Nyakua Nyakitita: Mhadhiri DIT anayeokota makopo barabarani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyakua Nyakitita: Mhadhiri DIT anayeokota makopo barabarani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkurabitambo, Sep 9, 2012.

 1. M

  Mkurabitambo JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  WASWAHILI siku zote
  husema hujafa
  hujaumbika! Ukweli wa
  usemi huu unatimia
  unapomwona mtu
  huyu.
  Ungemwona miaka 13
  iliyopita ungeshangaa,
  lakini leo mtu aliyeitwa
  mstaarabu, bondia wa
  kutegemewa na mcheza
  twist wa ukweli, Nyakua
  Nyakitita amebadilika
  kweli.
  Mtu ambaye alikuwa
  mhadhiri wa
  kutegemewa katika
  Taasisi ya Teknolojia
  Dar es Salaam (DIT),
  msomi aliyebobea
  katika uhandisi, kazi
  aliyoianza katika miaka
  ya 1990, sasa anaishi
  kwa kuombaomba,
  kuchora ramani na
  mambo yasiyojulikana!


  Leo hii, msomi huyo
  yuko katika hali ya
  kusikitisha ya uchafu
  uliokithiri, anashinda
  karibu na maeneo ya
  chuo hicho makutano
  ya Barabara za
  Morogoro na Bibi Titi
  Mohammed huku
  akiokota makopo na
  takataka nyingine na
  mara nyingine
  akikusanya mawe na
  kuyapanga kwa
  kutengeneza michoro
  ya vitu mbalimbali
  ikiwamo ramani ya
  Tanzania na kuandika
  majina ya marafiki
  zake.
  Nini kilichomsibu hadi
  kufikia hapo?
  Kabla ya kupata
  matatizo ya akili
  mwalimu na mhandisi
  Nyakua aliishi maisha
  mazuri tu ambayo kwa
  vijana wa sasa
  wanasema, ‘yalimtoa’
  kwani alitembelea nchi
  kadhaa kwa ajili ya
  ziara za mafunzo au
  kozi ndefu na ambazo
  zilimpa fursa nzuri ya
  ‘kujirusha’.
  Watu walio karibu na
  mwalimu huyo
  wanasema alikuwa
  kijana mwerevu kweli
  kweli aliyefanya vyema
  katika masomo yake
  kote alikopita.
  Kaka yake, , Peter
  Murya, anasema mdogo
  wake alikuwa na
  mwanzo mzuri kimaisha
  tangu anazaliwa mpaka
  anapata shahada zake
  mbili.
  Anasema alikwenda
  kusoma nchini Urusi
  ambako alikaa kwa
  miaka saba na aliporudi
  alikuja akiwa na mke
  raia wa nchi ile (Urusi)
  ambaye walibarikiwa
  kuwa na watoto wawili.
  “Nadhani walifunga
  ndoa huko huko kwani
  walikuja tayari wakiwa
  na watoto wawili, wa
  kiume Paulus na wa
  kike Masha,” anasema
  Peter
  Anaongeza kuwa mdogo
  wake aliporudi kutoka
  Urusi aliajiriwa katika
  Shirika la Viwango
  Tanzania (TBS) na
  baada ya mwaka mmoja
  alipata mwanamke
  mwingine Mtanzania na
  hakutaka ushauri wa
  yeyote kuhusu suala
  hilo.


  Anapohojiwa zaidi
  kuhusu kilichomfanya
  awe katika hali hiyo
  Nyakua anajibu hivi:
  “Siasa za vyama vingi
  ndizo zilizonifanya niwe
  hivi. Nilimfanyia
  kampeni Rais Mkapa
  hadi akaingia
  madarakani, lakini
  hakunipa alichoahidi.”
  Anaongeza: “Nilitakiwa
  aidha niwe Ikulu, jeshini
  au kule kwingine.”
   
 2. v

  valid statement JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hajalogwa kweli huyo??,
   
 3. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu hata mimi nimewaza hivyo
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Ndugu zake wahangaike makanisani akaombewe sana kama kuna mkono wa mtu yataisha tu hakuna kurogwa milele mbele ya neno la Mungu,yatakimbia mapepo na majini yoote na atarudi kama kawaida akili zake kama hazijaaribika kabisa ataweza tena kuwa kawaida kabisa!!!wahangaike kwenye maombi!
   
