Nusu siku ndani ya jeneza

Nusu siku ndani ya jeneza

Mzizimkavu hii story uliyo leta humu ina mafunzo ya kweli, na chakushangaza huyo kiumbe anatamani kutubu ila ndo hawezi tena, ila sisi uku tuna nafasi hiyo twaichezea. Kingine hii story inavyo muongelea mwanamke, si kwa ubaya ila maandiko yamesema we mwanaume ishi na mwanamke kwa akili, huyu kiumbe kama anavyo itwa ana nini mpaka tukae nae kwa akili hivyo? Ila asante sana nasubiri hiyo jioni unipe mambo zaidi...
 
NUSU SIKU NDANI YA JENEZA -11-

ILIPOISHIA JANA:
Niligeuka kuangalia pa kukaa, nikaona kiti kingine kidogo lakini kizuri sana, cheupe, nikakaa kwa kujiachia.
ENDELEA MWENYEWE

"
Unajijua?" yule kiumbe aliniuliza.
"Ndiyo."
"Unajijuaje?"
"Mimi ni binadamu."
"Siyo kweli."
"Siyo kweli kivipi?"
"Kuna ubinadamu baada ya kifo?" aliniuliza.
Nilibaki kimya. Yeye akaendelea:
"Binadamu ni uhai, ukishakufa si binadamu tena unakuwa maiti, mfu au marehemu. Wewe umewahi kusikia watu wakisema binadamu huyo atazikwa kesho?"
Nilitingisha kichwa kuashiria kwamba alichosema ni kweli, akaendelea:
"Je, umewahi kusikia wakisema binadamu huyo atasafirishwa kwenda mahali kwa mazishi?"
Pia nilitingisha kichwa kukataa kwamba sijawahi kusikia.
"Kwa hiyo ubinadamu ni uhai, baada ya kifo hakuna ubinadamu?"
"Ndiyo," nilimjibu.
"Ndiyo maana nilikuuliza unajitambua? Ukanijibu ndiyo, wewe ni nani ukasema ni binadamu. Wewe si binadamu kule si ulishakufa au hujaambiwa?"
"Nimeambiwa."
"Kwa hiyo wewe ni maiti?"
Nilisita kumkubalia, lakini mwishowe niliamua kukubali tu. Nilisita si kwa sababu si kweli bali kwa vile niliona ni jambo zito sana mimi kuitwa maiti. Maiti inatisha, maiti inaogopwa, huwezi kulala na maiti hivihivi tu hata kama marehemu alikuwa mke au mumeo.
Yeye kama alijua, akasema:
"Nyinyi binadamu mna jambo moja la ajabu sana. Huwa hamuamini maandiko yenu wenyewe. Ukiitwa maiti unaogopa, lakini si ukweli kwamba baada ya kifo ni&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];"
Mimi nikadakia nikasema hukumu. Nikiwa na maana kwamba baada ya kifo hukumu ndiyo andiko nililoanza kulijua mapema sana kwenye maandiko.
"Siyo mauti. Baada ya kifo ni maiti. Mtu ukishakufa tu unakuwa maiti."
"Sisi kwenye maandiko yetu tunajua baada ya kifo hukumu."
"Ni sawa kabisa. Lakini sisi huku tunajua hukumu ipo tangu kuzaliwa kwako maana maisha yameshajulikana hata hujaanza kuishi, ila baada ya kifo ni maiti. Na mtu akishakufa hajui kitu."
"Hajui kitu kivipi?" nilimuuliza.
"Hajui kitu kwa maana kinachoendelea."
"Ha! Mbona kuna elimu kule duniani inasema mtu akishakufa anasikia kila kitu ila kusema ndiyo hawezi?"
"Umewahi kulala usingizi wa fofofo?"
Nilimkubalia kwamba nimewahi.
"Unaweza kusikia kitu?"
"Hapana."
"Sasa kufa ni mara mia zaidi ya kulala usingizi mzito. Jifunzeni sana. Roho ikishatoka kinachobaki ni mwili na ubinadamu haupo tena."
"Kwani roho ni nini?" nilimuuliza.
"Roho ndiyo nafsi."
"Na nafsi ni nini?"
"Uhai."
"Uhai ni nini?"
"Unajua uhai wa binadamu upo kwenye damu. Humo ndimo mwenye nafsi. Ndiyo maana mtu akimwaga damu nyingi hawezi kuishi tena."
Yule kiumbe aliyeonekana mwenye uwezo mkubwa wa kuzungumza aliendelea kusema:
"Maandiko yenu yanaweka wazi kila kitu kwamba damu ndiyo nafsi, damu ndiyo pumzi. Moyo unaporusha damu mwilini na kuvuta ndipo mtu anapopumua au mnasema kuhema.
"Mungu wenu katika maandiko ameweka wazi mambo mengi sana kuhusu damu na uhai au nafsi. Ukisoma kwenye sheria za vyakula, kuna wakati Mungu wenu alikataza watu wasile nyama fulani, halafu baadaye akaruhusu wale.
"Alikuwa akikataza na kuruhusu kwa misimu, lakini wakati wote Mungu wenu amekataza ninadamu msinywe damu kwa kuwa humo ndimo mwenye nafsi ya mtu."
Aliposema hivyo nilishtuka kidogo kwani ninavyojua mimi kuna kabila nchini mwangu linakula damu ya wanyama. Nilishindwa kuuliza, lakini yule mtu akaendelea kusema:
"Ukikuta mtu anapenda kunywa damu hata ya mnyama, mara nyingi katika maisha atakumbwa na tabia ya kufanya maamuzi ya ajabu yenye vitendo visivyokubalika."

