Nyakua Nyakitita: Mhadhiri DIT anayeokota makopo barabarani


Honky tonky guy.......sasa hivi kaiziria kabisa JF
 
Please wasiliana na ndugu zake. Jibu lipo. Sisi ni mashahidi wa mambo hayo. Apelekwe kwenye makanisa ya walokole ataombewa na kupona. Mimi napendekeza apelekwe kwa Kakobe au kanisa lililo karibu.

Nakumbuka wakati wa Nyerere walianza walokole wanajidai kuombea watu, Nyerere kama anavyojulikana alikuwa Mkatoliki swafi kabisa, akawaambia kama kweli si muende Muhimbili na Ocean Road kuna wagonjwa wengi yanini mnakaa na kupiga kelele Mnazi Mmoja. Hawajaonekana tena mpaka Nyerere anaachia ngazi.

Kwanini kama wapo hao waombaji na wanafanya kweli wasiende kupunguza msongamano wa wagonjwa mahospitalini?
 
PASCO umenikumbusha mimi nilisoma na NIA SUDI wewe ukiwa form 3 T baada ya kutoka form one na 2 ukiwa Z.
Darasa lote la form 3M lilikuwa vipanga wa kuotea mbali,hata hviyo kama unavyo nukuuu majority ended up
nowhere na hii kama unavyo kumbuka Mwl Kalimuna alitaka form 4 M yote ibaki palepale Tambaza baada ya darasa zima kuwa limefaulu kwa kiwangu cha juuu kabisa na ninaamini haijawawi tokea tena ufaulu ule,cha ajabu alipigwa mizengwe
huo mpango ukaishia hapo.Kumbuka ile timu ya ISSA JUMA,ATUBONE,KENETH,JONATHAN HAULE (AFISA) Prudecence Angello(R.I.P)AMBWENE just to mention a few.
Kweli vipanga huwa wanaishia patupu
 

Wagonjwa huwa hawana sadaka za kuwapa
 
Kuna umuhimu wa serikali kusaidia watu wote wanaofanana na huyu bwana
 
Duu Mkuu Upanga, umenikumbusha mbali, sikujua Prudence ni RIP!, mara ya mwisho alikuwa Mkurugenzi halmashauri fulani Moro!. Issa Juma alikuwa Tanesco Atu na Ambwene walikuwa bank!. Those good old days, wee acha tuu!.
Ila Mkuu Upanga, na wewe kumbukumbu yako pia sii mchezo!, huwezi amini mimi nilikuwa sikumbuki tena jina la darasa langu!. Nilifikiri vichwa ni darasani tuu, kumbe mpaka leo!. Mzee wa Upanga, wewe ndio Chief nini?.
Wengine nawakumbuka wako scatered sana. Patrick Kamera yuko Toronto, Peter Chagu Japan, kijana wa Ben karudi US, Philipo Mgaya yuko UK, wale wa hapa mjini, huwa tunakuna Ijumaa moja moja pale Calabash ni kwa Milton. Kama uko bongo, One day karibu tukumbushie zile good old days!.
 
Mfalme Suleman aliomba kwa Mungu kama hivi: (Usinipe utajiri hata nikakukufuru, usinipe umasikini hata watu wasiokujua wakakudhihaki. naomba unipe hekima nijue namna ya kuingia na kutoka kwa watu wako hawa ulionipa niwaongoze). Kumbe lilikuwa goli la kisigino, Mungu akampa hekima, na zidi ya hapo na utajiri juu. Akatesa na vimwana rasmi 700 pamoja na viconcubine 1000, akila ng'ombe 40 na mbuzi 100 kwa uchache kila siku. Mwacheni Mungu aitwe Mungu. Hajatokea tajiri kama yeye hata leo, twaambiwa hatokei tena ng'o! Ndo maana twaambiwa tunateseka sababu hatujui kuomba, na kama tunaomba basi twaomba vibaya ili tukipata tutumie kwa hila, basi Mungu akituangalia anatuhurumia na kutuepushia hayo mabaya kwa kutotupatia tutakavyo. "Eee Bwana tufundishe kuomba"- tusipojua udhaifu wetu na kushika adabu tukakubali kufunzwa kama mitume walivyoomba, tutaendelea kukatwa vichwa kadiri tunavyoinuka. Vita yetu sio ya mwili na damu bali ni vita ya ulimwengu wa rohoni, ambavyo anayevweza ni Mungu tu! Mfalme wa giza hataki tutese duniani mara mia kisha uzima wa milele, maana raha hiyo anaijua na amekataliwa kuipata tena!!!!
 
Mkuu za Leo, kwa kuongezea tuu, baba yake na Mfame Suleiman ni Mfalme Daudi, huyu Daudi, alimtamani mwanamke mrembo sana akiitwa Bathsheba, aliyekuwa ni mke wa jemedari wake mkuu aitwae Uria, ili ampate Bathsheba, akampanga njama za kumuua, akamtuma vitani ili afe, kweli Uria akauliwa vitani, huku nyuma Daudi naye kujitwalia huyo mjane wa Uria, Bathsheba na kumfanya mkewe ndipo akamzalia Suleiman!.

Nabii Suleiman alikuwa na wake 800 na masuria 200, jumla ni 1,000. Pamoja na utajiri na wake wote alionao, pia alipewa hekima kuliko watu wote na kosa lake ni moja tuu, tamaa ya kupenda "chini" kupindukia!, hivyo alipokuja kutembelewa na Queen of Sheba, akaomba na kukubaliwa, akapata nae mtoto!. Kwa vile huyu Queen Sheba, hakumwanini Mungu wa Israel, Mfalme Suleiman aliwehuka (alikuwa genius) na kutangatanga porini hadi mwisho wa maisha yake, na mali zake zote, zikapururwa na yule Queen of Sheba na zimehifadhiwa chini ya milima ya Abyssinia na ndilo chimbuko la Mashimo ya Mfame Suleiman!.

Daudi ndiye aliyeandika kitabu cha Zaburi, Suleiman aliandika Mithali wakati akiwa na busara, alipoanza kuendekeza tamaa ya "chini" akaandika "Wimbo Ulio Bora" na mwisho alipoanza kuwa insane, na kumuasi Mungu, akaandika kitabu cha "Mhubiri". Ukivisoma hivyo vitabu vitatu, Mithali na kumsoma Mhubiri, na Wimbo Ulio Bora, unaweza usiamini vitabu hivyo vyote vimeandikwa na mtu mmoja!

Pasco.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…