 5. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  wampeleke kwa wataalamu watamshughulikia...
   
 6. F

  Funge JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 585
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Please wasiliana na ndugu zake. Jibu lipo. Sisi ni mashahidi wa mambo hayo. Apelekwe kwenye makanisa ya walokole ataombewa na kupona. Mimi napendekeza apelekwe kwa Kakobe au kanisa lililo karibu.
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Du inasikitisha, ndugu zake inamaana wamekubaliana na hiyo hali? Si wangemtaftia matibabu? So sad!
   
 8. u

  ukweli2 Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Nyakua huwa akitaka kuingia pale DIT haswa kantini (mangesho) huwa anazuiliwa na walinzi ila akibahatika kupita na kufika mangesho huwa anawaita kwa majina kabisa baadhi ya waalim na kuomba chochote kitu akipewa kama hajarithika nacho humtaja kabisa huyu mwalim aliye mpa na kumwambia wewe wa kunipa mimi kiasi hiki?niongezee (anataja jina la mhusika)
  huwa nashangaa kabisa,jinsi alivyo sasa inakuaje anakumbuka waalim wenzake?na kwa nn anapenda kukaa maeneo yae ya DIT?
   
 9. Mjanga

  Mjanga JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 1,245
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  ndugu Mkurabitambo unataka kutupa ujumbe gani?? hebu funguka vizuri!
   
 10. Change_it

  Change_it JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kuna siku nilipita maeneo ya DIT nilikuwa na rafiki zangu tukaona mawe mawe yamepangwa pembene kuna jamaa kalala kama vile kichaa, lakini ule mpangilio ilituwia vigum kuamini kwamba atakuwa chizi tukaanza kubishana kwasababu ule mpangilio wa mawe hauakuwa wawa kawaida kama vile umedizainiwa hivi, basi tukaondoka bila majibu na vile ndo tuko kwenye mji wenye vimbwanga vya kila aina tukaendelea na safari zetu tukukiwa na mshangao kwa mara ya kwanza kuona chizi akifanya kitu ambacho kwa kawaida huwezi kudhani. baada ya kuona hii thread ndo nikakumbuka.
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kuna mstari mwembamba sana unaotofautisha kati ya akili nyingi na uendawazimu. Inaonekana jamaa alikuwa nazo nyingi zikapitiliza. Kama walimu wenzake wapo kwa nini wasimchukue wampeleke Muhimbili au Mirembe akapate tiba ya afya ya akili badala ta kumuacha akihangaika hapo maeneo ya chuo?
   
 12. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  mleta mada mpaka sasa sijamuelewa ! Huyo mtu mimi nimemuona na hayo mawe nimeyaona, nilijiuliza maswali mengi kisha nikapuuza, kumbe nilikuwa sawa kuwa na doubt !
   
 13. M

  Mpalisya Imbogo Member

  #13
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ndugu zake wampeleke Jangwani grounds kuanzia tarehe 23 Sept mpka 30 Sept 2012 kutakuwa na maombezi ya wagonjwa. Pia wakiweza waende kanisa la ufufuo na uzima wampeleke huko au wakawaeleze wachungaji watawasaidia.
   
 14. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #14
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ni jambo la kusikitisha sana. Ndugu au rafiki zake wamsaidie kupata tiba ama Hospitali, makanisani au kwengineko ili mradi arudi katika hali yake ya kawaida.
   
 15. wiseboy

  wiseboy JF-Expert Member

  #15
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1,888
  Trophy Points: 280
  mtoa thread malisia basi, si umefungua mdomo, jaman sema usiogope...sema
   
 16. wiseboy

  wiseboy JF-Expert Member

  #16
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1,888
  Trophy Points: 280
  na kuna mwingine pale SUA anaye alikuwa profesa, huwa anakaa karbu na madarasa/ofice za soil science na pia karbu na library pale main compus, vp ilikuaje? kwa anae jua.
   
 17. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #17
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Anafanya kazi Usalama huyo itakua.
   