Ili kujua zaidi usikose kusoma usiku mwingi.....
 
Ni hadithi tu. Kama zile shuhuda za uongo za watu wanaodai kufufuka kwenye redio za dini.

bwana yesu asiyatie mhuri maneno yakinywa chako maana huyo shetani unae mpinga atakua mshitaki wako maana imeandikwa watatoa pepo watafufua wafu kwa jina langu lkn pia imeandikwa sio wote waniitao bwana bwana watauona ufalme wa mbinguni na kumbuka wapo mpinga kristo na usisahau ya kwamba tunamacho lkn hatuoni tuna masikio lkn hatusikii maana mambo hayo yamefunuliwa kwao watoto wachanga hakika ndugu yangu omba sana yesu asiyatie mhuri maneno yako kwa maana hata sasa hatumjui mkweli ni yupi tusihukumu kabla hatuja hukumiwa maana kazi ya kuhukumu sio ya kwetu
 
Mzizimkavu hii hadithi japo ni ya kutunga lakini ina facts nyingi ambazo ni za kweli. Nimpe hongera nyingi mtunzi wa riwaya hii. Na yaliyoelezwa humu yatawafungua na kuwaponya watu wengi sana hasa kama mtu atasoma na kutafakari kwa umakini. Ziwa la moto lipo kwa watenda dhambi wote pasipo kujali dini wala rangi zao. Ufafanuzi uliotolewa kwamba Jehanum ni sehemu iliyokuwepo nje ya mji wa Yerusalem enzi hizo kwa maana sehemu ya kuchomea takataka za mji ni kweli kabisa!! Lakini pia neno la MUNGU - BIBLIA imeweka wazi mambo mengi yanayozungumzwa humu na mengineyo, tatizo binadamu tumekuwa wavivu kusoma na kulitafakari neno. Na hii ni kwa sababu ya mungu wa dunia hii kutubana kwa kutunyima nafasi hiyo kwa kisingizio cha kazi na ugumu wa maisha. Aidha, kwa yeyote anayesoma uzi huu, suluhisho ni kumpokea BWANA YESU tu awe mwokozi wa maisha yako. Yesu yule ambaye hata mapepo huku kuzimu yanaogopa hata kutaja jina lake tu!! Vinginevyo waovu watageuka kuwa sehemu ya kuni za jehanamu.

Tuendelee MziziMkavu tunasubiri kuona mwisho wa huyu ndugu kwenye hiyo safari yake ya maono. I guess aliweza kurudi duniani maana tusingweza kusikia hizi shuhuda!
 
NUSU SIKU NDANI YA JENEZA -12-

ILIPOISHIA :
"Alikuwa akikataza na kuruhusu kwa misimu, lakini wakati wote Mungu wenu amekataza binadamu msinywe damu kwa kuwa humo ndimo mwenye nafsi ya mtu."
Aliposema hivyo nilishtuka kidogo kwani ninavyojua mimi kuna kabila nchini mwangu linakula damu ya wanyama. Nilishindwa kuuliza, lakini yule mtu akaendelea kusema:
"Ukikuta mtu anapenda kunywa damu hata ya mnyama, mara nyingi katika maisha atakumbwa na tabia ya kufanya maamuzi ya ajabu yenye vitendo visivyokubalika."
SASA ENDELEA

