Nyama safi ya popo.....

Ama wanasema tembea uone mengi na never say never. Wakati sehemu nyingi katika bara la Africa tunawachukulia popo kama viumbe vinavyohusishwa na imani za kishirikina na hata muonekano wake tu ni wa kuogofya kwa baadhi ya watu, katika baadhi ya maeneo ya bara la Asia kama Indonesia, mnyama huyu anatumika kama kitoweo maridhawa kabisa hususan wale wnaoitwa fruit bats,unaambiwa ni watamu mithili ya kuku sekela. View attachment 785503View attachment 785505View attachment 785506View attachment 785507View attachment 785509View attachment 785510View attachment 785512
Hawa jamaa hawana tofauti na dog. WAcheki, utaelewa ninachomaanisha.
 
Sasa kama wamakonde wanakula panya!! kwani panya ana tofauti gani na popo?
 
Popo, nyani, nyoka, mamba ni kitoeo kizuri katika baadhi ya sehemu. Haya ndiyo yaliyonifanya nishindwe kuolewa West Africa
Kweli dada wee ulowa hapa hapa tu, huko kwingine unaweza kulishwa hadi machavichavi na popo tena popo mwenyewe popo bawa
 
Kuna watu wanakula kila kitu isipokuwa MAWE tu
Na mawe yangelainika wangeongeza chumvi na kula
Mnasema mmestaarabika wenzenu wanafakamia kila kitu
Tulikamata kenge wanne na jamaa akaanza kuwachinja kwa kweli huyu kiumbe alinitisha alipoweka kiganja shingoni kuzuia kisu lakini wote walikula kisu
Moto ukakokwa lakini cha ajabu nyama inatetemeka hata baada ya kupikwa sana.
Unapakuwa bado inatetemeka

Popo nimeona watu wakila ukitembelea Bangkok na Burma na Philippines utaona mama ntilie wanauza popo na pia kuna wale mende wakubwa sio wa chooni
 
Popo, nyani, nyoka, mamba ni kitoeo kizuri katika baadhi ya sehemu. Haya ndiyo yaliyonifanya nishindwe kuolewa West Africa
kuolewa na kula hayo majitu kuna uhusiano gani? mademu wa Bongo bwana full mashauzi
 
Back
Top Bottom