababu ya mbegu aliyoipanda Mwalimu miaka hiyo ambayo tulikuwa hatujazaliwa. Hiyo ndiyo dira au sera za mtu mwenye uelewa kama wa Mwalimu kuweka msingi ambao matokeo yake yanasaidia kizazi hata cha tatu na cha nne.

Sasa X-PASTER labda sema tuu unataka kuchokoza watu hapa lakini najua unaelewa nichokisema hapa.

Tanzania ni kubwa kulinganisha majirani zetu. Ili kujenga nchi kubwa kama yetu ilibidi mwalimu aondoe ukabila, sasa najua hili hatulioni kama ni faida lakini mimi nimewaona wakenya wengi ambao badala ya kuongea vizuri kama Wakenya wao wanaangaliana kwa makabila. Yaani unakuta Mkenya yuko radhi aongee na Mtanzania kuliko Mkenya mwenzake eti kwasababu anatoka kabila tofauti. Sasa utaniambiaje sera zake zilikuwa mbovu? Wewe hapo unabonga kiswahili kama huna akilia nzuri sasa unafikiri isingekuwa Mwalimu ungeweza kujidai hivyo?

Mi nafikiri wewe na wengi mnaomponda Mwalimu hamuelewe kitu kidogo kinachoitwa msingi. Nyerere aweka msingi mkubwa ila hao waliomfuata waliharibu kila kitu.

Hayo mambo ya kupanga foleni ni kutokana na njaa iliyokumba ukanda wetu (1975) na matatizo ya mafuta yaliyosababishwa na kutokuelewana kati ya waisraeli na warabu. kabla ya hapo uchumi wetu ulikuwa mzuri tuu na madini yetu yalikuwa salama.

Pia kumbuka kuwa wamagharibi walihakikisha ujamaa haufanikiwi (vita vya baridi) kwasababu kufanikiwa kwake kungeleta ushawishi mkubwa katika bara letu kwa hiyo walihakikisha kiuchumi hatufanikiwi. Hata hivyo tulikuwa na viwanda vyetu kama bora, na bidhaa nyingi za made in Tanzania. Chakushangaza sasa hivi watu wanaona ufahari kuvaa Gucci feki eti ruksa aaaaH inakera.

Nchi haipimwi maendeleo kwa watu kumiliki vigari vya mkopo kutoka dubai kama tunavyo danganywa na viongozi wetu bali itaendelea kama itazalisha; iwe tekinolojia, mawazo, bidhaa, nishati n.k na kuuza nchi nyingine na hapo itaweza ingiza fedha za kigeni ambazo zikaingia kwenye mzunguko na kuleta maendeleo. Sio kuchapisha mapesa yasiyo na thamani, yanayo jaa bila ya kuzalisha kitu. Upo mkuu?

Nitaishia hapa kwa leo.
 
Are you serious mkuu!?

Mkuu nimekuliza kwani inasikitisha saana pale ambapo unakataa japo unaelewa vyema mchango huyu mzee alifanyia Taifa hili, kwa miaka hiyo ishirini aliweza kujenga/kuanzisha viwanda na mashirika zaidi ya 300. Sasa kinachonisikitisha ni unaposema mashirika aliyoanzisha yalikufa akiwa madarakani. Ndio sikatai matatizo ya kiutawala yaliyokuwepo katika uendehsji wa hayo mashirika ambayo mengi kwa sasa ni marehemu na kuingiliwa na chama, lakini mpaka Nyerere anaondoka mashirika aliyoanzisha yalikuwa yanafanya kazi
Labda nikupe changamoto; Je kipindi cha Mzee Mwinyi aliweza kufufua na kuanzisha mashirika mangapi? Pili na Mkapa aliweza fufua na kuanzisha mangapi kwa kipindi alicho kaa madarakani miaka kumi

Mkuu hata kama unamchukia Nyerere ni vema ukadhamini walau hata mchango wake ambao naamini hata kaa atokee kiongozi atakeyevunja record yake.
 
Chamoto

Kuna watu hata hawajui University ni nini si unajua waliogopa umande. Mbona unawakweza sana hawa malofa?
 