"
Kama vitendo gani?"
"Vingi tu. Kama vile kuua, kudhuru, kuharibu, kutukana. Mara nyingi kutukana huku kunakuwa hadharani. Pia unaweza kushangaa mtu anakuwa na tabia ya kupenda sana kitu fulani."
"Da! Nimejifunza mengi sana."
"Bado hujajifunza, hapa umeletwa ili ujifunze mbinu inayotumika kuua watu duniani. Hii mbinu tunataka wewe ndiyo uende ukaisambaze kwa dunia ukiwa mwalimu wa mbinu hiyo lakini nguvu yote itatoka kwetu.
"Sasa hivi niliposema kaa lengo langu nianze kukupa hiyo mbinu ili sisi tuweze kuvuna wanadamu wengi katika kipindi hiki ambacho dunia itafikia mwisho wakati wowote ule."
"Kwani hata wewe hujui mwisho wa dunia ni lini?"
"Najua."
"Ni lini?"
"Kha! Mbona hata wewe unajua ni lini!"
"Mimi sijui, kwenye vitabu vyetu tuliambiwa hakuna anayejua siku ya mwisho wa dunia, hata malaika wa mbinguni."
"Ni kweli lakini maandiko hayohayo yameweka wazi ishara ya siku za mwisho na ishara hizo zote zinaonekana sasa au nasema uongo?"
"Ni kweli."
"Kwa hiyo unakubali kwamba hata wewe unajua kuwa dunia imefikia mwisho?"
"Kweli nimejua."
"Sasa tunataka kukutuma duniani, kazi utakayotakiwa kuifanya ni pamoja na kuhakikisha kila siku unaua binadamu zaidi ya mia moja."
"Hee! Niue binadamu wenzangu?" niliuliza kwa mshtuko nikataka kusimama.
"Kijana tulia. Unatakiwa kufuata maagizo yetu."
"Sijawahi kuua na kuua ni dhambi kubwa sana."
"Kwani kuna dhambi ndogo?" aliniuliuza kwa sauti ya ukali.
"Najua hakuna, lakini kuua mtu dhamira inauma sana kuliko nikimwibia mtu."
Aliniangalia kwa karibu dakika moja halafu akageuka pembeni na kumwangalia kiumbe mwenzake mmoja ambaye alikuwa kama msaidizi wake, akasimama na kunisogelea.
Aliponifikia aliweka mkono wake juu ya kichwa changu, palepale nikajikuta niko kwenye kundi la viumbe wengi lakini kuna kiongozi mmoja mkubwa ambaye alikuwa akitoa maagizo fulani.
Alikuwa amesimama akamnyooshea kidole kiumbe mmoja akimwambia:
"Wewe lazima ukamuue kwa ajali leo hii Alia, yule mfanyakazi wa kampuni ya madini, muda huu yupo kazini. Halafu si unajua yule wakati wa kulala au akiamka huwa hasali kwa Mungu wake? Kwa hiyo ni mwepesi sana.
"Unachotakiwa kufanya, nenda nyumbani kwake kampige ugonjwa wa ghafla mkewe na umwangushe chini halafu ashindwe kusema. Yule mtoto wake mkubwa atampigia simu baba yake.
"Sasa baba akiambiwa mkewe kaanguka na hawezi kuongea, itabidi atoke ofisini haraka na ataendesha gari kwa spidi sana.
"Halafu uende pale Kituo cha Mabasi cha Faya, mwamuru dereva mmoja wa daladala aondoe basi kwa kasi ukimpiga upofu asione vizuri mbele, akifika kwenye makutano ya Barabara ya Faya na Morogoro apite bila kuangalia taa, Alia naye atakuwa ameshafika pale na taa zitamruhusu apite, watakutana na ajali itatokea, Alia atakata roho palepale, sawa?"
Kile kiumbe hakikujibu sawa, ila kilisimama wima kikainamia mbele kama ishara ya kumtii kiongozi wake, akafutika mbele yetu. Niliogopa sana kusikia mpangilio ule.
Kumbe ilimaanisha kwamba, ajali inapotokea inakuwa imepangwa na pepo wachafu tena kwa mpangilio wa ajabu, kwamba ajali ianzie wapi na kuishia wapi! Ina maana Alia hakujua kama kule kupigiwa simu kuwa mke wake kashikwa na ugonjwa wa ghafla ndiyo ilikuwa tiketi ya sababu ya kufa kwake.
Kama angejua angetoa amri akimbizwe hospitalini halafu yeye atafuata huko polepole.
Baada ya yule kufutika, yule kiongozi akiwa bado amesimama akamnyooshea kidole kiumbe mwingine, akamwambia:
"Wewe! Kwanza simama."
Yule kiumbe akasimama kwa utii wote huku akimwangalia yule mtoa amri. Mtoa amri akaendelea:
"Nataka ukasababishe ajali mbaya ya lori na basi. Ajali hii nataka itokee Barabara ya Chalinze-Morogoro. Unachotakiwa kufanya, wakati basi linatokea Morogoro kwenda Dar es Salaam, wewe toa malori mawili Chalinze kwenda Morogoro.
"Yale malori yataanza kufukuzana mpaka yanapokaribia kukutana na lile basi, mpige upofu dereva wa lori la nyuma, aamue kumpita mwenzake bila kuangalia mbele na wakati huohuo mfanye dereva wa basi aongeze spidi mpaka kukutana uso kwa uso na ajali itokee.
Utakachotakiwa kukifanya baada ya ajali ni kukusanya damu za watu watakaoumia, lakini usiue maana leo letu ni damu ya binadamu, si mnajua tuna sherehe mwisho wa mwezi huu?
"Basi harakisha ili kitengo cha damu kiwe na akiba ya kutosha, watu waumie sana, wavunjike miguu, mikono, wapasuke vichwa lakini usitoe roho ya hata mmoja wao.
Yule kiumbe naye akainama kwa ishara ya unyenyekevu na kufutika mbele ya macho yangu. Nilianza kujiuliza ina maana katika maelekezo yale itafika zamu yangu?
Kisha yule mkubwa wao akaangalia huku na kule mpaka mimi akanipitia na jicho lake moja tu lililo kwenye paji la uso, akaniambia:
"Wewe, simama kwanza."
Nikasimama huku nikitetemeka moyoni nikijiambia sitakubali kutumwa kwenda kuua wala kusababisha ajali.

