Nijibu hoja zako kwa aya moja tu. Nashukuru nitambua kuwa hukuwa na misingi ambayo ambayo kwayo Mwl Nyerere aliianzisha na sasa inadunisha maendeleo yetu. Ninchokiona unataja baadhi ya matukio yaliyofanywa na baadhi ya maraisi waliofuata tena waislamu na kusema wamefanya vizuri. Kwa taarifa yako marais wote hawa wanatekeleza mpango wa taifa ulioasisiwa na Mwl Nyerere. Kabla ya kuuhishwa miaka ya 1990 ulisomwa na Mzee Kingunge pale Kizota mwaka 1987. Huo ulikuwa mpango wa miaka 15. Wakati huo Mwl Nyerere alikuwa mwenyekiti wa ccm. Baada ya mwenye kuweka msingi wa uendeshaji uchumi; Mh Mkapa aliimarisha uchumi mkubwa na kuuanza mkakati wa kutengeneza barabara kwa kauli mbiu kutoka Dar-Kagera kwa taxi au wengine walikoleza bajaji. Muda uliisha akiwa kamalizaa daraja la Mkapa. Mh Kikwete hakuwa na kingine ni kumalizia barabara zilizoachwa atake asitake. Kama unakumbuka alianza kwa kusuasua mpaka serikali ikawa inalipa faini kwa kutokupeleka pesa. Mh Kikwete baada ya matokeo magumu 2010 ndipo alipojitenga na wanamtandao wake na kumrudisha Mh Magufuli kwenye ujenzi huku wakimzuia baadhi ya maamuzi kama vile swala la uzito wa malori. Haya yote yanafanywa kwenye misingi aliyoiweka Mwl Nyerere kwa viongozi kubadilishana kwa amani na kutekeleza mpango wa maendeleo.Hizo barabara zote unazozisema zilijengwa na makampuni ya nje na 90% hazikujengwa wakati wa Nyerere.
Kikwete ndiye aliyefanya mapinduzi ya barabara Tanzania.
Wakati wa Nyerere hata Dar mjini kulijaa mahandaki na tulizikuta na lami walivyotuachia wakoloni.
Hivi uliziona barabara za Dar alizowachiwa Mwinyi na Nyerere?
Nijibu hoja zako kwa aya moja tu. Nashukuru nitambua kuwa hukuwa na misingi ambayo ambayo kwayo Mwl Nyerere aliianzisha na sasa inadunisha maendeleo yetu. Ninchokiona unataja baadhi ya matukio yaliyofanywa na baadhi ya maraisi waliofuata tena waislamu na kusema wamefanya vizuri. Kwa taarifa yako marais wote hawa wanatekeleza mpango wa taifa ulioasisiwa na Mwl Nyerere. Kabla ya kuuhishwa miaka ya 1990 ulisomwa na Mzee Kingunge pale Kizota mwaka 1987. Huo ulikuwa mpango wa miaka 15. Wakati huo Mwl Nyerere alikuwa mwenyekiti wa ccm. Baada ya mwenye kuweka msingi wa uendeshaji uchumi; Mh Mkapa aliimarisha uchumi mkubwa na kuuanza mkakati wa kutengeneza barabara kwa kauli mbiu kutoka Dar-Kagera kwa taxi au wengine walikoleza bajaji. Muda uliisha akiwa kamalizaa daraja la Mkapa. Mh Kikwete hakuwa na kingine ni kumalizia barabara zilizoachwa atake asitake. Kama unakumbuka alianza kwa kusuasua mpaka serikali ikawa inalipa faini kwa kutokupeleka pesa. Mh Kikwete baada ya matokeo magumu 2010 ndipo alipojitenga na wanamtandao wake na kumrudisha Mh Magufuli kwenye ujenzi huku wakimzuia baadhi ya maamuzi kama vile swala la uzito wa malori. Haya yote yanafanywa kwenye misingi aliyoiweka Mwl Nyerere kwa viongozi kubadilishana kwa amani na kutekeleza mpango wa maendeleo.