Ndugu yangu X-PASTER unajua sisi ndiyo nchi pekee East Africa kujega university yetu. Hiyo university of Nairobi na Makere walijenga wazungu. Sasa uliza nani alijenga UDSM? Leo hii wewe umefaidika na matunda ya Nyerere kwa kusoma hadi chuo kikuu halafu unasema sera zake mbovu? Kweli shukurani za punda ni mateke.

Kusoma kwa tabu mpaka chuo kikuu, hakunifanyi mimi kuyafurahia yale ambayo hayakufaa kuwepo kwenye siyasa za nchi hii.

Sasa ngoja turudi kwenye historia ya Tanganyika ili uelewe kwanini mwalimu alianzisha hizo sera zake. kumbuka Tanganyika ilikuwa ni koloni la wajerumani, Kama unavyojua koloni ni kama kuwa na mtoto wa kumzaa inabidi umlee. Uthibitisho huu upe hadi leo jinsi wajerumani walivyowekeza Tanganyika (hapa ieleweke sitetei unyonya wao) kama reli, Boma, shule, barabara, mashamba ya mkonge na miji mbalimbali.

Baada ya vita kuu ya kwanza Muingereza, alituchukua kama yatima, na utaona hakuwekeza zaidi ya kujenga vijumba vya uzunguni, hakufanya kitu cha maana kama ujenzi wa reli ya kati ya Mjerumani.

kwa hiyo nchi yetu haikuwa na kitu wakati Mwalimu anaichukua, ilibidi aijenge upya, ndiyo maana alianzisha sera zake za watu, siasa safi na uongozi bora. Katika watu aliwekeza kwenye elimu. Mimi sikubahatika kusoma kipindi hicho cha elimu bure kwasabau sikuwa nimezaliwa lakini wazazi wangu na ndugu zangu wengi walisoma bure.

Kwasababu ya elimu bure waliweza kusoma na hatimaye hata watoto wao (sisi) tumeweza kufika hapa tulipo kwasababu ya mbegu aliyoipanda Mwalimu miaka hiyo ambayo tulikuwa hatujazaliwa. Hiyo ndiyo dira au sera za mtu mwenye uelewa kama wa Mwalimu kuweka msingi ambao matokeo yake yanasaidia kizazi hata cha tatu na cha nne.

Sasa X-PASTER labda sema tuu unataka kuchokoza watu hapa lakini najua unaelewa nichokisema hapa.

Nakuelewa sana, kuliko unavyo fikiria, enzi za Nyerere ukuwepo na yale hayajakukuta. Hizo sera za UPE ndio zilizo ua elimu ya Watanzania wengi.

Tanzania ni kubwa kulinganisha majirani zetu. Ili kujenga nchi kubwa kama yetu ilibidi mwalimu aondoe ukabila, sasa najua hili hatulioni kama ni faida lakini mimi nimewaona wakenya wengi ambao badala ya kuongea vizuri kama Wakenya wao wanaangaliana kwa makabila. Yaani unakuta Mkenya yuko radhi aongee na Mtanzania kuliko Mkenya mwenzake eti kwasababu anatoka kabila tofauti. Sasa utaniambiaje sera zake zilikuwa mbovu? Wewe hapo unabonga kiswahili kama huna akilia nzuri sasa unafikiri isingekuwa Mwalimu ungeweza kujidai hivyo?
Nyerere hakuondoa ukabila Tanganyika wala Baada ya kubadilisha jina la nchi na kuitwa Tanzania...! Kama Tanganyika au Tanzania kulikuwa na ukabila, ni vipi Kinjeketile Ngwale ambaye alikuwa kabila la Mmatumbi, aliweza kuwaunganisha Wangoni, Wangindo na makabila mengine ya kusini mwa Tanganyika kupigana na Mjerumani?

Inashangaza sana Kwa Mtemi Mirambo wa Unyanyembe, aliweza kuunda jeshi la Waruga ruga, ambalo lilikuwa na askari kutoka makabila ya mbali mbali, kama vile Wangoni, Wahehe na Wenyeji wa Tabora.