Ili kujua zaidi usikose kusoma leo jioni nisiwachoshe sana....
 
SASA ENDELEA…

"Kama vitendo gani?"

mzizi mkavu,tupia tu kwani sasa hivi sio jioni?kwani jioni mpaka jua lizame?
 
bwana yesu asiyatie
mhuri maneno yakinywa chako maana huyo shetani unae mpinga atakua
mshitaki wako maana imeandikwa watatoa pepo watafufua wafu kwa jina
langu lkn pia imeandikwa sio wote waniitao bwana bwana watauona ufalme
wa mbinguni na kumbuka wapo mpinga kristo na usisahau ya kwamba
tunamacho lkn hatuoni tuna masikio lkn hatusikii maana mambo hayo
yamefunuliwa kwao watoto wachanga hakika ndugu yangu omba sana yesu
asiyatie mhuri maneno yako kwa maana hata sasa hatumjui mkweli ni yupi
tusihukumu kabla hatuja hukumiwa maana kazi ya kuhukumu sio ya
kwetu
mpaka leo hujui unaamini nini? kweli imani haba wewe endelea kuamini tu hizi comedy sticky katika neno la MUNGU kwa njia ya YESU KRISTO
 
NUSU SIKU NDANI YA JENEZA -13-

ILIPOISHIA JANA USIKU:
Utakachotakiwa kukifanya baada ya ajali ni kukusanya damu za watu watakaoumia, lakini usiue maana lengo letu ni damu ya binadamu, si mnajua tuna sherehe mwisho wa mwezi huu wa nne?
"Basi harakisha ili kitengo cha damu kiwa na akiba ya kutosha, watu waumie sana, wavunjike miguu, mikono, wapasuke vichwa lakini usitoe roho ya hata mmoja wao.
Yule kiumbe naye akainama kwa ishara ya unyenyekevu na kufutika mbele ya macho yangu. Nilianza kujiuliza ina maana katika maelekezo yale itafika zamu yangu?
Yule mkubwa wao aliangalia huku na kule mpaka mimi akanipitia na jicho lake moja tu lililo kwenye paji la uso, akaniambia:
"Wewe, simama kwanza."
Nikasimama huku nikitetemeka. Moyoni nilijiambia sitakubali kutumwa kwenda kuua wala kusababisha ajali.
SASA ENDELEA:

Yule kiumbe aliniangalia kwa muda wa kama dakika moja nzima, haongei kitu wala hapanui kinywa. Baadaye akasema:
"Nitakupa kazi. Kaa kwanza."
Nilikaa huku macho yangu yote yakiwa kwake.
Akamsimamisha mwingine akisema wewe pale, simama haraka sana.
Niligeukia kule alikoelekeza kidole yule kiumbe mkubwa nikamwona kiumbe mwingine akisimama kwa utii wote.
"Nenda kasambaze uwezo mdogo kwa wanawake wajawazito kujifungua wenyewe hadi wafanyiwe upasuaji. Naona kuna kampeni ya wajawazito kujifungua salama, mimi sikubaliani nayo, lazima katika kila wanawake wajawazito kumi, wanane wajifungue kwa kupasuliwa ndiyo lengo letu la mwaka huu. Hakikisha mikono ya madaktari inakuwa na uharaka wa kufanya kazi hiyo."
Bado nilikuwa nimemkazia macho yule kiumbe aliyekuwa akipewa mwongozo, aliinamisha kichwa kwa utii, akapotea mbele ya macho yetu. Sasa nilijua inakuja zamu yangu ingawa bado mle ndani mlikuwa na viumbe wengi.
Aliniangalia kwa kupitisha macho yake kwangu lakini mwisho yakaenda kutua kwa kiumbe aliyekaa pembeni yangu, akamwambia asimame. Yule kiumbe akasimama.
"Ile meli uliipinduaje?"
"Ile iliyoua abiria wengi?" yule kiumbe alimuuliza mkubwa wake.
"Unataka nikujibu nini?"
"Nilipeleka mawimbi makubwa baharini, bahari ikasukwasukwa na upepo mkali hadi meli ikapinduka na kuzama."
"Serikali ikasemaje?"
"Serikali ilitoa tamko kwamba kuchafuka kwa bahari ndiyo kulisababisha ajali na watu, hasa wavuvi wakatakiwa kuchukua tahadhari katika kipindi hicho,."
"Ohoo! Kwa hiyo serikali haikujua kama sisi ndiyo tulisababisha?"
"Haikujua mkuu, ilijua ni upepo mkali wenye mawimbi makubwa."
"Safi sana, kaa nitakupa kazi."
Akakaa kwa heshima zote.
Nilijiuliza maswali mengi. Hiyo meli wanayoisema ni ipi, ni ya Tanzania au? Maana Tanzania nayo kuna ajali za meli kama tatu zilitikisa. Kuna MV Bukoba, MV Skagit na MV Spice Islanders.
"Vurata," aliita yule kiumbe mkubwa. Ndiyo nikajua kumbe nao wana majina. Sikuwahi kusikia. Alisimama kiumbe mmoja wa ajabu kuliko wenzake wote. Yeye masikio yalipita kichwa hata ya sungura hayaoni ndani, alikuwa mweusi sana, ni sehemu za macho tu ndiyo alionekana vyema. Midomo yake ilikuwa ya duara kama sehumu wa juu ya kikombe cha chai.
Shingo yake ilikuwa ndefu kama vile mtu alitundika kichwa chake kwenye mti ulionyooka. Aliposimama akawa anajibinuabinua shingo na kutoa ulimi mweupe kama karatasi na mrefu mfano wa kujiko kikubwa.
Nilimwogopa sana, maana kama alinijua vile, kila wakati alikuwa akiniangalia mimi na kuachia tabasamu ambalo lilizidisha ubaya wake kuliko alipokuwa hatabasamu. Huyo ndiye Vurata. Mkuu wake akamwangalia kisha akauliza:
"Umerudi lini Vurata?"
"Jana usiku," alijibu kwa haraka sana.
"Safi sana. Nipe matokeo," alisema mkuu wao kisha akacheka na kuniangalia mimi huku akijitapa:
"Sisi huku tunashughulika na vitu vingi sana vingine kama havina maana lakini kwetu vina maana. Enhe, nipe matokeo."
"Matokeo timu ya Yanga imeifunga Simba bao moja kwa bila."
"Mfungaji nani?"
"Anaitwa Tegete."
"Dakika ya ngapi?"
"Ileile ya sabini kama ulivyotaka mkuu."
"Ulifanyaje?"
"Ile timu nyekundu ilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kushinda maana mtaalam wao alikuwa mzuri, lakini nilipofika uwanjani niliwanyong'onyesha miguu ikawa mizito."
"Vurugu ulizituliza?"
"Ndiyo mkuu."
"Sasa hakikisha kila mwaka upinzani unakuwa mkali kwa timu hizi. Sitaki moja iwe juu ya mwenzake kwa sababu ikitokea hivyo mashabiki watapungua na sisi lengo letu mpira uendelee kuwa na mashabiki wengi kuliko wanaokwenda kanisani."
"Hilo halina shida mkuu."

Ili kujua zaidi usikose kusoma usiku mwingi.....
 
Back
Top Bottom