Sasa msikiti unaingiaje hapo, jadilini hoja tu. Mie mwenyewe naamini nyerere katuchelewesha sana. Kwanza aling'atuka baada yakuona mambo yamemzidi, wakati anaondoka mashirika yote yalikuwa icu. Halafu kwann mnaksirika sana nyerere akisemwa! Kwani yeye nani? Alifeli, tena alifeli sana tu.Hivi unafikiri kuongoza nchi ni sawa na kuongoza huo msikiti wako?
Kama msikiti umewashinda mpaka mnahamasisha watu kupiga risasi mapadre itakuwa nchi.
Ujamaa na kujitegemea ndio lengo kuu na limewekwa kwenye katiba 1977. Kumekuwa na hatua mbalimbali za kufikia lengo hilo ambalo lilianza 1967. Moja ya mipango mifupi ni kuunda vijiji vya ujamaa mpaka 1975 zoezi lilikamilika na watu walikuwa kwenye vijiji vya ujamaa. Mabadiliko yoyote huwa na changamoto zake na zilikabiliwa na huo nao ni msingi wa kuimarisha umoja wa Watanzania. Watu walipata huduma za jamii kwa pamoja kama vile shule maji na zahanati. Mliokaririshwa ubaya wa zoezi hili ndio mnaimba kama kasuku ubaya. Tuliobeba mizigo kwenda kwenye vijiji tunaihisi raha ya kushirikiana huko vijijini na kuwa karibu na huduma.Mpango wa Taifa ulikuwa ujamaa na kujitegemea.
Kuhamisha watu kupeleka vijiji vya ujamaa. Haukuwa na tija.
Marais wote waliofata baada yake hawakuufata, amma kwa kuuona haukufaa au kwa kulazimishwa na wafadhili?
Jibu ulete wewe mwenye kuujuwa mpango zaidi ya huo.
Mungu akusamehe bure tu, umri! ila misingi unayoiona sasa ujue pia imewekwa, hakuna asiyefanya kosa, jitazame kwanza mwenyewe utajua ni makosa mangapi uliyoyatenda ndani ya familia yako tu, halafu hukumu.Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.
Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?
Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?
Tujadili.
Halafu kujua hili ni kosa ni mtazamo tu wa mtu. Kosa ambalo wewe unaona Mwl Nyerere alilitenda mimi naweza nisilione kwani huenda lilinisaidia. Hatimaye tunajikuta tunalazimika kuomba mchakato wa kumtanganza kuwa mtakatifu uharakishwe.Namuomba Mungu anioneshe tukio hilo.Mungu akusamehe bure tu, umri! ila misingi unayoiona sasa ujue pia imewekwa, hakuna asiyefanya kosa, jitazame kwanza mwenyewe utajua ni makosa mangapi uliyoyatenda ndani ya familia yako tu, halafu hukumu.
Kuna watu wamezaliwa UK na wamesomea msingi UK lakini ukisikiliza kiingereza chao kwa wewe na mimi tuliyekijua kwa kujifunza tunaweza kuziba masikio. Mtu anasema " We was" nadhani akiandika hapa FaizaFoxy utakuwa wa kwanza kumshambulia. kujua Lugha ama kutojua Lugha kifasaha siyo kua huna Elimu ama una elimu. Kama ulisomea Lugha na ukashindwa kuandika ama kuongea lugha vizuri ndiyo unaweza kumashambulia mtu. Watanzania tujifunze kuona mbali ya box. Hao wenye lugha hawana hata muda wa kumrekebisha mtu akichomekea kama tulivyo sisi. Ukikosoa mtu kosoa content ya alichokiandika siyo lugha ama spelling mistakes...Ukitaka kuwa mwalimu wa Lugha nafasi zipo nyingi sana katika shule zinazojiita English Medium......... Me sayKajifunze kuandika Kiingereza ndio uje nikuelewe una maanisha nini.
Huo ndio msingi uliowekwa na Nyerere. Hujuwi Kiingereza na nna uhakika hata Kiswahili hukijui.