Nyerere aliondoa ukabila, ni ajabu Dar kipindi kile cha harakati za kugombea uhuru, alikuta watu tayari wamesha changanyika, kulikuwa na Wazaramo, Wamanyema na makabila mengine, akiwemo na yeye Mzanaki, soma historia ya TAA...!

Nyerere hakuondoa ukabila, Tanganyika kulikuwa hakuna ukabila.

Mi nafikiri wewe na wengi mnaomponda Mwalimu hamuelewe kitu kidogo kinachoitwa msingi. Nyerere aweka msingi mkubwa ila hao waliomfuata waliharibu kila kitu.

Hayo mambo ya kupanga foleni ni kutokana na njaa iliyokumba ukanda wetu (1975) na matatizo ya mafuta yaliyosababishwa na kutokuelewana kati ya waisraeli na warabu. kabla ya hapo uchumi wetu ulikuwa mzuri tuu na madini yetu yalikuwa salama....

Nitaishia hapa kwa leo.
Misingi aliyoweka Nyerere ilikuwa mibovu, na ndio maana mpaka leo Tanzania inashindwa kusimama yenyewe kwa kuwa na misingi ambayo si imara. Alishindwa ndio maana akang'atuka baada ya kutawala hii nchi kwa miaka 24.

Kura tulikuwa tunapiga kwa kumchagua yeye peke yake, yaani Nyerere VS Kivuli

Ukitiki kwenye kibox cha Hapana, wanasema kuwa ni sawa sawa maana hapana mwingine ila yeye, ukitiki kwenye Ndio, wanasema Ndio yeye huyu huyu hakuna mwingine.
 
Kusoma kwa tabu mpaka chuo kikuu, hakunifanyi mimi kuyafurahia yale ambayo hayakufaa kuwepo kwenye siyasa za nchi hii.

Sasa ulitegemea elimu iwerahisi ndugu? Hebu niambie ni wapi kuna elimu rahisi? Hata nchi za dunia ya kwanza elimu siyo rahisi. Moja ya zao la kuelimika ni kujifunza kuwa na nidhamu kwahiyo mazingira ya mwanafunzi yanakuwa naugumu fulani hivi ili kumfanya anayesoma aweze kutumia akili yake zaidi kutatua matatizo.

Nakuelewa sana, kuliko unavyo fikiria, enzi za Nyerere ukuwepo na yale hayajakukuta. Hizo sera za UPE ndio zilizo ua elimu ya Watanzania wengi.

Sasa kama sera za upe hazikuwa nzuri kwanini waliojua kusoma na kuandika walikuwa zaidi ya 90%.

Nyerere hakuondoa ukabila Tanganyika wala Baada ya kubadilisha jina la nchi na kuitwa Tanzania...! Kama Tanganyika au Tanzania kulikuwa na ukabila, ni vipi Kinjeketile Ngwale ambaye alikuwa kabila la Mmatumbi, aliweza kuwaunganisha Wangoni, Wangindo na makabila mengine ya kusini mwa Tanganyika kupigana na Mjerumani?

Inashangaza sana Kwa Mtemi Mirambo wa Unyanyembe, aliweza kuunda jeshi la Waruga ruga, ambalo lilikuwa na askari kutoka makabila ya mbali mbali, kama vile Wangoni, Wahehe na Wenyeji wa Tabora.

Nyerere aliondoa ukabila, ni ajabu Dar kipindi kile cha harakati za kugombea uhuru, alikuta watu tayari wamesha changanyika, kulikuwa na Wazaramo, Wamanyema na makabila mengine, akiwemo na yeye Mzanaki, soma historia ya TAA...!

Nyerere hakuondoa ukabila, Tanganyika kulikuwa hakuna ukabila.

