Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,152
- 10,862
Kwanza huyo Nyerere hakuwa na hata haya kutetea uongo ufanane na kweli. Alidai anawachukia makaburu, na hali alikuwa anajuwa kabisa, tulikuwa tunawauzia tumbaku, na wao wanatuuzia Land Rover, hata zile almasi za Mwadui wana hisa kubwa tu...!
Nje kwenye vyombo vya habari alijionyesha kama mpenda haki na mpigania uhuru, lakini kwa ndani alikuwa akifanya kinyume chake.
Nyerere ndani ya nafsi yake alijua kabisa kuwa yeye si mpigania haki, kwa sababu aliwanyima Watanzania haki ya kuyatoa mawazo yao.
Hivi wale wote leo wenye kuweza kupanua vinywa vyao na kuwasema viongozi wa serikali na chama tawala, enzi ya Mchonga wangethubutu?
Ndivyo alivyofanya Nyerere, na kuna watu watakuja hapa na kudai kuwa Nyerere alikuwa ni mzalendo.
Enzi hizo uzalendo ni kuwaweka watu kizuizini na kutunga sheria ya kuwashitaki wakati wako kizuizini.
X-paster uliyashuhudia haya,achana na hawa waliosimuliwa makanisani mwao.
Kwenye hadhara akisema udini mbaya lakini akiwa ikulu hujisifu kwa kusema sikumchagua huyu kuwa waziri kutokana na uwezo wake katika siasa bali kutokana na imani yake (ukatoliki).