Mama Obama,
Ni kweli Nyerere alifanya makosa ya msingi kama binadamu. Lakini wakati anaondoka madarakani aliacha miundo mbinu ya uchumi ambayo kama ingeendelezwa, nchi hii inagekuwa imepinga hatua kubwa ya maendeleo. Kwa mfano;
1. Miundo mbinu ya kifedha: wakatika anatoka madarakani aliacha benki ya NBC ikiwa kati ya benki 12 bora Africa nzima. Kati ya benki hizo, 6 zilikuwa za Africa ya kusini , 4 za Nigeria na 1 ya Ghana na NBC. Na benk zote zilizokuwepo hapa nchini zilikuwa zinaendeshwa na watanzania wenyewe.
2. Elimu: Kiwango cha kujua kusoma na kuandika kilikuwa juu kuliko nchi karibu zote za Africa- zaidi ya 90%, elimu iliyotolewa ilikuwa sawa kwa watu wote ( tajiri na maskini)
3. Mgawanyo wa Rasmali za taifa: tofanuti ya kipato kati ya tajiri na maskini ilikuwa kwa uwiano 1:9( soma kitabu cha miaka kumi baada ya azimio la Arusha);
4. Miundo mbinu ya kiuchumi: Kulikuwa na viwanda vinavyo jiaendesha na kulipa kodi zaidi ya 60% ya kodi iliyokuwa inakusanywa kati ya 1985 na 2000;
5. Kilimo kilikuwa mchangiaji mkuu wa uchumi wa taifa( GDP), hii ina maana kuwa watu waliokuwa wanajiari walikuwa wengi kuliko ilivyo sasa.
Watu kwa wakati huo walikuwa wanjitambua zaidi hata kulizo ilivyo sasa. Kosa lake liko wapi?
Tujifunze uzalendo wa kutolaum viongozi wetu
Ninachopingana nacho ni kitendo cha kumlaumu Nyerere kwa hali iliyopo sasa, sizungumzii wakati wa Nyerere. Ndio maana nashangaa kufeli kwa sasa kunahusiana vipi na utawala wa Nyerere uliopita zaidi ya miaka thelathini sasa?Mbona hata alivyokuwa madarakani nchi ilifeli kama ulikuwepo nadhani uliona au unaweza kutupa mafanikio ya Nyerere kiuchumi wakati yupo madarakani.
Jamaa alichemka saana ile kuomba radhi haikuapahali pakeNchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.
Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?
Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?
Tujadili.
Hakika nimenufaika kusoma ulichokiandika, umetiririka vyema kabisa, umejaribu kuonyesha "inconsistency" ya kukubali kwangu kuwa Nyerere alifanya makosa kama binadamu na ukashangazwa na nilivyomalizia kwa kuuliza amefanya makosa gani. Hoja yangu bado ipo palepale, makosa makubwa aliyoyafanya akiwa rais aliwahi kukiri hadharani kuyafanya na akayaombea msamaha. Baadhi ya makosa aliyoyafanya na kuyaombea msamaha hatupashwi kuendelea kuyashikiria.Kama binadamu Nyerere amefanya makosa, lakini mazuri aliyoyafanya ni mengi kushinda makosa. Na nimesema makosa aliyoyafanya hakufanya kwa faida yake mwenyewe, haswa kwa elimu yetu, alifikiri wakati huo ndiyo itatufaa sisi Watanzania kwa kujitegemea sisi wenyewe. Wakati wa utawala wa Nyerere kulikuwa na mvutano wa siasa za communist na capitalism na Nyerere alikuwa hataki kufungamana na upande wowote, kwa hiyo aliona siasa ya kujitegemea bila kutegemea mataifa mengine ni bora kwa Watanzania.
Nakubaliana na wewe kabisa elimu ya kiwango cha kusoma na kuandika kilikuwa kikubwa Africa nzima na uhuru wa Watanzania kulalamika kuhusu Viongozi wao ulikuwa mkubwa, na kwa wakati huo elimu yetu ilikuwa ikienda na wakati huo.