Nirahisi kukusanya watu wa eneo fulani (ambao wanaishi mazingira/utamaduni unaofanana) kuliko kumchukua Mmakonde na Mhaya na kuwaambia ninyi ni wammoja, wapi na wapi bwana. Kwahiyo hapo bado naamini kuwa Mwalimu alihusika kutuunganisha. usivione vyaelea, vimeundwa, X-PASTER

Misingi aliyoweka Nyerere ilikuwa mibovu, na ndio maana mpaka leo Tanzania inashindwa kusimama yenyewe kwa kuwa na misingi ambayo si imara. Alishindwa ndio maana akang'atuka baada ya kutawala hii nchi kwa miaka 24.

Nyerere kama binadamu alikosea mengi tuu lakini kuna mazuri aliyoyafanya. Mimi nafikiri sasa hivi Tanzania ndiyo inashindwa kusimama yenyewe, hatuna sera kabisa kama Taifa.kipindi cha Nyerere Tanzania ilijulikana msimamo wake, mfano kusitisha uchimbaji wa madini hadi hapo Tanzania itakapo kuwa na wataalamu wa kutosha wenye uelewe wa kulinda rasilimali zao.

Kura tulikuwa tunapiga kwa kumchagua yeye peke yake, yaani Nyerere VS Kivuli

Ukitiki kwenye kibox cha Hapana, wanasema kuwa ni sawa sawa maana hapana mwingine ila yeye, ukitiki kwenye Ndio, wanasema Ndio yeye huyu huyu hakuna mwingine.

Hapa hata mimi nakubali haikuwa haki na nikama udiktekta fulani hivi na hulo lilikuwa ni kosa la Mwalimu kujipa nguvu kubwa ya kuchanguliwa.
 
Nilidhani watanganyika wamesha amka ,lakini MMMM,,,,,,Hadi leo munadumisha fikra za mualimu?.

Kaazi kwelikweli.
 
Chamoto

Kuna watu hata hawajui University ni nini si unajua waliogopa umande. Mbona unawakweza sana hawa malofa?
X-PASTER ni msomi na anaelewa sana mambo aliyoyafanya Nyerere sema tuu nameamua kuamini anavyoamini yeye.
 
Mwalimu Nyerere au Baba wa Taifa alikuwa na mapungufu yake kama kiongozi hata mwenyewe alishazungumzia hili la kuwa na mapungufu mara nyingi tu. Alikuwa msafi, alikuwa mcha Mungu pia, hakuwa na uroho wa utajiri wa haraka haraka kwa kutudhulumu Watanzania mali yetu kwa aina moja au nyingine au kujilimbikizia mshahara mkubwa kupita kiasi.

Hivyo sababu hizi ndizo zilizomfanya awe na uwezo wa kumkemea yoyote yule bila ya kumuogopa. Pamoja na kuwa aling'atuka miaka mingi sana lakini alijijengea sifa kubwa katika nchi mbali mbali za Afrika na dunia nzima na ndiyo maana hadi hii leo ukikutana mtu wa kutoka mojawapo ya nchi za Afrika au hata duniani na akifahamu unatoka Tanzania na anajua machache kuhusu Tanzania basi atakuuliza kuhusu Nyerere (hatakuuliza kuhusu Mwinyi, Mkapa wala Kikwete)

RIP Mwalimu.
 
Pamoja na mambo mengi kwenda ndivyo sivyo hapa TZ lakini hakuna Kiongozi yoyote wa zamani mwenye uwezo wa kukemea nchi isiangamie, nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini? Nimepata jibu kwamba japo hakuna mtu mkamilifu kabisa 100% lakini Mwalimu Nyerere alikuwa mtu safi ndio mana hakuogopa kusema pale alipoona ndivyo sivyo.

Ari hiyo hakuna aliyenayo sasa kwani kila mmoja akijaribu anaogopa kuambiwa mbona na wewe......................................................

Wana JF kweli si kweli? kama si kweli nani anaweza kuvaa kofia ya Mwalimu Nyerere?

Tatizo la kukuzwa huku ukikaririshwa fulani ni msafi na mjamaa. Hivi enzi hizo za Nyerere ,nania likua na ubavu wa kuikosoa serikali? ,unadhani hisi chatroom na hizi blogla na utandawzi na uhuru wa leo ulikuwepo enzi hizo? unajua kuwekwa kizuizini wewe?
 
