Tuna mfumo wa hovyo wa vetting ya kupata viongozi makini TanzaniaEti huyu naye aliapa kutumikia hiyo nafasi yake!
Mbona viongozi mnashindwa kutatua matatizo makubwa waliyonayo wananchi badala yake mnaruka kufanya kazi za ajabu ajabu.
Wanyassa wilaya yenu haina matatizo kumbe ni vimini na milegezo tu?
Na huko Mahakamni atataka wahukumiwe kwa sheria ipi? Hizi sio enzi za Magufuli watu walihujumiwa kwa "sheria" ya maagizo ya MagufuliMkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, amepiga marufuku mavazi yasiyo na staha ikiwemo vimini na suruali za milegezo wilayani kwake na amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Nyasa, kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote watakao vaa mavazi ya namna hiyo.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na kujibu kero za wananchi wa Kijiji cha Lulimbo wilayani humo, ambapo pia akakemea tabia ya wanaume wanaopiga wake zao na kuwataka wabadilike la sivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
"Wanyasa ni wastaarabu bwana, hata wakiwa wanacheza Mganda wanavaa nguo nyeupe na hazichafuki hata wakicheza masaa na masaa, nguo fupi na Milege Hazitakiwi wilayani Nyasa," amesema Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lulimbo
Safiii, bado wanaume wenye tabia za kike kusuka nywele na kuvaa hereniMkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, amepiga marufuku mavazi yasiyo na staha ikiwemo vimini na suruali za milegezo wilayani kwake na amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Nyasa, kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote watakao vaa mavazi ya namna hiyo.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na kujibu kero za wananchi wa Kijiji cha Lulimbo wilayani humo, ambapo pia akakemea tabia ya wanaume wanaopiga wake zao na kuwataka wabadilike la sivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
"Wanyasa ni wastaarabu bwana, hata wakiwa wanacheza Mganda wanavaa nguo nyeupe na hazichafuki hata wakicheza masaa na masaa, nguo fupi na Milege Hazitakiwi wilayani Nyasa," amesema Mkuu wa Wilaya.
View attachment 1905898
Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lulimbo