Mambo yamebadilika , na Viongozi waliochukuwa kutoka kwa Rais Nyerere walikuwa na nafasi ya kuimprove education yetu kwenda na Wakati, badala yake wakaididimiza elimu yetu, wakauza benki zetu na viwanda, NBC ilikuwa ni benki yangu, na hii ilimuuma sana Rais Nyerere Wakati iliuzwa kwa bei ya kutupa, benki AMBAYO ilikuwa ikiendeshwa na Watanzania wenyewe. Nimeeleza wazi kuwa viongozi waliofuatia walikuwa na chance ya kuimprove education yetu, badala yake wakaivuruga nchi na nchi nzima ikakosa nidhamu. Wakati wa Rais Nyerere uonevu kwa watu wa kawaida ulikuwa hausikiki., cheo ni dhamana, kila mala Viongozi wakikumbushwa. Ukitumia Mali ya umma kwa manufaa yako mwenyewe hautaendelea kulala kwenye nyumba ya Serikali. Mwalim alikuwa sio selfish, he had Tanzania at heart.
Nakubaliana na wewe, kulikuwa Hakuna tofauti kubwa kati ya masikini na matajiri na ulikuwa huwezi kujitajirisha kutumia Mali ya umma wazi wazi kama tunavyoona Viongozi wa leo. Vitendo wanavyofifanya Viongozi wa leo, wizi wa wazi wazi wa Mali za umma, na bado wako bungeni na wengine bamoja na record mbaya ya kutumia ama kuiba Mali za umma bado wanadhikila nafasi zao, na wengine wako bungeni wakiendelea kututungia sheria, Wakati wa Mwalimu isingetokea.
Umeanza na kusema ni kweli Rais Nyerere kama binadamu alifanya makosa, kisha ukamalizia amefanya makosa gani? Narudia tena, Rais Nyerere hakufanya makosa kwa kusudi ili ajinufaishe mwenyewe, uamuzi wote alioufanya wakati huo alifikiri ulikuwa wa kuwanufaisha Watanzania. Na hii inagusa elimu yetu, vijiji vya ujamaa, na kadharika.
Oh .. kumbe leo Ijumaa .. the day of rage!
Kajifunze kuandika Kiingereza ndio uje nikuelewe una maanisha nini.
Huo ndio msingi uliowekwa na Nyerere. Hujuwi Kiingereza na nna uhakika hata Kiswahili hukijui.
Ujamaa na kujitegemea ndio lengo kuu na limewekwa kwenye katiba 1977. Kumekuwa na hatua mbalimbali za kufikia lengo hilo ambalo lilianza 1967. Moja ya mipango mifupi ni kuunda vijiji vya ujamaa mpaka 1975 zoezi lilikamilika na watu walikuwa kwenye vijiji vya ujamaa. Mabadiliko yoyote huwa na changamoto zake na zilikabiliwa na huo nao ni msingi wa kuimarisha umoja wa Watanzania. Watu walipata huduma za jamii kwa pamoja kama vile shule maji na zahanati. Mliokaririshwa ubaya wa zoezi hili ndio mnaimba kama kasuku ubaya. Tuliobeba mizigo kwenda kwenye vijiji tunaihisi raha ya kushirikiana huko vijijini na kuwa karibu na huduma.
Marais wote waliofuata wamefuata lengo hili la ujamaa. Tatizo umekaririshwa ujamaa wa Karl Max na ndio unaoujua. Hata kuruhusu sekta binafsi kushiriki katika uchumi nao ni ujamaa. Kikubwa ni kumkinga mwananchi asinyonywe na wenye mtaji kimshahara,au kwa bei. Uwepo wa vyama vya wafanyakazi, na mamlaka za udhibiti wa watoaji huduma kama EWURA,TIRA, SUMATRA na nyingine nyingi ni uthibitisho wa taifa la kijamaa. Kipindi cha nyuma kulikuwa na tume ya bei. Taifa la kibepari hakuna hizi mamlaka hutegemea nadharia ya Adam Smith karne ya 17 juu ya kuacha biashara huru kwani kuna nguvu ya soko itaamua aliuita "invisible hand" itarekebisha. Mamlaka hizi hudhibiti wafanyabiashara wasiungane kupandisha bei.
Kwa kila unachokiona kinafanyka leo serikalini misingi yake ilianza toka enzi za Mwl Nyerere na huu ni wakati wa utekelezaji. Tunao amini kuwa wazo ndio uhalisia tunaendelea kumuona Mwl Nyerere katika haya yanayotendwa na viongozi wa sasa.