[BILA RUSHWA..HAKI HAIPATIKANI....TOA RUSHWA UPATE HAKI.....(?)
RUSHWA NA TANZANIA DAM-DAM.....!
TAASISI IPI RUSHWA KWAO MWIKO?
NASEMA KWA KUWA YAMENIKUTA......!

Nimeipenda hii!

Tatizo la kukuzwa huku ukikaririshwa fulani ni msafi na mjamaa. Hivi enzi hizo za Nyerere ,nania likua na ubavu wa kuikosoa serikali? ,unadhani hisi chatroom na hizi blogla na utandawzi na uhuru wa leo ulikuwepo enzi hizo? unajua kuwekwa kizuizini wewe?

Hata mbuyu uliota kama mchicha kwanza.
 
Mwalimu Nyerere alikuwa na mchango mkubwa sana katika kuijenga Tanzania na Afrika. Hilo halibezwi. Lakini Mwalimu alikuwa na mapungufu yake. Tusifikie mahali tukamwabudu.

Wale wanaodhani kuwa ubadhirifu/ufisadi ulianza baada ya Mwalimu kuondoka madarakani ni wale ambao walikuwa bado ni watoto wakati huo. Wangapi kati yenu wanakumbuka kuhusu kitu kinaitwa Party Supremacy? Wakati ule TANU/CCM walikuwa wanachota pesa pale Treasury na hakuna kuulizwa. Sisemi kuwa Nyerere alikuwa anafaidika na hizo pesa lakini waliokuwa chini yake walikuwa wanatumia vibaya hizo pesa. Wale waliokuwa wanajaribu angalau kuuuliza ni kwa nini hayo yalikuwa yanatendeka waliadabishwa. Jibu lilikuwa Chama hakijadiliwi nje ya chama. TANU/CCM hawakukaguliwa walivyotumia hayo mapesa ambayo walikuwa wanachota pale Treasury - Chama hakijadiliwi nje ya Chama. Miaka ya mwishoni kuna pesa zilichotwa pale Treasury kuanzisha SUKITA ambayo leo hii haipo. SUKITA walikuwa wanaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi Tax-Free.

Kuhusu Nyerere kuthamini elimu mimi nakubaliana kwa kiasi fulani tu japo kuwa nachanganyikiwa kidogo. Wakati tunapata uhuru Tanu Youth League walikuwa wanaimba wimbo huu: "Akina Yes Yes Wadai Mishahara. Nyerere Fungua Majela Wafungwe. Wanaopinga TANU.....". Wakati wa enzi zile watu wengi walikuwa wanaamini kabisa kuwa Nyerere alikuwa anawaogopa wasomi. Nyerere alisema elimu Tanzania itolewe mpaka level ya Primary School. Wachache waende form four, wachache Form six, na wachache sana ambao wangekuwa viongozi waende Chuo kikuu (UDSM). Soma kitabu chake kuhusu elimu-nimesahau jina lake. Matokeo yake leo ni nchi ya mwsho kwa kuwa na wasomi waliomaliza Sekondari au Chuo kikuu.

Kuhusu kujenga vyuo vikuu Nyerere alikuwa na uchungu wa kuwa na chuo kikuu chetu wenyewe. Lakini tukumbuke michango ya watu kama akina Oscar Kambona. Yeye alipelekwa Ulaya kusoma akataka kusomea sheria na ilimshinda. Alipata usongo na kuamua pamoja na Mwalimu kuanzisha Dar es salaam University College with Faculty of Law as the first Faculty. Chuo kikuu kilianzia pale Lumumba. Majengo unayoyaona pale mlimani yana historia ya wafadhili kadhaa. Hall 2 na 5 yalijengwa na USA (John Kennedy ), Hall 1 and 4 and probably 6 waingereza, Faculty of Arts (UK), unaweza kutafuta wengine kwa majengo yaliyobaki.