 18. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Tipping point ni wapi mkuu?
  Msatri mwembamba uko kati ya love and hate. Lakini "geniusness" and insanity mh, I don't believe!
   
 19. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #19
  Sep 10, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145

  Aisee, hii taarifa ndio inanifumbua macho. Mara kwa mara napita hapo na ama kumwona yeye mwenyewe au kuona kazi zake au vyote viwili lakini sikujua historia yake. Lakini kila nikipita nilikuwa nashangaa ueledi wa kisanii alio nao. Kumbe kuna siri kubwa nyuma yake. Serikali sijui kama inawaona watu hawa na laiti wangekuwa na sera ya kusaidia watu wa namna hiyo. Wamelitumikia Taifa kwa uaminifu sana, kama kuna makosa ndio tafsiri ya ubinadamu tu.

  Unanikumbusha daktari mhadhiri wa MUCHS ambaye anaimba nyimbo na kuchezacheza pale stendi ya daladala Muhimbili, daktari wa ukweli na mwalimu mzuri anayewashauri wanafunzi wa MUHAS kwa weredi hadi sasa, akimwambia mwanafunzi "umekosea, fanya hivi" asiposiki kweli anafeli, akifuata ushauri wanapasi. Anakumbuka shule ya medicine hata sasa na kuwapa tuition wanamshangaa na sasa amekuwa rafiki yao sana. Aliosoma nao wamestaafu wakiwa maprofesa. Wasiomjua wanamwangalia kwa dharau.

  Yupo Engineer mwingine aliyekuwa anatembea akipima barabara ya United Nations na kuchorachora. Naishiwa maneno. Mungu tu peke yake na awafungue sasa, maana kama cha moto wameshakiona, na sasa wanahitaji kubadilisha upepo wa maisha.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,568
  Likes Received: 18,313
  Trophy Points: 280
  Nyamgluu, watazame wa genious wa ukweli, angalia life style zao, angalia dressing zao, angalia smartnes zao utanotice kuna jambo!. Wengi mnamfahamu Profesa Shaba!. Kwanza ma genius wengi wa ukweli, hawanaga maisha marefu!.

  Nikiwa Tambaza tulikuwa na genius wetu akiitwa Nia Sudi, jamaa alitoka familia duni akiishi Msasani Mkikoroshini nyumba ya udango, haina umeme, alikuwa hasomi mwalimu akifundisha yeye alikuwa akitetemesha tuu mguu, mtihani wa form VI, alipiga point 7 na alikuwa na A-9!, akachaguliwa Kibaha na safari yake ikaishia pale!, kwanza alichanganyikiwa, then aliugua and passed away! RIP NIA SUDI!.

  Kuna vipanga wengine wawili hapo hapo Tambaza waliokuwa mbele yetu, Mustapha Kudra na Elhanan Elirehema Mushi, wote hawa walimazina form VI na point 7, by now lazima wangekua mahali visible, ukiserch, hukuti feed back yoyote kwenye majina yao in such a way one is not sure if they are still alive!.

  Kuna familia moja ya kigogo maarufu nchini, ilikuwa ikiishi pale anapoishi VP. Watoto wa 6 wa familia hiyo wote ni vipanga, mkubwa alisoma Tambaza, akatoka na I ya 7 o-level na 1 ya 3 A level, akaripoti UDSM, he died on the car accident akiwa mwaka wa 2!. Mdogo mtu wa kike alipiga Medicine Muhimbili, akajiua akiwa mwaka wa 4!. Waliomfuatia wawili ni wakike mmoja kwa sasa ni Daktari na Mkurugenzi wa taasisi muhimu nchini na mdogo mtu ni Jaji wa Mahakama Kuu. Last born wao ni mvulana he died misyterious death at the age of twenties!. Familia hiyo ina bahati mbaya kwani mzee huyo ana mtoto mkubwa wa kiume aliyezaa nje ya ndoa, I'm not very sure kama ni mzima upstairs!.

  Mkifuatilia maisha ya ma genius hata wa historia, angalia waliishije na walikufaje, Jesus, Newton, Galileo Galilei, Archmedes, Socrates na Plato etc.

  Pasco.
   
Loading...