Kuna kitu kingine ambacho kinanikera kila wakati. Kupenda sana kuwa na mashirika ya umma, kama ATC. Sisi ambao tumeona tokea wakati yanaanzishwa mpaka yanakufa tunaomba mtuache tufe kwanza halafu muanzishe huko nyuma. Sitaki kurudia enzi za kuomba simu kwa muda wa miaka 10! na ukifungiwa technician anafanya ni mradi wake kila siku anachomoa waya na kukujia kukuomba pesa afix. Sipendi kupata sukari, sabuni, mabati, n.k. kwa mgao pale kwa kitongoji. Nimeshuhudia toka kuchukuliwa COSATA na kuwa STC (State Trading Corporation au saidia Tujenge Chetu - a mammoth supermarket indeed). STC iliwashinda wakati wa Werner Kapinga akapelekwa NMC. STC ikagwanyika kwenda mashirika mengi kama DABCO, HOSCO, AISCo, BHESCO, RTCs, etc. Waliofanya kazi huko walikuwa miungu watu. Enzi za hali ngumu nilishuhudia HOSCO (au DABCO) wakiwa na duka pale karibu na Askari monument wakiuza Freezer moja kwa shiling laki 3.Pesa nyingi sana wakti huo kwani mshahara wa JKN ulikuwa Shs elfu tano? Duka zima lilikuwa na hilo freezer moja tu!
 
Kwanza huyo Nyerere hakuwa na hata haya kutetea uongo ufanane na kweli. Alidai anawachukia makaburu, na hali alikuwa anajuwa kabisa, tulikuwa tunawauzia tumbaku, na wao wanatuuzia Land Rover, hata zile almasi za Mwadui wana hisa kubwa tu...!

Nje kwenye vyombo vya habari alijionyesha kama mpenda haki na mpigania uhuru, lakini kwa ndani alikuwa akifanya kinyume chake.

Nyerere ndani ya nafsi yake alijua kabisa kuwa yeye si mpigania haki, kwa sababu aliwanyima Watanzania haki ya kuyatoa mawazo yao.

Hivi wale wote leo wenye kuweza kupanua vinywa vyao na kuwasema viongozi wa serikali na chama tawala, enzi ya Mchonga wangethubutu?

Ndivyo alivyofanya Nyerere, na kuna watu watakuja hapa na kudai kuwa Nyerere alikuwa ni mzalendo.

Enzi hizo uzalendo ni kuwaweka watu kizuizini na kutunga sheria ya kuwashitaki wakati wako kizuizini.
 
Mi naomba nikupongeze kwa mchango mzuri. Mimi mtu kama X-plastaz huwa na shindwa kumwelewa na sina hakika kama amesoma na kuijua vilivyo historia ya nchi yake vizuri. Nampa changamoto moja then next time akija kwenye jukwaa la wasomi kama hili aje akiwa timamu. nakuomba X-plastaz kasome essays on socialism and Education for self reliance. Ndo utajua kama Mwl. aliweka misingi mibovu ama la, matatizo tulionayo leo yameletwa na baadhi ya watu wenye mawazo finyi kama yako,walio shirikiana na wazungu.
 
Muache huyu ndugu aendelee kulaumu lakini bado hajasema ni nani anaweza kukaribia mambo ya Mwalimu mfano ''azimio la Arusha lilikuwa azimio la misingi ya utu na haki'' au hata hili halijui?
 
Alikuwa muadilifu, ni kama Dr. W. Slaa ni muadilifu na ndo maana haogopi kusema.
 
Si kwamba alikuwa shupavu bali uwezo ule ulitokana na kwamba alikuwa akitawala wafu.Waliokuwa hai walikuwa waoga sana.
Mashujaa ni maraisi waliomfuatia.Ukomo wa ushupavu uko kwa Kikwete.
Kwa mtindo wake ule wa kutawala kuwafanya raia hata mawaziri wake kama watoto kwa kuwakaripia kama mbuzi na kulazimisha analolitaka yeye;angekuwepo leo angekuwa akizomewa kila anapopita na angekwishasababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Tungemwambia acha mfumo kristo!,Angejifanya haambiliki akawafunga masheikh wote.Tungeingia mitaani.
 
Back
Top Bottom